Je, unajua namna ya kusave faida kwenye duka au biashara nyinginezo ndogo ndogo?

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
360
386
Kiujumla duka litakupa faida pale tu mzunguko wa mauzo unapokuwa mkubwa, Mzunguko utakuwa mkubwa pale tuutakapohakikisha mteja hakosi kitu dukani kwako. Ujanja ni kuuza vitu vyote ambavyo eidha maduka mengine Hawsuzi mfano sindano za viatu ,cherehan, za mikono, Huu ni mfano tu Ila vipo vingi ambavyo unaweza kuwa mbunifu zaidi
Location

Ili uweze kuongeza mauzo ni lazima utafute sehemu nzuri pia yenye mzunguko mkubwa wa watu mfano wapabgaji au wapita njia wengi

Mfano
Mtaan kwangu Kuna duka linauza mauzo kwa siku laki 4 Hadi laki 8 siku za weekend
Ukiona duka lenyewe Sasa limeshona kila kitu
Na anafungu mapema na kulala kwa kuchelewa

Tuje hapa kama anauza laki 4 kwa siku anasave elfu 40 kila siku na Kodi na mambo mengine yote anatoa dukani hayahisiani na hiyo aliyotoa Mtu kama huyo kwa mezi atakuwa na 1,200,000 kwa mwaka atasave 14,400,000 Duka ukilipenda litakupa faida kubwa sana Shida yetu kubwa ni kuzarau au kufanya duka kama store ya familia ukiishiwa sukari unachukua tu hulipi mafuta, unga nk hivyo huwezi kuona faida

Pia tunafungua muda tunaotaka na kufunga tunavyotaka Pia kila mtu ni muuza duka siyo dada wa kazi siyo watoto wa ndugu zako siyo baba Wala mama Hivyo tunakosea mbona hatutumi dada wa kazi aende ofisini kwako kwa niaba yako? Au mbona huondoki kazin kabla ya muda?

Duka ni kazi kama zilivyo kazi nyinginezo Tuliwekee mfumo maalumu wa kiuendeshaji Ukiwa na maduka 2 na ukayasimamia vizuri utaenjoy maisha!!!

Biashara ya genge
Biashara ya genge ni biashara ya kipato kinachokidhi


Enapo utapata location nzuri
Ukiwa na mtaji wa milion 1
Unaweza kuanzisha genge tena lenye vitu vingi
Kikubwa uheshimu kazi yako na kuipa thaman
Kuipa muda maalumu wa kuifungua na kuifunga kwa muda maalum,
 
Uko sahihi....Kuna jamaa mmoja...ni bwasheee...mrombo yupo Dar...anakomaaa mwenyewe dukani....ni duka genge....kwa nyuma anauza vinywaji.....hakuna kitu utakosa dukani....hata ukija usiku wa maanani 9 hivi...kidirisha kipo wazi..." bwashee nataka fegi".....ana reply faster.....fegi unapata bwasheee🙂🙂🙂
 
Uko sahihi....Kuna jamaa mmoja...ni bwasheee...mrombo yupo Dar...anakomaaa mwenyewe dukani....ni duka genge....kwa nyuma anauza vinywaji.....hakuna kitu utakosa dukani....hata ukija usiku wa maanani 9 hivi...kidirisha kipo wazi..." bwashee nataka fegi".....ana reply faster.....fegi unapata bwasheee
Muulize anasave sh ngapi utashtuka kama siyo anasave faida ya laki au laki na ishirini kwa siku
 
Back
Top Bottom