Kwakweli hili suala limenigusa sana. Nilizaa na mwanamume aliekuwa mpenzi wangu hatukuweza ishi pamoja nikaondoka na mtoto kwetu hawakupendezwa na mimi kuzaa bila kuolewa walikuwa sahihi, niliendeleza maisha na mtoto wangu kwa muda wa mwaka mmoja ndipo niliezaa nae akaniomba nimpeleke mtoto kwa mama yake nikampeleka baadae ikatolewa sugestion niwakabidhi mtoto akiacha kunyonya,nikaona si busara ndipo walipomuiba akiwa na miaka mitatu nikafuatilia mahakamani na Kivulini pia lkn kote sikupata msaada,nikaishia kusikia mtoto yupo huku mara kule, nikaenda nikamchukua, nikashtakiwa kwa wizi wa mtoto, nikanyanganywa mtoto niliezaa mwenyewe akiwa na miaka mitatu baba yake akakabidhiwa kwa amri ya mahakama ya mwanzo. NIKAWEKEWA wanted nisionekane maeneo yakwao. Baadae sikujua mtoto alipo tena hadi mwaka juzi akiwa darasa la pili ndipo nilipotafutwa na baba wa mtoto akidai mwanao ananisumbua njoo umsalimie, nikaenda baadae mtoto akalilia kwenda na mimi nikapewa wiki moja niende nae nitamrudisha, nikakaa nae nikamrudisha. Nikapewa masharti kuwa nikitaka tena kumuona mtoto sharti nipige simu kwa mkewe na approve ndipo nitamuona,anyway nilimuomba Mungu azidi kunipa ujasiri. Siku moja ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake mtoto nikawapigia simu nilete zawadi lol nilijibiwa kuwa sijawahi zaa hivyo sina mtoto km huyo. Nilipiga moyo konde nikaenda hadi hapo kwao nikampa mtoto zawadi nikaondoka wakiniangalia. From that wamehama na sasa ni mwaka wa pili sijamuona tena mtoto wangu na anatimiza miaka kumi.
Reason kubwa ya kutokuwa na access na mtoto kwa mujibu wa baba yake ni kwamba anampenda sana amefanana nae.