Kwa waliozaa kabla ya ndoa

Kwa waliozaa kabla ya ndoa

Well ukisema hivyo napata point yako na taratibu naanza kukuelewa.

Kama kalazimisha mwenyewe tena kwa nia mbaya then nakosa jinsi ya kumtetea. Good luck xfactor ila hakikisha kwamba hulindi ndoa yako ukasahau kumlinda mtoto.

Mtoto ni baraka aisee,na ndoa ambayo haimtambui mtoto Hata kama ni wa nje hiyo sio ndoa. Tatizo ni hawa wazazi wenzetu wa kike,wachache sana ambao ni waelewa. Hawajui tu kuwa mwisho wa siku mtoto ndio anakuwa victim
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini unapendelea hivyo?

Kwasababu mama ana uchungu sana na mtoto kuliko mama wa kambo. Wapo mama wa kambo ambao wana roho nzuri lkn hawezi kuwa na uchungu sawa na mama mtoto.Pia Mara nyingi ni ngumu kwa baba wa kambo kunyanyasa mtoto kuliko mama wa kambo.

Lingine ni kwamba akiishi na mama yake hizi complication ambazo mleta mada kazipata zinakuwa zimepungua kwa kiasi kikubwa
 
Aisee!

Wengine tunapenda kuwa na watoto wetu 24/7 365.

Na kuwa mtu ambaye hawatendei vizuri haiwezekani kabisa.
 
Sometimes inabidi wachangiaji tuwe extrimist tuu no way out!

Baba ndio kichwa cha nyumba hakuna mwingine wa kumpangia ratiba wala cha kufanya

Ukiwa umezaa kabla ya ndoa iwe bahati mbaya au makusudi kaa tayari kwa mitatizo kama hii

Huwezi kupanda mchongoma ukavuna bolibo

Am out!

Tofautisha uanaume na ubabe mkuu.Mke sio kimada bali ni ubavu wako wa kushoto na mtu ambaye ameshikilia dhamana ya maisha yako kwa maana ya kwamba ndio anasimamia nyumba yako.

Hivyo kutumia mabavu sio busara na hutojenga,sanasana utajenga uwasama mwingine wa pili ukiachilia uwasama uliopo na mama wa mtoto.

Kabla hujao hakikisha unampata mtu muelewa na mueleze ukweli kuhusu mtoto. Pili Kaa naye chini kiutu uzima uongee naye otherwise ikitumia mabavu ndio mtoto ataishia kunyanyasika ukiwa haupo. Haya mambo wala hayahitaji kuwa baunsa.
 
Hilo la kuhakikisha mtoto hanyanyaswi ni jema, ni vizuri una uhakikisha hilo. Lakini bado hutumii busara wala haki kusema mtoto asiende kwa mama yake kamwe. Kama ulijua ulozaa nae sio mwema kwanini ulizaa nae on the first place. Ungesubiri ukazaa na ambae ni mke wako ili kusiwe na mtafaruku wa aina yoyote ile.
kwa wanaume wetu hawa, mi nafikiri mwanamke ukishaamua kuzaa unatakiwa ujue majukumu ya mtoto ni yako kwa asilimia kubwa sana whether umeolewa or not. huyo mama mtoto alifanya kosa kumuacha mwanae akalelewe na mwanamke mwingine wakati yeye yupo. apart from kukataliwa kwenda kuona mwanao, huna hakika na malezi ya huyo mke mwenzio. Wanaume hawalei watoto,kina mama ndio tunalea. Mtoto anaweza kuwa anapitia magumu bila wewe kujua.

Upande mwingine, maisha ya bongo yanajulikana. kumuacha mzazi mwenza wa mmeo aje home kwako ni risk kubwa sana. Hujui kama atakuja kwa wema au kwa ubaya. it just makes sense mtoto awe anapelekwa kwa mama yake, lakini si mama mtu kwenda nyumbani kwa watu.

Kuondoa lawama, kila mwanamke na alee mwanae
 
Aisee!

Wengine tunapenda kuwa na watoto wetu 24/7 365.

Na kuwa mtu ambaye hawatendei vizuri haiwezekani kabisa.

Kila mtu yupo hivyo mkuu ila inategema na mama wa mtoto. Ukipata ambaye ni muelewa mbona maisha yanaenda vizuri na mtoto unakaa naye vizuri tu.
 
Dah Mwanademokrasia sana wewe.

Hapo ningekuwa mie, mjadala ungekuwa una uwanja mdogo sana, ningeilinda haki ya huyo Mama kuja kumwangalia mwanae hapo nyumbani.

Lakini ingekuwa ni sharti aje kwa heshima na ustaarabu na ingekuwa ni sharti aje kwa APPOINTMENT TU, lazima aongee na Mke kabla hajaja, sio kukurupuka tu bila appointment.

Na mke ndio atakubaliana nae aje lini na muda gani, na atapanga muda ambao mie sitakuwepo nyumbani.

So kama angekuwa ni mke wangu uchaguzi ungekuwa sio kuja au kutokuja bali ni jinsi ya kuja na muda wa kuja.

Kwa wanawake, unavyomfanyia mwingine ebu pia angalia kama ungelikuwa wewe ndio yeye au fikiria ungekuwa wewe ndio huyo mtoto ungejisikiaje?ni wajibu wa mke hasa kama ulijua kabla hajaolewa kuwa mme wake ana mtoto kabla kumfanya mtoto yule aishi maisha normal kadri awezavyo, hii ya mtoto kupelekwa kumsalimia Mama bar au kwenye kiosk utafikiri ni mzigo, hapana, kisaikolojia itamuathiri sana mtoto na hapo nyumbani atakuwa kama second class person, hawezi kujiona sawa.

Kama hilo limeshindikana basi mrudishe mtoto akakae na Mama yake mzazi, na wewe sasa ndio utakuwa unaenda kwa huyo Mama kumtembelea mtoto wako, sasa hapo huyo mke ataangalia ni ipi afadhari kati ya huyo kuja hapo au wewe kwenda kwa huyo mwanamke.
 
Huyo mke wako ana visa kupitiliza.

Kwanini usimrudishe huyo mtoto kwa mama yake ukatoa hela ya matumizi huko?!Kuna sababu yoyote ya msingi inayozuia mtoto kuishi na mama yake?! Mwanzo kabla hujaoa kulikuwa na utaratibu gani kuhusiana na malezi ya mtoto?! Ni sababu zipi zilipelekea umchukue mtoto baada ya kuoa na sio kabla?! Mke wako anam-treat vipi huyo mtoto?!

Anaenyanyaswa KWELI hapo ni mama mtoto na mtoto wala sio huyo mkeo. Fanya umtendee haki mtoto na mama yake pia. Usisombwe na ubinafsi + visa vya mkeo ambavyo vinaonekana havina logic.

Ni kweli kabisa.

Mwanamke kama huyu utamwamini vip kweli kukulelea huyo mtoto?

Huyo mtoto hapo yaelekea ni kama mzigo tu kwa mke wake, ni wajibu wa Baba kuchukua hatua maana mtoto hawezi kujilinda.

Solution ni mke aelewe ili kumfanya mtoto ajione sawa na watoto wengine au Baba akubali mtoto arudi kwa mama yake.
 
Dah hii ni hali ngumu sana, POLE ndugu!
Nimeupenda ushauri wa xfactor. "Boarding school" pia inategemea na jinsi unavyoyatazama malezi ya mtoto. Kwa hali ya sasa, mimi naamini sana katika kukaa na mtoto muda mrefu kuliko kumpeleka sehemu kama "boarding school". Kama una ndugu waweza watumia hao kama kiunganisho cha mtoto na mama yake kama alivyosema xfactor. Kumbuka muda wote kuwa pamoja na kuyafanya haya kwa kulinda "interest" ya mkeo, mtoto nae anatakiwa kukua salama kisaikolojia. Haijalishi mtoto analelewaje na mkeo, kumbukumbu na uhitaji wa mama haiwezi kuisha; na hata kama mama alifanya ujinga wa kiasi gani kumbukumbu ya mwanae haiwezi kumfutika.
Mwisho wa siku ni ujasiri wako wa kiume na busara ndivyo vitakufanya ulishinde hili
 
Mleta mada kuna jambo hujaclarify hivyo ushauri wa watu unashindwa kuwa focused. Kwa mfano, mama wa mtoto hana uwezo wa kumlea mwanaye? Kama alimlea kwa kipindi chote cha miaka 10 nyuma ni kitu gani kimesababisha uone sio busara yeye kuendelea kumlea? Je naye ameolewa au ana mahusiano na mwanaume mwingine?

HOFU YA MKEO
Hofu kubwa ya mkeo wa ndoa sio kufika kwa mzazi mwenzio kwako, hapana. Hofu yake ni uwezekano wa yeye kumharibia ndoa yake-anafahamu kiporo hakihitaji moto mkali. Hofu ya pili ni uwezekano wa kuleta visa na vurugu nyingine tu za kibinadamu kutokana na utofauti au kupishana kwa tabia.
Mwanamke yoyote mwenye akili lazima atatumia nguvu zake zote kuilinda ndoa yake isiharibike au kuvunjika. Anachokifanya mkeo ndio hichi.

NINI CHA KUFANYA
Njia bora ya kutatua hili jambo ni kuruhusu mama amlee mwanaye, nawe uwe unagharamia matumizi ya mtoto akiwa kwa mama yake. Najua unaweza ukawa unamiss na kutamani uwe unamwona mwanao siku zote lakini kwa kawaida mwanaume sio mleaji hivyo (kati ya saa 12 za mwanga, utakuwa naye sio zaidi ya saa 3, mengine yote atalelewa na mkeo/housegirl/walimu n.k) hivyo kubali tu uwe unakaa naye wakati wa likizo za shule. Nyakati nyingine mwachie mama yake. Kama unaona hili haliwezekani na ni lazima mtoto akae kwako, jaribu kwa kiasi kikubwa kuheshimu hisia za mkeo kwani anachokilinda pia ni kwa faida yenu wote (ukitaka kujua hili, ngoja ndoa ivunjike halafu utaona reaction ya mzazi mwenzio baada ya kurudiana na kufurahiana kwa mda mfupi). Kwa vyovyote vile, hatua ya mzazi mwenzio kufanya safari zisizokauka kwako kwa dhumuni la kumfata/kumsalimu mtoto inapaswa kuwa jambo la mwisho kabisa kufikiriwa. Na hata ikibidi iwe hivyo, lazima ifanyike katika makubaliano yenye masharti maalum na yaliyoridhiwa na nyinyi nyote kwa pamoja.

HAKI YA MTOTO
Mtoto ana haki ya kulelewa katika saikolojia itayompa afya kimtazamo, hisia, ukuaji na maadili. Mama wa mtoto ana nafasi kubwa sana ya kumjenga mtoto kisaikolojia akaelewa mathalani, ni kwanini hamuishi pamoja au ni kwanini anakuona mara chache. Kwa uzoefu, wanaume huwa hatulipi uzito na huwa hatuliwezi vema hili swala la kujenga saikolojia bora ya mtoto katika kumtengeneza awe mtu wa namna gani baadae. Wanawake wanaiweza kazi hii vizuri kutokana na ukaribu wao kwa watoto hasa wakiwa kwenye umri mdogo (kama huo wa mwanao). Saikolojia hii itasaidia pia kutunza upendo na imani ya mtoto kwako wewe kama baba.
 
Mada kama hizi huwezi kumkosa Matola bin tutusa... anjikumbusha alivopigwa kibuti na mke wake
 
Last edited by a moderator:
........Mtu kama umezaa nje ya ndoa au ulikuwa na ndoa mkaachana ni vizuri mtoto akae na mama yake.
Kama wewe baba una uchungu na mtoto wako....hakika endelea kulea mtoto akiwa kwa mama yake.

Sasa wewe mtoa mada hii, nini kimesababisha umchukue mtoto kutoka kwa mama yake mzazi?

Je huwezi lea mtoto akiwa kwa mama yake?

Mimi huwa siwaelewi wanawake wanaoacha mtoto alelewe na mwanamke mwingine na wakati mama mzazi upo.

..........Mimi hata itokee bahati mbaya tumeachana na my hubby, God forbid! Simuachii mwanangu mwanaume. Sitaki mwanangu alelewe na mama wa kambo.
Na hata akigoma kulea poa tu, nitalea mwenyewe!!!
 
Simuachii mwanangu mwanaume. Sitaki mwanangu alelewe na mama wa kambo.
Na hata akigoma kulea poa tu, nitalea mwenyewe!!!

Hutaki mwanao alelewe na mama wa kambo, sawa.

Je, huna tatizo akilelewa na baba wa kambo?
 
Niliwahi kuishi na bro wangu pale Arusha miaka ya 2006, yeye kabla ya kufunga ndoa na mkewe tayari alikwishazaa nje watoto wa3, wakike yupo kateshi, wakike yupo mbulu na wakiume yupo kisongo ila hakuwa amemwambia mkewe.
Alipoamua kufunga ndoa mke wake wa sasa aliyezaa naye watoto wawili aliamua kutest zali la kumweleza mkewe na kwenda kumchukua yule mtoto wa kiume pale kisongo akiwa darasa la nne na kuja kuishi naye ngusero akisoma s/m sokoni one.
Maskini mtoto alinyanyaswa na kuteswa na yule shemeji mpaka huruma, akampa marufuku mama yake kuja kumwona pale nyumbani, shuleni wala kanisani au hata kuongea kwa simu.
Mtoto akawa anajaribu kutoroka kwenda kwa mama yake anakaa huko wk 2 basi akirudi pale home atasemwa na kusingiziwa kuwa katoka kuchukua madawa ya uchawi ya kumuua yule shemeji ili mama yake arudie ndoa na yule mtoto atanyolewa nywele zote za kichwani, kwapani mpaka matako.ni ili atolewe huo uchawi.
Hayo yalikuwa yanafanywa na shem bila bro kujua na kale katoto kalikuwa hakasemi ila alipokuja kugundua akaamua kumhamisha shule na kumpeleka kwa bibi yake huko songea ndo ikawa pona ya yule mtoto.
Baadhi ya wanawake ni makatili sana kwa watoto ambao sio wao na akipata mwanya wa kumfanya atakacho anamfanya kweli huyo mtoto.

baba alichangia huyo mama kuwa na hasira hamna kitu kibaya kama mwanaume au mwanamke kumficha mwenzie kuwa ana mtoto isikie tu kwa mwenzio
 
Hutaki mwanao alelewe na mama wa kambo, sawa.

Je, huna tatizo akilelewa na baba wa kambo?

........Akilelewa na baba wa kambo is okay, sababu mimi nitakuwa naye mwanangu muda wote.

Na baba wa kambo akishanipenda mimi, basi atampenda na mwanangu. Wanaume wengi hawanaga tatizo na watoto wa kambo kama wanawake.
 
Aisee! Mi nilidhani kiasili wanawake ni watu wenye upendo sana.

Sasa kama hivyo ni kweli, iweje wawe na tatizo na watoto wao wa kufikia?

Na je, wewe unaweza ukalea mtoto wa kambo?

Au katika kusema kwako kwamba huwezi kumwacha mwanao alelewe na mama wa kambo umejitumia mwenyewe kama kipimo cha jinsi mwanao atakavyolelewa kwa kujiangalia na kuona kama na wewe unaweza kulea mtoto wa kambo au la?
 
..........mimi sina tatizo na kulea mtoto wa kambo, mtoto wa kambo ni kama mtoto wangu.
Naye anastahili upendo, sijui kwa nini baadhi ya wanawake ni wakatili sana kwa watoto wa kambo!

Hawajui jinsi ulivyompata mtoto wako kwa uchungu, na hivyo hivyo hata huyo wa kambo alikuja kwa uchungu.

Napenda sana watoto!! Mimi binafsi kama bado nipo hai sipendi mwanangu alelewe na mtu mwingine, hiyo ni mimi.
 
Aisee! Mi nilidhani kiasili wanawake ni watu wenye upendo sana.

Sasa kama hivyo ni kweli, iweje wawe na tatizo na watoto wao wa kufikia?

Na je, wewe unaweza ukalea mtoto wa kambo?

Au katika kusema kwako kwamba huwezi kumwacha mwanao alelewe na mama wa kambo umejitumia mwenyewe kama kipimo cha jinsi mwanao atakavyolelewa kwa kujiangalia na kuona kama na wewe unaweza kulea mtoto wa kambo au la?

Ishu ni mbili hapo mkuu,Hata kama yeye hana tatizo kulea mtoto wa mwanamke mwenzie

1. Mama wa kambo Hata kama atakuwa ni mzuri na muelewa lakni hawezi kuwa zaidi ya mama wa mtoto

2. Sisi wanaume hatuna hizi habari za kunyanyasa watoto wa kambo. Tuna mambo mengi hivyo hatuna michongo ya kuanza kummind mtoto. Ndio maana bora mtoto alelewe na baba wa kambo(alelewe na mama yake) kuliko na mama wa kambo
 
.............Halafu ujue tatizo muda mwingine lipo kwa mtoto, ujue mimi naweza kumuadhibu mtoto wangu wa kumzaa ikawa poa tu........lakini mtoto wa kambo umuadhibu basi utaonekana mbaya.

Na watoto wa kambo wengi wakishaona anaishi na mama wa kambo, basi hata ukimpa adhabu ataona umemuonea.

Kulea mtoto wa kambo mama wa kambo ni mtihani!! Inabidi umlee kama yai, maana ukimrudi tu ni kosa kaonewa.
 
Ishu ni mbili hapo mkuu,Hata kama yeye hana tatizo kulea mtoto wa mwanamke mwenzie

1. Mama wa kambo Hata kama atakuwa ni mzuri na muelewa lakni hawezi kuwa zaidi ya mama wa mtoto

2. Sisi wanaume hatuna hizi habari za kunyanyasa watoto wa kambo. Tuna mambo mengi hivyo hatuna michongo ya kuanza kummind mtoto. Ndio maana bora mtoto alelewe na baba wa kambo(alelewe na mama yake) kuliko na mama wa kambo

In all fairness, wapo wa mama wa kambo ambao ni wema sana na wenye upendo mwingi tu kwa watoto wao wa kufikia.

Lakini nakiri kuwa wa hivyo huwa ni tunu.
 
Back
Top Bottom