willpower
JF-Expert Member
- Dec 3, 2019
- 408
- 2,291
Miaka kadhaa nyuma, asubuhi siku ya jumapili, niliamshwa kwa kelele zisizo za kawaida, watu kadhaa walikuwa wakigonga mlango, japo nilikuwa chumbani lakini ugongaji ule wa mlango haukuwa wa kawaida.
Nikaamka na kukutana na watu wanne, mzee mmoja, vijana wawili wakiwa na askari. Swali lilikuwa moja tu unamjua ‘’Sofia’’?(Sofia sio jina halisi). Nikiwa najiandaa kujibu, polisi akasema twende tukazungumzie kituo cha polisi. Sofia alikuwa nani? Kufahamiana kwangu na Sofia; ilikuwa hivi…….
Miaka hiyo nikiwa naishi kwenye nyumba ya mjomba wangu maeneo ya Kijitonyama huku ndio nikiwa nimeanza ajira tu katika ofisi moja katikati ya jiji Mtaa wa Azikiwe.
Asubuhi moja nikiwa kituoni hapo Sayansi, ikapita taxi, ikasimama na dereva tunaelekea Posta, twende kwa shilingi 1000. Nikaona badala ya kusubiri daladala ya Mwenge Posta acha nipande tax. Mbele alikuwa dereva na abiria wa kike, huku nyuma nilikuwa mimi na jamaa mwingine.
Tukafika Posta, jamaa wa taxi akasema atatushusha pale mbele ya Haidery Plaza - kuna kituo cha kuuzia mafuta pale; miaka ile ilikuwa Oryx na pia kulikuwa na mgahawa.
Kwa kuwa ilikuwa mapema sana nikaona niingie kupata chai, nikiwa nimeshaagiza chai, huyu dada naye akaingia na kwa bahati nzuri akaja akakaa meza moja na mimi.
Hapo sasa ndipo nilipomuona vizuri, binti mweupe mwenye asili ya Kiarabu, mzuri na kwa kweli alikuwa anavutia.
Mazungumzo ya mambo kadhaa, nikaona binti anatoa ushirikiano mzuri. Nikaona hawa ndio wale mabinti wazuri lakini huwa hawajisikii, kwa kweli kwa wakati huo sikuwa na jambo la kumvutia.
Asubuhi hiyo, nikapokea simu ya mkuu wa kitengo kuwa nimwambie secretary wa ofisi anunue vifaa vya ofisi (stationeries); dada akasikia mazungumzo na kusema kuwa yeye ofisi yake inauza hizo stationeries hivyo nimuungishe kwenye biashara.
Hapo nikapata namba yake na yeye akachukua namba yangu kwa urahisi tu.
Nilipofika ofisini, nikamwambia secretary kuwa hivyo vifaa akavinunue katika duka nililoelekezwa na Sofia (nikampatia namba ya yule dada, biashara ikafanyika). Majira ya mchana Sofia akapiga simu kunishukuru kwa kumuungisha kwenye biashara yake.
Kuanzia hapo ikawa kawaida kwetu kuchati na kuwasiliana mara kwa mara. Mpaka kufikia wakati huo nilijipima na kuona kabisa kuwa huyo binti japo ni umri wangu lakini ananizidi mambo mengi; hivyo hata wazo la kumtongoza sikuwa nalo.
Ikafika mpaka nikakaribishwa kwenye ofisi ya Sofia, ikawa ni kawaida kwetu kunywa chai pamoja pale mgahawani lakini pia mara kadhaa tulikuwa tunakula kwenye mgahawa uliokuwa maarufu miaka ile wa Food World mtaa wa Azikiwe.
Kwa mara ya kwanza Sofia akaniwezesha kula Pizza, miaka ile Steers ilikuwa mtaa wa Samora opposite na British Council (kwa sasa kuna Petrol station ya Lake Oil).
Uzuri wa Sofia, kama amekuita sehemu basi lazima atafanya malipo, kwahiyo kipato changu kidogo wakati ule kilikuwa salama kabisa. Mara chache nilikuwa nikitumia pesa ndogo kwenye breakfast.
Mawasiliano ya mara kwa mara yakapelekea kuanza kuchati usiku, na wakati mwingine mazungumzo ya usiku. Kulikuwa na offer fulani hivi ya kuzungumza usiku bure.
Hapo sasa ndipo stori za kazi na urafiki zikaingia kwenye mapenzi; katika kuhojiana dada akasema kuwa yeye ni single na mpaka wakati huo alikuwa bado anaishi kwao na hata hiyo ofisi ni ya baba yake; iliniwia vigumu kuamini lakini mfululizo wa simu za usiku na kukutana naye mara kwa mara ikanipa uhakika kwamba huyu ni single.
Licha ya kumkaribisha nilipokuwa ninaishi mara kadhaa lakini Sofia alikuwa anakataa, lengo la kumkaribisha gheto ilikuwa walau nione je nikiwa naye ndani kama anaweza kutoa penzi. Wanaume wengi tunaushahidi wa kutosha kuwa mwanamke anayekubali kuja kwako basi walau una asilimia 60 ya kumpata. Hii mbinu ikafeli lakini pia sikuwa na ujasiri wa kumtongoza moja kwa moja.
Kuingia kwenye Mahusiano ya kimapenzi
Kuna siku moja baada ya kama miezi miwili tangu nimfahamu Sofia, akaniambia anataka kwenda kutembea Bagamoyo weekend kama nina muda tunaweza kwenda wote . Nikampatia jibu kuwa nipo free, hivyo tutaenda bila shaka. Mpaka kufikia wakati huu mimi na Sofia tulikuwa na utani mwingi sana, mambo tuliyokuwa tunachati yalikuwa ni ya kimapenzi zaidi.
Safari ya Bagamoyo ikafika, tukiwa tunatembelea maeneo mbalimbali ya Bagamoyo, Sofia akapokea simu; katika mazungumzo mwisho akamaliza kuwa leo hatorudi nyumbani analala mtu fulani(alitaja jina la kike).
Majira ya saa kumi nikamuuliza; jioni hii tuanze safari, Sofia akasema tunarudi kesho, leo tunalala Bagamoyo huku akimalizia ‘’au hutaki kulala hotelini’’, kufikia hapo nikaona sasa zile chatting za masihara zinaenda kuwa kweli.
Jioni ile kweli tukalala katika hoteli moja, na kwa kweli usiku ule nikatunukiwa penzi tamu na Sofia. (Mpaka leo na huu utu uzima wangu; naomba nikiri kuwa Sofia ndio mwanamke mtamu zaidi kati ya wanawake wengi waliowahi kunitunuku).
Bagamoyo ikafungua ukurasa mpya wa penzi na Sofia. Kumbuka mpaka wakti huo Sofia alikuwa anajua ninapoishi lakini hakuwa anewahi kufika.
Tulipokuwa tunarudi kutoka Bagamoyo, ndipo akaniambia kuwa anataka kujua ninapoishi, baada ya kushuka mwenge tukaanza safari ya kwenda gheto.
Tulifika na Sofia kwa mara kwanza akafika ninapoishi; nikamfuatia kiepe kwa Kipanga (huyu alikuwa mkaanga chipsi maarufu sana mtaani kwetu pale Kijitonyama).
Sofia akapiga kiepe yai na kushushia na soda kutoka kwenye kifriji changu kidogo cha mtumba nilichonunua pale Magomeni. Baada ya kutazamana kwa muda ikapigwa mechi nyingine ila wakati huu ikawa kwenye uwanja wa nyumbani, yote kwa yote Sofia alikuwa fundi; ukizingatia ile rangi ya Arabuni, usafi wa mwili, ulaini na uteke wa maongo yake; kwa kweli nilijiona nipo juu ya huu ulimwengu.
Nikamsindikiza na akarudi kwao; jioni hiyo ilikuwa ni mwendo wa sms tu juu ya kilichotokea, nilihisi kama naota hivi lakini ilikuwa kweli; binti Sofia alikuwa ameshakuwa mpenzi wangu bila ya mimi kutongoza na kwa kweli kwa hadhi ya maisha yetu ni wazi kuwa alikuwa amenitunuku tu.
Maisha haya ya kimapenzi yaliendelea kwa muda mrefu, tofauti yetu ya kidini ilifanya kusiwe na wazo la ndoa; lakini pia bado umri ulikuwa unaruhusu kuendelea kula mema ya nchi.
Sofia alianza kufahamiana na rafiki zangu wachache na ndugu kadhaa; wote waliomuona walikuwa wakimsifia na kushangaa nimewezaje kuwa huyu binti.
Kwa upande wa pili, nilichoweza kujua kuhusu Sofia ni lile duka, mdogo wake wa kike ambaye alikuwa akisoma chuo fulani hapa mjini na kufika mpaka nje ya geti lao.
Sofia alidai kuwa hataki iwe wazi sana maana kwa taratibu za dini ikijulikana kuwa mimi ni wa dini nyingine basi italeta shida. Maelezo hayo yaliniridhisha kabisa; ili mradi napata mema ya nchi, tena kwa uhuru wote na mara chache naweza kwenda naye kwenye matukio ya kijaa (ndoa,sendoff n.k). Kwangu hizo siri hazkikuwa tatizo.
Tukiwa na miezi kumi ya mahusiano, ndipo siku moja Sofia akaniambia kuwa atasafiri na familia yao kwenda eneo fulani hapa Tanzania. Na kama ilivyo kawaida ya wapenzi wa Dar es Salaam, tukapata wasaa wa kuagana na kutakiana safari njema.
Baada ya hapo simu ya Sofia ikawa haipatikani kabisa, nilijitahidi kupiga na kutuma meseji lakini kwa siku mbili simu ikawa haipatikani. Safari ilikuwa Alhamisi jioni, akaanza kutopatikana ijumaa, na jumamosi.
Jumapili asubuhi ndio nikaja kugongewa na hao watu wanne akiwemo polisi mmoja.
Swali lilikuwa moja tu unamjua ‘’Sofia’’?(Sofia sio jina halisi). Nikiwa najiandaa kujibu, polisi akasema twende tukazungumzie kituo cha polisi.
Kilichokea ni kuwa; kumbe Sofia alikuwa mke wa mtu, jamaa alimuoa na kumuacha akiishi nyumbani kwao maana yeye alikuwa akifanya kazi nje ya nchi.
Na ile safari aliyoniaga kumbe jamaa yake alikuwa amerudi na hivyo walikuwa wamekutana na kwa bahati mbaya sana jamaa akakuta zile meseji zetu za kimapenzi kwenye simu ya Sofia.
Baada ya hapo jamaa alitoa kipigo cha hatari, na muda huo Sofia alikuwa amepelekwa hospitali. Aliyetoa taarifa zangu ni mdogo wake na Sofia yule aliyekuwa anasoma chuo, alipewa kibano aseme na hakuwa na namna zaidi ya kuja na hao watu mpaka nilipokuwa naishi. Baada ya maelezo mengi na mambo mengine sikuonekana kuwa na hatia katika yote yaliyokea japo ilinipotezea muda na pesa pia.
Sofia yupo mjini hapa, ni mke na mama wa watoto kadhaa, ni mama mtu mzima kwa sasa. Vijana wadogo tuwe makini na hawa wanawake, unaweza kuingia mtegoni bila kujua.