Baadhi ya biashara zinazohitaji mtaji mdogo kuzianzisha na baadaye kuzikuza kuwa kubwa zaidi

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,171
Habari wakuu kwa mujibu wa ratiba yetu leo

Tunajadili Fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo unaweza kuzifanyia kazi ndani ya nchi yetu kulingana na Mazingira uliopo.

Wakuu kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira na salary au kipato kutokukidhi kwa wale wenye ajira, naona Ni vema tukashirikishana Kila Aina ya Fursa inayoonekana au kupatikana 🤝🤝

Kwa leo tuangalie biashara unazoweza kuanzisha kwa mtaji mdogo.🤏👌👌

Kwanza kabisa hakuna biashara ndogo Ila kila biashara unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka kufikia maono yako💪💪

Naamini hata kwa wale wenye Ajira bado Kuna maono yako unayo ya kukuongezea kipato Chako au kuweza kupata Uhuru wa kiuchumi
💪💪💪
Kwa wenye Ajira hapa lazima upate kijana mwaminifu ufanye naye kwa muda ukisubiri ukuaji wa biashara yako iweze kukuajiri mwenyewe na wengine.

1. BIASHARA YA BITES/VITAFUNWA
Hivi Ni vitafunwa unaweza kutengeneza Kama crips, sambusa, chapati, maandazi, mihogo ya kukaanga, vitumbua, karanga za mayai, ubuyu, korosho, visheti etc unaweza sambaza vitafunwa maofisini as package kwamba pack moja ina andazi, sambusa, chapati na kachori au ukauzia nyumbani, moja ya vitafunwa hivyo. Bites pia unaweza peleka kwenye maduka na supermarket, faida yake huwa nusu kwa nusu ya mtaji unaoutoa.

2. BIASHARA YA VINYWAJI BARIDI STENDI ZA DALADALA
Hapa utahitaji Deli au Ndoo uweke VITU vya kutunza baridi Cha kufanya, nunua mabarafu, nunua vinywaji, tafuta kijana au wewe mwenyewe uza stend za daladala, mwanzo mgumu Ila ukikaza inalipa.

3. BIASHARA YA UJI WA ULEZI, UJI WA MCHELE NA MAKANDE
Kodi toroli, jaza chupa zako za uji aina zote, tembeza kwenye magereji na sehemu za bodaboda, unaweza tembeza mwenyewe au ukampa kijana faida ni mara mbili ya mtaji ukitumia elfu kumi, jua utapata elfu 30. Kuna baadhi ya watu wanaidharau sana hii biashara lakini ina faida sana, jaribu ujionee maajabu.

4. KUNUNUA KUPACK DAGAA NA KUSAMBAZA MADUKANI NA MAJUMBANI
Hawa dagaa wanapatikana masokoni, hawa wanakua hawana mchanga kabisa, unanunua vifuko unapack unauza mtaani au madukani kwa Bei ya jumla. Kuna dagaa wa Kigoma, Zanzibar au Mwanza waliokaangwa.

5. BIASHARA YA MATUNDA

Watu wengi wanapenda kula matunda wakati mchana andaa kwa usafi matunda yako hapa, unaweza tumia elfu kumi tu.

Unaweza kununua matunda mchanganyiko katika soko lolote linalouza matunda then nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda, pack matunda yako ambapo yakiuzika vyema unapata faida nzuri.

Hayo ni mawazo yangu Karibu kushare mawazo zaidi.
 
Vinywaji
emoji91.png
VINYWAJI gani mkuu, maana Kuna ambacho mtaji wake mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom