xfactor pamoja na yote hayo bado humtendei haki mzazi mwenzio. Besides, unadhani kwa kumkataza mtoto kwenda kwake ndo hatajaribu kukuharibia ndoa yako kama lengo lake ni hilo?! Be fair, kama unavyopenda wewe kukaa na mwanao ndo na yeye anapenda vile vile, mpe uhuru nae. Pia usidhani mtoto atakuja kukushukuru kwa hilo. Maana hapo ulipo unafikiria "ndoa yangu, ndoa yangu" na wala sio mtoto. Don't be like that aisee. Binafsi nisingefurahia kama mtu nlonae angekuwa kama wewe iwapo angekuwa amezaa kabla ya kukutana na mimi. Besides, Sio kila ubaya unaokusudiwa humfika mtu, mengine hupita tu kwahiyo usiishi kwa hofu ya kufanyiwa ubaya kupitia mtoto. Pia kumbuka kwamba huyo mtoto anakua na atakuja kufanya maamuzi yake mwenyewe linapokuja swala la kuonana/kuwa na mama yake mzazi. How will you control him/her then?! Kama ujinga si atajazwa tu?!
Muhimu ni wewe kutumia nafasi yako kama baba,mume na mzazi mwenza vizuri. Usikandamize sana upande mmoja ukapendelea kwingine na mwisho ukaishia kuharibu badala ya kujenga kama ulivyokusudia.