Kwa waliozaa kabla ya ndoa

Kwa waliozaa kabla ya ndoa

Mimi ni mwanaume nilibahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa.
Sasa miaka 10 baadae nimeoa na nimemchukua huyu mtoto wangu naishi naye.

Sasa mke wangu ameniwekea masharti ambayo nafikiri ni magumu kutekelezeka. Naamini kuwa mwanamke niliye zaa naye ana haki ya kumuoma mtoto wake kila anapohitaji kufanya hivyo.

Sasa mke wangu hataki huyu mama mtoto afike nyumbani kumuona. Hataki mtoto aende kwa mama yake. Anataka mama mtoto akitaka mtoto tumtume housegirl ampeleke mtoto hoteli foleni halafu wakimaliza kuongea arudi naye.

Hali hii imeniingiza kwenye migogoro maana mama mtoto anaona namnyanyasa na upande mwingine mke wangu anaona pia namnyanyasa.

Hebu niambieni what is the beat way ku deal na hii situation?

Inaonekana huyo mkeo anahela kukuzidi.
 
Daaah aisee umenihuzunisha sana. Umebeba mimba miezi tisa....umeenda leba umenyonyesha af mtu anakunyang'anya mtoto hivihivi.....ningekuwa mimi ningemuiba nitokomee nae huko

Umethibitisha ukweli wa maelezo yake? Nimeona mengi sana hapa duniani watu si wakweli hawasemi kwa usahihi ukweli wa mambo.
 
Umethibitisha ukweli wa maelezo yake? Nimeona mengi sana hapa duniani watu si wakweli hawasemi kwa usahihi ukweli wa mambo.

Kwani mangapi yanatusikitisha na kutufurahisha hapa jukwaani ilhali hatujui undani wake? Mimi nimesikitika kwa ku-assume hii ni ya kweli
 
Huyo mke wako ana visa kupitiliza.

Kwanini usimrudishe huyo mtoto kwa mama yake ukatoa hela ya matumizi huko?!Kuna sababu yoyote ya msingi inayozuia mtoto kuishi na mama yake?! Mwanzo kabla hujaoa kulikuwa na utaratibu gani kuhusiana na malezi ya mtoto?! Ni sababu zipi zilipelekea umchukue mtoto baada ya kuoa na sio kabla?! Mke wako anam-treat vipi huyo mtoto?!

Anaenyanyaswa KWELI hapo ni mama mtoto na mtoto wala sio huyo mkeo. Fanya umtendee haki mtoto na mama yake pia. Usisombwe na ubinafsi + visa vya mkeo ambavyo vinaonekana havina logic.

wewe inaelekea hujaolewa jinsi unavyoreason. unadhani wewe ungekuwa na mtoto wa nje mmeo angeruhusu uliezaa nae aje aje kwako eti kumuona mtoto? na angekataa ungemlaumu kama unavyomsema mwanamke mwenzio eti ana visa visivyo na logic?!

nahisi uko kwenye nafasi kama ya huyo dada mwenye mtoto ndo maana unaongea kwa kuwa upande wake. khaaa!
 
Mimi ni mwanaume nilibahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa.
Sasa miaka 10 baadae nimeoa na nimemchukua huyu mtoto wangu naishi naye.
Kuna nini kimebadilika mpaka ukaamua kumchukua? Shule? Mama yake hawezi kuendelea kumtunza/kukaa naye? Mama yake ameolewa na mwanaume mwingine?

Sasa mke wangu ameniwekea masharti ambayo nafikiri ni magumu kutekelezeka.
Ni lazima kuwepo na masharti. Suala hili haliwezi kubakia holela na ndoa yenu ikabaki salama.

Naamini kuwa mwanamke niliye zaa naye ana haki ya kumuoma mtoto wake kila anapohitaji kufanya hivyo.
Hakuna haki isiyo na mipaka. Ndio anayo haki ya kumuona mwanaye lakini haki hiyo inaishia pale ambapo haki za wengine (mke wako kwa mfano) zinaanzia. Haki ni lazima iendane na wajibu na pia kuheshimu haki za wengine. Kwa mfano, hana haki ya kuja nyumbani kwako achilia mbali kwa muda anaotaka yeye isipokuwa kama wewe na mkeo (wenye nyumba) mmeridhia.

Sasa mke wangu hataki huyu mama mtoto afike nyumbani kumuona.
Yupo sawa. Mkeo anayo haki ya kuamua ni nani aingie nyumbani kwenu.

Hataki mtoto aende kwa mama yake.
Hapa mkeo anavuka mipaka. Hana haki ya kumzuia mtoto kwenda nyumbani kwa mama yake.

Anataka mama mtoto akitaka mtoto tumtume housegirl ampeleke mtoto hoteli foleni halafu wakimaliza kuongea arudi naye.
Nyie wanne (mume, mke, mama mtoto, na mtoto (miaka kumi tayari anajitambua, ni lazima kupata maoni yake)) muweke utaratibu ambao utazingatia haki na wajibu wa kila mmoja. Bila ya shaka kila upande utalazimika ku compromise ili kulinda haki za wengine kwa kiasi kinachokubalika. Hiyo proposal ya mke ni mmojawapo ya options tu, lakini ningeshauri kuwepo pia na frequency inayoeleweka na isiyoweza kuleta usumbufu usio wa lazima (sio kila akitaka, analetewa!, anaweza kutaka kila siku, mtaweza?) - kwa mfano inaweza kuwa fortnightly au monthly etc. Njia nyingine, badala ya house girl wenu kumpeleka, mama mtoto yeye atume mtu wa kuja kumchukua mtoto. Hata hivyo hili ni suala la muda mfupi tu, akifikisha miaka 12 (anaweza kuwa form one hivi) naamini huyo mtoto ataweza kwenda mwenyewe tu. Wengine huamua kuwapeleka kwa ndugu (mjomba, babu, bibi, shangazi etc) watoto wa namna hiyo. Lakini kubwa katika utaratibu wowote mtakaokubaliana ni wewe kutofanya vitendo vitakavyoweza kuashiria kuwa bado una mahaba na mama mtoto. Hii itampa hofu mamsap wako na hivyo kutokukuamini.

...Hali hii imeniingiza kwenye migogoro maana mama mtoto anaona namnyanyasa na upande mwingine mke wangu anaona pia namnyanyasa.
Kama nilivyosema hapo juu, katika suala hili ni lazima kila upande uta compromise maana ni lazima kuzingatia haki za wote. Bila ya shaka mkeo alijua kuwa una mtoto kabla hajaamua kuolewa na wewe. Suala hili la mtoto wako linaelekea halikuzungumzwa vizuri kipindi hicho. Haya mabadiliko kwa namna moja ama nyngine ni lazima yatamsumbua mkeo hasa kama unakwenda kinyume na matarajio yake. Lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ameolewa na mwanaume ambaye tayari alizaa na mwanamke mwingine na hivyo haki zake katika ndoa hiyo kwa vyovyote vile zitazingatia haki za baba wa mtoto, mtoto na mama wa mtoto.
 
Huyo mkeo ana common sense kweli?

wewe ndio huna common sense. wewe ungeoa mwanamke mwenye mtoto ungeruhusu mwanaume alezaa nae aje aje kumuona? hebu jiweke kwenye viati vya huyo mama kabla hujauliza mambo ya common sense bwana.
 
sijui nisemeje, lakini ukweli haiwezekani huyo mama wa mtoto aje hapo kuona mtoto, tena haikubaliki, moyo wa mwanamke umebeba mengi, yaani sijui ni semeje ili unielewe, tafuta namna ambayo mama wa mtoto atamuona mwanae lakini sio nyumbani ukoishi na mkeo, kama inawezekana huyo bidada anakaa karibu basi awe anapelekewa mtoto anashinda nae au kukaa nae then anamtuma mtu anamrudisha, sio habari ya yeye kukanyaga hapo nyumbani, kwanza unaweza kusabisha matitizo ambayo hukutarajia, unajua akili za wanawake wewe? kwanza hata wewe acha kucheka cheka na huyo mwanake, mlizaa yakaisha, hapo ni suala la mtoto tu, habari ya mazoea ya kufuatana nyumbani mmhm!, awe anapelekewa mtoto kwishaaaaaa.


Mungu weeeee! ningekuwa mimi hata muda wa kuja jf kuuliza usingepata, siku nyingi ningekuwa nimefanya maamuzi magumu, mwanamke aliezaa na mme wangu aje nyumbani kwangu. kiruuuu

teh!teh! teh! kwani akili za wanawake zikoje!?
 
wewe ndio huna common sense. wewe ungeoa mwanamke mwenye mtoto ungeruhusu mwanaume alezaa nae aje aje kumuona? hebu jiweke kwenye viati vya huyo mama kabla hujauliza mambo ya common sense bwana.

Kuja nyumbani kwangu hapana, lakini siwezi kukataza huyo mtoto asiende kwa baba yake.
 
Chunguza kwa umakini mkubwa juu ya upendo wa mkeo kwa mwanao. Ukiwa na uhakika kuwa mwanao anapata upendo unaotegemewa kutoka kwa mkeo, tafakari juu ya nafasi ya mama mzazi mwenzako kwa mwanao.

Kujua kama mkeo ana upendo thabiti kwa mwanao itakupa nafasi nzuri zaidi ya kujua mtoto huyo aishi kwako kwa wakati fulani au wakati wote ni aheri aishi kwa mama yake.

Wewe kwenda kumtazama mtoto kila mara kwa mama yake au mzazi mwenzio kuja kumtazama mwanae kwako kila mara, vyote vina madhara kwa mwanao kisaikolojia. Mtoto atajiona kuwa ni tofauti na watoto wako wengine au watoto wengine wa mzazi mwenzako, kama anao.

Ushauri wangu ni kwamba kama una uhakika na upendo wa mkeo kwa mtoto wako, zungumza na Mama wa mtoto ili muweke utaratibu unaoeleweka. Mtoto anaweza kuishi kwako au kwa Mama yake, wakati wa likizo atapumzika kwako au kwa Mama yake. Kama ataishi kwako, likizo aende kwa Mama yake. Kama ataishi kwa Mama yake, likizo ataishi kwako. Kama anaumwa, yeyote atakuwa na uhuru wa kwenda kumwona mwanaye aliko bila masharti yoyote.

Kama mkeo atagomea hata proposal hii, ujue ana matatizo, na mwanao yupo hatarini. Ni aheri kumnyanyasa mtu mzima mwenye uwezo wa kujitetea kuliko kuruhusu mtoto kunyanyasika. Ni aheri uonekane humfurahishi mkeo ambaye ana uwezo wa kujitetea kuliko kuruhusu mtoto anyanyasike kwaajili ya kumfurahisha mkeo.

Aisee umeporomoka utamu sana. Ushauri mzuri sana.
 
Ah mambo mengine kupunguziana siku za kuishi Tu!
 
Hapo hofu ya mkeo ni ww na mama mtoto kupasha kiporo.. cha muhimu wekeni utaratibu wa nyinyi kumuona mtoto bila kuonana... amfuate hapo hotelin amchukue akakae nae muda ukifika amrudishe hapo hotelin simple... nahisi ww ndo umesababisha hayo maana unaeza kuta unaviashiria vya kuendelea kumkubali mzazi mwenzio... ila mkeo mkabaji mzuri, tatizo anasahau haki za mama na mtoto
 
Kwakweli hili suala limenigusa sana. Nilizaa na mwanamume aliekuwa mpenzi wangu hatukuweza ishi pamoja nikaondoka na mtoto kwetu hawakupendezwa na mimi kuzaa bila kuolewa walikuwa sahihi, niliendeleza maisha na mtoto wangu kwa muda wa mwaka mmoja ndipo niliezaa nae akaniomba nimpeleke mtoto kwa mama yake nikampeleka baadae ikatolewa sugestion niwakabidhi mtoto akiacha kunyonya,nikaona si busara ndipo walipomuiba akiwa na miaka mitatu nikafuatilia mahakamani na Kivulini pia lkn kote sikupata msaada,nikaishia kusikia mtoto yupo huku mara kule, nikaenda nikamchukua, nikashtakiwa kwa wizi wa mtoto, nikanyanganywa mtoto niliezaa mwenyewe akiwa na miaka mitatu baba yake akakabidhiwa kwa amri ya mahakama ya mwanzo. NIKAWEKEWA wanted nisionekane maeneo yakwao. Baadae sikujua mtoto alipo tena hadi mwaka juzi akiwa darasa la pili ndipo nilipotafutwa na baba wa mtoto akidai mwanao ananisumbua njoo umsalimie, nikaenda baadae mtoto akalilia kwenda na mimi nikapewa wiki moja niende nae nitamrudisha, nikakaa nae nikamrudisha. Nikapewa masharti kuwa nikitaka tena kumuona mtoto sharti nipige simu kwa mkewe na approve ndipo nitamuona,anyway nilimuomba Mungu azidi kunipa ujasiri. Siku moja ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake mtoto nikawapigia simu nilete zawadi lol nilijibiwa kuwa sijawahi zaa hivyo sina mtoto km huyo. Nilipiga moyo konde nikaenda hadi hapo kwao nikampa mtoto zawadi nikaondoka wakiniangalia. From that wamehama na sasa ni mwaka wa pili sijamuona tena mtoto wangu na anatimiza miaka kumi.

Reason kubwa ya kutokuwa na access na mtoto kwa mujibu wa baba yake ni kwamba anampenda sana amefanana nae.

Nimesikitika sana.
 
Sometimes inabidi wachangiaji tuwe extrimist tuu no way out!

Baba ndio kichwa cha nyumba hakuna mwingine wa kumpangia ratiba wala cha kufanya

Ukiwa umezaa kabla ya ndoa iwe bahati mbaya au makusudi kaa tayari kwa mitatizo kama hii

Huwezi kupanda mchongoma ukavuna bolibo

Am out!

Wewe kweli extremist. Nimecheka sana.
 
@MBEBA MAONO KAJA kwa nini wanakutendea yote hayo

Pole sana

Mungu wa Mbinguni atakufariji

Damu haipotei

Kila jambo linalotokea ni mpango wa Mungu

Huyo ni mwanao aliyekaa tumboni mwako 9 months.....ni wa kwako

Jipe moyo

There is one day utakuwa pamoja na mwanao

Story yako imenigusa sana

Pole
 
Mi nafikiria tu akili ya mtoto sasa hivi inafikiria nini, i cnt imagine ningekua vipi kama dad kaoa mwingine afu nimekua na mom then niende kuishi kwa dad mom niwe namuona kwa kubahatisha ati hotelini, duh! mkuu kama head inabidi ukae ujifikirie mara mbilimbili maana ushuri wangu kwa sasa ni useless.. Mimi kama nimempa binti mimba hata by mistake huyo ndo angekua mke wangu, ingebidi nijifunze kumpenda tu jinsi alivyo.. Ila hiyo option haitokusaidia maana its too late for u..
 
Back
Top Bottom