Namkumbuka H/Master Andrew Kwayu, Mama Temba akitufundisha 'Namba ', 'Kicheche' akitufundisha siasa.
Bible Scripture aiidha pale Don Bosco au ktk jengo moja pale karibu na Muhimbili Hosp.
Ugomvi ktk soccer sie na Tambaza Boys miaka ya nyuma ilikuwa kitu cha kawaida. Siku moja ulitokea ugomvi mkubwa pale ktk uwanja wa shule Muhimbili P/School, tukavulumishiwa mawe na vijana wa O Level, refa alikuwa Padri mmoja wa Ki-Phillipino toka Bon Bosco, baada ya hali kuwa mbaya alichomoa bastora na kupiga risasi mbiili juu! Hiyo ikawa salama yetu.
Nakumbuka ilikuwa tukichoka ku-bukua, tulikuwa tukiingia Pale Paramedical Muhimbili kucheza disco.
Kipindi hicho tukiwa na akina Akilimali Kighoma Malima, Patrick Mkandya, Ismael Kulengwa(Mzee wa kambi), Asimwe Kabunga, Lusajo, Arnold Nzali; Tito William, Muhindi Musyangi, Nelson (Easy E), Rweyemamu (Mom), Adronicus Buberwa, Kantalamba, Abraham Chenelo na wengine wengi.