Mahusiano mabaya aliyopitia Kasinde kwenye maisha yake (uhalisia)

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,236
36,268
Habari za jumapili,

Nikiwa na akili zangu timamu, leo tarehe 29/05/2022 nimeona nisimulie moja ya mahusiano niliyopitia kwenye maisha yangu wakati wa uschana....

Sio mazuri kusimulia sababu yananiletea kumbukumbu mbaya na mapigo ya moyo hunienda mbio jasho hunitoka viganiani na miguuni na huanza kujawa na jazba.....

Akili ikaniambia hiyo kwa sasa ni historia basi naishia kuvuta pumzi nzitoo na kurejea hali ya kawaida.

Kiufupi mahala popote nnapokuwa nikiona au nikisikia mwanaume na mwanamke wanarumbana na kusikia vishindo vya kupigana huwa najiwa na hiyo hali niliyoielezea hapo juu.

Maisha haya tumepewa na aliyetuumba, yana siri nzito sana wadau wengine ni wapambe tuu na katu hawawezi elewa unachopitia.

Okay kilicho nifanya nisimulie hii leo, nimechoka kusoma nyaraka za mwanaume kamuua mkewe/ mchumba ake, mama watoto wake sababu za mapenzi.....😡😡😡😡🤬🤬🤬🤬.

Mwaka 1990 nikiwa niko kwenye ajira yangu ya kwanza tangu nitoke jeshini, nilifahamiana kaka mmoja ambaye tulijikuta tunaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Alinitongoza nami kabla sijamkubalia nilimdadisi mambo kadha wa kadha, why me, huna girl friend? Kwanini mmeachana? Lengo la kuwa na mimi ni lipi?

Kijana akamwaga sera anataka kuoa na ameona mimi namfaa kwa jicho lake tuu aliponiona mara ya kwanza.

Baada ya kukubali, kabla sijakubali kwenda kumtembelea kwake (baba yangu alinifundisha kuweka makubaliano mezani kweupe).

Mara mbili nakubaliana nae tuzungumze eneo la wazi mezani kuhusu mahusiano yetu, ile tunakaa tuu kumbe anakuwa amewasiliana na washkaji zake wanakuja wanajaa kwenye meza hata hatuwezi ongea mambo yetu tunaishia kuzungumza kama kundi la marafiki muda unaenda kila mtu anarudi kwao.

Mara ya tatu (hii sijui kwanini sikuiona kuwa si dalili nzuri) nikamwambia hii ni mara ya tatu unarudia kuita marafiki zako mimi na wewe basi.

Akajirudi na kusema anashindwa zuia marafiki zake ila safari ijayo tukaongelee nyumbani kwake huko hawawezi kuja na ataheshimu maongezi hatutagusana........!

Shida ilianzia hapa... (poor me ndo nilikuwa nimeacha kufanya maagizo niliyofundishwa na baba yangu mzazi 😪😪😪😪)

Nilifika kwake, anaishi kibachela sebleni ana kapeti tuu hakuna kiti wala stuli. Chumbani ana kitanda na kabati la nguo.....!!

Sasa tutaongea tumekaa chini sebleni...! Nje hapafai maana alikuwa amepanga vyumba vya uwani choo cha kushea na kuna wapangaji wengine hivyo mazingira ya kuongea nje hayakuwa poa.

Nikasema najiamini tukae kitandani mazungumzo yaanze.....😭😭😭😭😭

Niliishia kupewa shoo, nikalala hapohapo hadi asubuhi. Nakumbuka ilikuwa jumapili na jumatatu yake ni kazini. Alikuwa kazini anapelekwa na mkonge (gari ya kazini) akaniambia tuamke tuoge halafu dereva wake atanipitisha kwangu nivae ili niwahi kazini.
Miaka hiyo hawakuwa Na foleni barabarani hivyo hiyo ndo ukawa mwanzo wa mahusiano yetu pasi kuwekana/kukunaliana namna ya kuendana.......

Nasema ukweli ile shoo ya ile jumapili alipania aniteke na alifanikiwa.

Baada ya kuzoeana ndo naanza kuona rangi zake, waschana wake wa zamani, nikienda kwake nakuta hereni ambazo si zangu chini ya kitanda, kwenye wallet yake nakuta passport size ya mschana mwingine....!

Nikawa naumia kumuacha siwezi nikifikiria shoo....!

Akamalizia na kunionesha makucha yake akinywa pombe akilewa anavyokuwa mkorofi....!!! Keuwiiiii...!! Wivu sasa gunia la mkaa lori tatu...!!

Alikuwa na wivu balaa, nikaanza kukonda......😞😞😞😔😔😔😔😔 nikienda nyumbani baba ananiuliza mama, nini shida? Au hiyo kazi kama inakutesa tutafute nyingine.... namwambia hapana baba...

(Wababa wenye binti zenu mliotumia muda kuwalea binti kuwa imara na wajasiri, ukiona hana furaha msemeshe kama baba na binti akusimulie yanayomsibu, utanusuru maisha ya binti yako). Kwa wasio na baba zao, makaka mchukue nafasi.....

Jamaa akawa anajua ameshaniteka sifurukuti kila kitu natii halafu yeye anatongoza saa ingine mbele yangu, nakutana na meseji za wanawake zake kwenye simu, vikaratasi kwenye mifuko ya nguo ya namba za simu za waschana nikajisemea ntakufa kwa kuletewa magonjwa ambukizi.

Siku moja nikamtafuta aliyenitoa bikira, alikuwa mkoa tofauti na tunaoishi. Kipindi chote hicho huyu mchumba kila mtu anaishi kwake...

Ilikuwa mchumba kaenda kwao kijijini sikumbuki alienda kufanya nini so mie weekend nikasemeshana na aliyenitoa bikira mwisho nikajikuta napanda basi akanipokea stendi hadi kwake.

Mchana kutwa usiku kucha tunaongea na kuliwazana, sikumbuki girlfriend wake alikuwa wapi, sasa jumapili nikamwambia inabidi nirudi maana jumatatu kazini akasema utaondoka na magari ya jioni Tanga hata saa 12 unapata gari. Kufika stendi saa 12 na nusu hakuna gari, kosta wala haice hamna Duuh nikasema sikuaga kazini hii noma nikaanza kupanic halafu mchumba nae ilikuwa anarudi usiku wa jumapili...!!
Sikumuaga kama natoka nje ya mkoa...!

Jamaa aliyenitoa bikira akaniambia hapa hatuna la kufanya turudi nyumbani tukaendelee kupoozana kesho alfajiri unaondoka na gari za Mombasa saa moja na nusu uko Tanga unaingia kazini.

Nikarudi kulala kwa jamaa maliwazo kama yote, saa nne usiku mchumba anaanza kupiga simu uko wapi niko kwako kumefungwa, kule kwangu nimeibiwa...!!!
Basi hazina kama zote, jamaa akaniambia zima simu huyo utaenda kupambana nae kesho mwenyewe.

Ile nafika nyumbani ili nibadili nguo niwahi kazini kumbe mchuchu alikuwa ananisubiria aone ntarudi na nani...! Siku hiyo sikwenda kazini siku hiyo...

Alinidunda kwa mara ya kwanza, nililia maana nilishindwa kuficha kuwa nilikuwa wapi na alishika simu yangu akakuta sms za jamaa akavunja simu yangu kwa hasira.

Nilipiga yowe majirani wakaja akatoka nikajifungia ndani siku nzima, naliaaaaaa. Sijawahi kuongeza Na mwanaume huyu hata mahari hajanitolea ananipiga....!

Yes nimetoka kulala na mwanaume, yeye nakuacha Na marangi anayonionesha ya uhuni wake anafikiri siumii....!

Alikuwa na mfumo dume.

Jioni yake akarudi ananigongea sikumfungulia mlango, na simu sina maana kavunja. Alikaaa hapo nje anagonga hodi tangu saa 11 jioni hadi saa tatu usiku anaita na kuomba msamaha huku kapiga magoti mlangoni.

Nafungua mlango nikamwage takataka najua alishaondoka namkuta kibarazani akanidaka huku amenishika magoti anaomba msamaha kuwa ni hasira tuu nimsamehe hatarudia tena na kuwa ananipenda...!

Kabla sijasema lolote akanikabidhi kadi kubwaaaaa la am sorry, na boksi la simu mpya...! Akanishikisha kisha yeye akachukua matakataka akaenda kutupa akarudi kanishika mkono tukaingia ndani....

Muda wote niko kimya tuu, moyoni nilishasema huyu naachana nae mambo ya kupigana sijawezi.

Hakupoteza muda akaanza kutumia silaha aliyonayo, nilipigwa shoo usiku huo ile ya siku ya jumapili ya kwanza cha mtoto.....

Na kukandwa juu.......

Huyu mchuchu tulidumu kwenye mahusiano miaka kumi, kipindi chote hicho napigwa matukio ya kuumizwa kisaikolojia, natukanwa akilewa amani hakuna, na mara ya mwisho mwisho mwaka wa tisa akaanza kunitishia mimi ukiniletea za kuleta nakuja Na mimi najiua......

Kuna siku akaniambia shukuru sana mizimu ya kwenu, usiku wa jana kisu kiliishia kwenye shingo yako....!!

Mambo ni mengi ila hadi naachana na huyu mchuchu, hatukuwahi kufunga ndoa (sababu kapuni) ila kuna miaka kadhaa tuliishi mkoa mmoja kama mke na mume.
Aliniathiri sana kisaikolojia sanaaa kiasi kwamba nikawa wanaume wengine nikawa nawaona kama waschana wenzangu.

Hata nilipoachana nae haikuwa rahisi, alikomaa na kunitishia lazima turudiane siwezi kumuacha ameshazoea mwanamke wa kumfanya anavyotaka na anajua sitochukua hatua yeyote.....

Hadi leo nina RB yake niliifanyia lamination, matukio niliyompiga uke mwaka wa kumi akaanza kuona nina mwanaume ananishauri vibaya, mara marafiki zako wakike sio wazuri... mie kimya ila nilikuwa mkaliiii nikamwambia ukinifata nakuua mwenyewe na RB yako nimeishikilia mkononi.

Najua mtakuwa na maswali mengi sababu mengi sijayasimulia ila kiufupi huyu mchuchu ndo aliyenifanya nikajenga hulka mpya ya leo niliyonayo....

Sijali sana sababu kwanza ni historia japo ni uhalisia wa maisha yangu, kwanini leo nimeisimulia...

Natamani hii hali ya kupatwa na hofu kila ninapoona au kusoma makala mwanamke anapigwa au ameuawa kikatili iniishe....

Huu mwaka wa pili sasa nimekuwa na tabia kila ijumaa napita Mohans ya Posta nachukua aina mojawapo ya Amarula naikunywa weekend.....

Naogopa kuwa kalevi, sipendi pombe ila napenda tuu kurembua tumacho.....

Mazoezi yalinipa tafu sana baada ya kutoka kwenye mahusiano hasi, ila umri unanifanya nakuwa mvivuuu sifanyi mazoezi wala sili msosi zaidi ya matunda.

Ila leo nimejipikilisha pilau tamuuuu....😋😋.

Babu, najua utasoma hapa, nisamehe sababu sijakuomba ruhusa ya kusimulia haya. Nisamehe babu yangu mpendwa sirudii tena.

Muwe na usiku mwema, ntajibu maswali ntayoweza.

NB: kuna memba humu wanafahamu baadhi ya uhalisia wa maisha niliyopitia. Tafadhali nilikusimulia tuu ila sijakupa kibali cha kuja kuandika hapa unavyonifahamu.

Nakuheshimu sijawahi kuandika kukuhusu, naomba unirejeshee heshima hiyohiyo.

Haya nnayosimulia nimeamua mwenyewe, wewe niliyokusimulia baki nayo tuu tafadhali.

Kasinde wa Babu 😇.
 
Pole kwa yote Kasinde, tunaishi kwenye dunia ambayo ina watu wenye nafsi tofauti tofauti...

Wapo watu waliopaswa kuoa au kuolewa na majambazi, lakini utakuta wanaoa au kuolewa na manesi, hapo ndipo kunatokea kutaniko la watu na sio unganiko la mioyo iliyopaswa kuwa na hatma moja...

Ngoja nikuchokoze Kasinde, hivi wakati huo hukuwa wapiga msuba kama sasa?? 🤔🤔

📱📱 mlizitoa wapi Kasinde kipindi hiyo Mandela anapambana na makaburu
 
Pole kwa yote Kasinde, tunaishi kwenye dunia ambayo ina watu wenye nafsi tofauti tofauti...

Wapo waliopangiwa kuoa au kuolewa na majambazi, lakini utakuta wanao au kuolewa na manesi na hapo ndipo kunatokea kutaniko na sio unganiko lamioyo iliyopaswa kuwa na hatma moja...

Ngoja nikuchokoze Kasinde, hivi wakati huo hukuwa wapiga msuba kama sasa?? 🤔🤔

📱📱 mlizitoa wapi Kasinde kipindi hiyo Mandela anapambana na makaburu

Shugaaaaaa nimechekaaaaa

Well msuba nilianza kuupiga katikati karibuu nani mwisho wa kuachana na mchumba.

Hiyo ya simu ilikuwa zishaingia TZ, kuna namna nimesimulia kuondoa dots au koneksheni na uhalisia kabisa....

Nashukuru nimefanikiwa. 🤓
 
Habari za jumapili,

Nikiwa na akili zangu timamu, leo tarehe 29/05/2022 nimeona nisimulie moja ya mahusiano niliyopitia kwenye maisha yangu wakati wa uschana....

Sio mazuri kusimulia sababu yananiletea kumbukumbu mbaya na mapigo ya moyo hunienda mbio jasho hunitoka viganiani na miguuni na huanza
Kasie mda umefika Sasa Tuzeeke wote
Karbu ule pension Yangu my Sweet Bibi Kasie
 
Daah... after all we had been through... Damn it... umeona umwage mchele... umejeruhi kwa tindikali kuta tulivu za Moyo wangu... vipi mbona mema yangu huja tamka, Truly nmekuwa Shetani kwa 10 years... haya bhana... lesson learnt...Night night
 
Daah... after all we had been through... Damn it... umeona umwage mchele... umejeruhi kwa tindikali kuta tulivu za Moyo wangu... vipi mbona mema yangu huja tamka, Truly nmekuwa Shetani kwa 10 years... haya bhana... lesson learnt...Night night
Hii comment iko na feeling Kali Sana .
 
Back
Top Bottom