Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

Hii biashara miyeyusho Sana , issue ni moja Tu worksmart earn more na hapa ndo akli inatakiwa ufanye kaz ..biashara gani kila sku unakuwa na shati moja limejaa unga ..Mimi hamna wakuu, hii biashara inafaa wazee waliofikia umri wa kufunga mahesabu just wanatafuta hela ya Kula mana washajenga washasomesha na mambo mengi ya msingi wamefanya .... Kijana unatakiwa upige show za kibabe unakunja hata 500000 Kwa wiki siyo mbaya....
Ifikie hatua mazingira yasituendeshe Sana Bali Sisi ndo tuyabadili mazingira yaendane na tunachokitaka ...
Mimi masuala ya kuuza mafuta kupikia kwa wiki 2 sijui sukari 3wks nije nipate kifaida cha 7500 yalinishinda...yaan hata iweje siwez rudi huko...si bora nikakusanye mikaranga tabora huko!
 
Mimi masuala ya kuuza mafuta kupikia kwa wiki 2 sijui sukari 3wks nije nipate kifaida cha 7500 yalinishinda...yaan hata iweje siwez rudi huko...si bora nikakusanye mikaranga tabora huko!
Hii biashara itategemea wapi umefungua na uwingi wa wateja. Kuna watu wanafanya na inawalipa sana na pia inategemea umeweka shilingi ngapi? Kuna watu wana mauzo ya siku mpaka milioni 2 hakosi laki faida

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kununua kwa carton kunakupa wewe faida kubwa zaidi ila bidhaa nyingine kama hazitoki sana ukinunua carton utaishia kupata hasara maana zitaexpire.
kabisa bora hizo ufanye hasa kwa vinywaji na sabuni sabuni ila mfano mambo kama blue bands maziwa ni shidaa
 
Wadau ili kupata mrejesho mzuri ni bora kununua vitu kwa wingi mfano katoni au kidogo kidogo?
Hiyo inaenda kulingana na mtaji na mzunguko wako...!!kama mtaji wako na mzunguko ni mdogo...nunua nusu nusu...angalau ujaze duka...mahitaji yakiongezeka utapanda kidg kdg
 
Biashara naona inafaida ikiwa eneo ni lako na umekaa mwenyewe..lakin kama umepanga na kumueka mtu cost ni nyingi ...
Kodi ya pango
Ela ya taka 10000 town
Umeme hapa kuna fridge zingine noma
Ela ya kula
Afu pia kuna hasara kama
Panya kula bizaa.
Bizaa kuaribika
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi, kreti la coca, paketi za sigara, pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama.

Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Shirima 😂😂😂
 
Kumekuwa na malumbano kuwa biashara ya duka hasa rejareja haina faida. Leo nitaleta baadhi ya bidhaa tu kupinga malumbano hayo (maana ndo ishu nnayoifanya)

Just kabla sijaanza, ukitaka kuona mafanikio ya hii biashara wewe muuzaji uwe mtaji wa kwanza. Kichwa chako kiwe mtaji dukani pia mazoea kwenye duka pamoja na mahusiano ya kimapenzi weka pembeni kabisa

1. Soda
Pepsi huuza kreti kwa sasa 9500(soda jumla hua 24 kwenye kreti). Ukiuza jumla utapata 12,000 (faida hua ni 2500)
Coca wanauza 10,000(hapa faida 2000). Take away zinauzwa katon 9,000 na znakuwa 12 (faida 3,000)

2. Vocha
Hapa nazungumzia za kurusha, za kukwangua sincerely speaking sijawahi kuuza na sitarajii.

- Tigo hutoa 6% kama faida kwa kila float utakayonunua (ukinunua float 10,000 unapata 600 (hapa bado faida za kwenye vifurushi). Ukiunganisha internet ya buku kwenye float wanakata 900 mteja atakupa 1,000..100 ya kwako

Voda hutoa 8% kila unaponunua float (ukinunua float 10,000 unapewa 800 (hapo pia kuna faida ukiunganisha vifurushi)

3. Maji makubwa Uhai
Lita 6 unanunua yakiwa matano kwa 8500 utauza kwa elfu 2 jumla unapata 10,000 (1,500 ya kwako)

Lita 12 unanunua kila moja 2500 utauza kwa 3,500 (1,000 kila dumu moja ni ya kwako)

4. Viberiti unanunua dazeni 4,500 unapata 9,000 (4,500 ya kwako)

5. Pampers unanunua 14,000, zinakuwa 40(kila moja utauza 500. Unapata 20,000 (elfu 6,000 ya kwako)

6. Sabuni ya unga ya kufunga
Utanunua kiroba elfu 31,000. Ukifunga vizuri na kwa kipimo cha 500 (faida mpaka 10,000 unapata)

Kuna vingi vya kuweka ila sitamaliza leo. Hapo bado sijataja unga, mchele, sukari, ngano, maharage, omato na vingne kibaaao

Hakuna biashara mbaya, ni wewe mfanyabiashara. Msimamo wako na unavyoichukulia biashara yako

great stuff

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom