Kwa wale mlio kwenye mahusiano ya muda mrefu mnafanya nini kuhuisha penzi pale linapokuwa limepoa?

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,368
2,000
Habari za wakati huu wanajamvi pendwa la MMU.

Ni siku ya tarehe 05/05/2021 kwa wale ambao siku ya jana 04/05/2021 ilikuwa siku ndefu poleni na wale ilikuwa kinyume chake hongera kwenu. Acha niende kwenye hoja moja kwa moja.

Nimekuwa kwenye mahusiano na binti wa mtu kwa mwaka na kitu sasa almost mwaka mmoja na nusu hivi na nimeshaenda kwao na mahari nimetoa almost yote. Tokea mwezi huu umeanza nimekuwa napata changamoto ya upendo kupungua kwake, najitahidi sana ila najikuta nakosa hata hamu ya kuongea naye au wakati mwingine naanza kuhisi kumchoka.

Hii iliwahi nitokea kipindi fulani, nilimuumizaga binti wa watu na nilijitahidi sana kupambana na hii hali ila yeye akashindwa kuvumilia akaondoka. Na wakati huu tena binti wa watu anajitahidi kunijali na kunijulia hali mara kwa mara ila mimi daah hisia zimeanza kukata kabisa.

Sasa hii hali naiona kama itanisumbua sana, nahitaji msaada wa mawazo au mapendekezo ya namna ya kuhuisha hili penzi..! I don’t wanna hurt her.

HELP ME OUT WAKUU

1620206487322.png

 

Jerry Ekky

JF-Expert Member
May 6, 2018
1,133
2,000
Tatizo ulilo nalo ni kutompa nafasi katika maisha yako huyo binti, hivyo inabidi uanze kulifanyia kazi hilo.

Pia hakikisha mnapata wasaa wa kutumia muda kiasi (km siku za wikiend n.k kulingana na muda wenu) mkiwa pamoja katika mazingira tofauti na mliyo yazoea (mfano., mkaenda hata mbuga za wanyama au maeneo ya utalii au hata mkaenda beach n.k) na kutumia masaa kadhaa pamoja huku mkipiga story mbalimbali ambazo zitawafanya nyote muwe na furaha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom