ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,579
- 44,825
Wafanyakazi tumenongwa sana tuache kutegemea single source, yaani hela za makazini tujiongeze kidogo na shughuli nyingine. Yaani kweli mtumishi inafika tarehe mshahara hujatoka unakosa hata 5000 aisee hii sio sawa kabisa kwanza yafaa katika account yako pasikose million 1 walau kidogo ili ikitokea hata dharura fasta unaisolve japo pesa ya kijinga sana sijui kwanini haitaki kukaa mfukoni.
Sasa mimi nimekuja na products ambazo ni rahisi kuzitengeneza hata ukiamua umetoka zako kazini ukiwa nyumbani unazitengeneza kisha unazisambaza madukani mnakubaliana na mwenye duka jinsi mtakavyogawana pesa na hasa bidhaa nzuri ni zile ambazo hata zikikaa muda mrefu dukani haziharibiki.
1. Juice za matunda: Hizi usiku unatengeneza hata lita tatu tu unaziweka kwenye friji asubuhi unampelekea mtu dukani unampa na vi take away, atleast hata akipata faida ya Tsh. 5,000/- mpe hata Tsh. 2,000/- utakuwa hujapoteza kitu kwa mwezi hukosi Tsh. 90,000/-.
2. Karanga za kukaanga: Hizi ni dakika chache unakaanga na kuzifunga katika packages unasambaza maduka yasikuwa nazo, hata ukipata faida ya Tsh. 20,000/- kwa mwezi ni safi kabisa.
3. Visheti na kashata: Hivi ni kama karanga tu, hata ukipata faida ya Tsh. 7,000/- kwa mwezi sio mbaya.
4. Icecream na ubuyu: Hii ukimpata dogo mmoja akawa anawauzia wanafunzi shuleni si ajabu ukapata faida mpaka ya Tsh. 25,000/-.
5. JIK: hizi unanunua bei ya jumla Dar unazipack kwenye vichupa unauza hata maofisini kwenu, sio mbaya ukipata hata faida ya Tsh. 10,000/- kwa mwezi.
6. Showergel, sabuni za kipande, sabuni za maji, za unga: Zote hizi ukiamua kuacha usingizi mmoja tu usiku unatengeneza na usazambaza sample chache.
7. Ufugaji wa kuku wa mayai wa kienyeji: Wasiwe wengi, hata wakiwa watano tu makoo inatosha, ukipata mayai 20 kila mwezi ukayauza umepata sio mbaya.
8. Asali: Ukinunua dumu ukaja kufungasha unapeleka maduka tofauti tofauti hata sample 5 tu kila duka.
Kikubwa ndugu zangu maisha yanazidi kuwa magumu, tujifunze kupunguza matumizi. Vitu vingine tunajikuta tunanunua halafu hata hatuvitumii kivile mfano nguo, viatu n.k.
Tuongezee na idea nyingine wadau ambazo rahisi kuzitengeneza, yaani hazili muda sana lakini pia rahisi kuzifungasha, na pia haziharibiki hata zikikaa muda mrefu dukani.