Aisee una kumbukumbu nzuri! Nilishamsahau mwl. Mchala. Mapera maziwa, hivi kwa kiingereza yanaitwaje? sijawahi kuyala tena toka nimalize Forodhani late 80's.
Sr. Edgara jamani, akikasirika alikuwa anaongea kikwao....nilikuwa nafurahia sana kwenda kule juu kushona.
Mwl. Tarimo nae alikuwa anafundisha Sayansi Kimu, tunaenda jikoni kujifunza kupika. Nakumbuka siku tulipika Sambusa....
Mw.Mohamed, she was my favorite teacher. Mwl wangu wa darasa nikiwa la nne, alikuwa anafundisha hesabu.
Mwl. Matata, ushepu balaa. Akigeuka kuandika ubaoni ni shidaaaa....alifundisha Kiswahili
Mwl. Bange, heasbu zimetulia pale.
Mwl. Nyalika, mwl wa English. Kuna siku nilikutana naye hazeeki......
Mwl. Nzige, Manyama, Shirima, Mbuya(RIP), Kauta, JJ, Msaki(mwl wangu darasa la kwanza), Sr. Kimathi, Mwalubandu, Barongo. dah, sitaisahau ile shule. Good memories kwa kweli....