Kwa wale mlio kwenye mahusiano ya muda mrefu mnafanya nini kuhuisha penzi pale linapokuwa limepoa?

Hii hutokea mkuu.. hii ni kwasababu bado moyo wako unahitaji kula ujana, haujawa tayari kujifunga kwa mtu. Chakufanya jipe muda.. usikimbilie ndoani sasahivi, moyo unaamini kuna mtu bora zaidi ya unaekuwa naye wakati huo, ukijifunga kwa ndoa sasahivi utajuta. Jipe muda
 
Habari za wakati huu wanajamvi pendwa la MMU. Ni siku ya tarehe 05/05/2021 kwa wale ambao siku ya jana 04/05/2021 ilikuwa siku ndefu poleni na wale ilikuwa kinyume chake Hongera kwenu. Acha niende kwenye hoja moja kwa moja.

Nimekuwa kwenye mahusiano na binti wa mtu kwa mwaka na kitu sasa almost mwaka mmoja na nusu hivi na nimeshaenda kwao na Mahali nimetoa almost yote. Tokea mwezi huu umeanza nimekuwa napata changamoto ya upendo kupungua kwake, najitahidi sana ila najikuta nakosa hata hamu ya kuongea naye au wakati mwingine naanza kuhisi kumchoka.

Hii iliwahi nitokea kipindi fulani, nilimuumizaga binti wa watu na nilijitahidi sana kupambana na hii hali ila yeye akashindwa kuvumilia akaondoka. Na wakati huu tena binti wa watu anajitahidi kunijali na kunijulia hali mara kwa mara ila mimi daah hisia zimeanza kukata kabisa. Sasa hii hali naiona kama itanisumbua sana, nahitaji Msaada wa mawazo au mapendekezo ya namna ya kuhuisha hili penzi..! I don’t wanna hurt her.

HELP ME OUT WAKUU
Nadhani adolescence inakusumbua
anyway tenga muda mwingi wa kuwa nae ikishindikana tumia muda mwingi kuwaziliana naye
They do love care especially kumjulia Hali au hata kumpigia cm bila kuwa na sababu
 
Ila sometime mahusiano ya mda mrefu huchosha, fatilia kuna watu wanaishi kwenye mahusiano mpaka miaka 5 end of the day wanajikuta wameachana,

Kwa upande wako huo mwaka na kidogo ni mchache sana, fanya upesi umuoe, maana utakapo kuwa katika ndoa kuna vitu viwili ambavyo nakuhakikishia vitakufanya usimchoke mkeo.

1. Kama mtabahatika kupata watoto, watageuka kuwa faraja kwako na kuongeza hamasa ya upendo.

2. Kukupikia chakula na kukufulia nguo pia kuandaliwa maji ya kuogo nk. Hii itakufanya ujione tofauti na ulivyokuwa single boy maana sometime vitu getto unavipanga hovyo hovyo, hakuna mpangilio maalum wa kula chakula, au sometime chakula unakila ukiwa kitandani huku unachat and so on
 
Nadhani adolescence inakusumbua
anyway tenga muda mwingi wa kuwa nae ikishindikana tumia muda mwingi kuwaziliana naye
They do love care especially kumjulia Hali au hata kumpigia cm bila kuwa na sababu

I am 30 brother, am already out of that age.
 
Ila sometime mahusiano ya mda mrefu huchosha, fatilia kuna watu wanaishi kwenye mahusiano mpaka miaka 5 end of the day wanajikuta wameachana,

Kwa upande wako huo mwaka na kidogo ni mchache sana, fanya upesi umuoe, maana utakapo kuwa katika ndoa kuna vitu viwili ambavyo nakuhakikishia vitakufanya usimchoke mkeo.
1. Kama mtabahatika kupata watoto, watageuka kuwa faraja kwako na kuongeza hamasa ya upendo.
2. Kukupikia chakula na kukufulia nguo pia kuandaliwa maji ya kuogo nk. Hii itakufanya ujione tofauti na ulivyokuwa single boy maana sometime vitu getto unavipanga hovyo hovyo, hakuna mpangilio maalum wa kula chakula, au sometime chakula unakila ukiwa kitandani huku unachat and so on

Ahsantee kwa mchango wako ndugu, Nitajitahidi kuongeza jitihada za kumfanya niwe karibu naye
 
Habari za wakati huu wanajamvi pendwa la MMU. Ni siku ya tarehe 05/05/2021 kwa wale ambao siku ya jana 04/05/2021 ilikuwa siku ndefu poleni na wale ilikuwa kinyume chake Hongera kwenu. Acha niende kwenye hoja moja kwa moja.

Nimekuwa kwenye mahusiano na binti wa mtu kwa mwaka na kitu sasa almost mwaka mmoja na nusu hivi na nimeshaenda kwao na Mahali nimetoa almost yote. Tokea mwezi huu umeanza nimekuwa napata changamoto ya upendo kupungua kwake, najitahidi sana ila najikuta nakosa hata hamu ya kuongea naye au wakati mwingine naanza kuhisi kumchoka.

Hii iliwahi nitokea kipindi fulani, nilimuumizaga binti wa watu na nilijitahidi sana kupambana na hii hali ila yeye akashindwa kuvumilia akaondoka. Na wakati huu tena binti wa watu anajitahidi kunijali na kunijulia hali mara kwa mara ila mimi daah hisia zimeanza kukata kabisa. Sasa hii hali naiona kama itanisumbua sana, nahitaji Msaada wa mawazo au mapendekezo ya namna ya kuhuisha hili penzi..! I don’t wanna hurt her.

HELP ME OUT WAKUU
Mahusiana ni kushawishiana na kujaza mapungufu yaliyopo kwa mwingine, sina uhakika ila inawezekana msichana hana jipia na kwa kutojua ameshindwa kutambua mapungufu yako hivyo kuyajaza na Kuwa sehemu ya maisha yako, na wewe inaonekana kama ulifanya hayo yote kwa kumwonea huruma bila kuangalia kama anawajika ktk maisha yako, pia sababu zingine ni uchumi kuyumba na kutokuwa na matarajio mazuri huko mbele. Shughulikia swala la uchumi kwa nguvu zote na msikize sana kujua hisia zake pia.
 
Duh Moyo wa binadam hua unakinai Hasa kama hakuna tuvituvitu vya kuboost

Ukitaka kulijua hilo Jaribu kula kachumbar yenye nyanya tuu yani Hakuna Kitunguu wa Pilipili mbuzi
 
Pendo la Mwanadamu lina ukomo, hakika ukumpenda hyo binti na pia ulichukua maamuzi yakutoa mahali kwa mihemko yako tuu ndio.maana hilo limetokea sasa.
 
Mimi naenda mwaka wa 3 huu sometimes kweli sisikii kuongea nae but sipendi aumie so naongea nae uzuri ni muongeaji mzuri. mwaka tu dah we noma punguzeni sex kidogo.
 
Katika maisha si kila kitu ni cha kila mtu, Swali kwako mtoa mada kitu gani ambacho unafanya katika maisha yako ambacho hakijawahi kukuchosha na una crave kwacho kila mara?

Je una watu unawapenda (wazazi, ndugu, marafiki) ambao unatamani wangekuwa karibu yako kila mara? Je wewe ni mtu wa kubadili marafiki mara kwa mara au ni mtu wakustick na marafiki zako wa muda wote. Je kama wapo hakuna rafiki wa kike kati yao ambaye unampenda na kummiss mara kwa mara? Kama yupo huoni kuwa huyo ndio anapaswa kuwa mpenzi wako.

Mi naona kama huyo mpenzi uliye naye si wako, na hujawahi kukutana na mpenzi wako. Utawatesa mno watoto wa watu. Kuna watu hawana upendo, kwa athari walizopata katika mapenzi ya kwanza au mapenzi ya familia walikotoka, Inahitaji therapy ya hali ya juu sana.
 
Kaka! Achana na wanaokukatisha tamaa.. ukweli mchungu ni kwamba mapenzi ni lazima yahusishe ‘rise and falls’. Kuna magomvi, kuna kuchokana na kuna kipindi kinafika mnachukiana kabisa (refer kipindi wanandoa wanapofumaniana).

Kikubwa usisahau kwamba wewe na mwenzako mmetoka kwenye matumbo tofauti, malezi tofauti, tabia tofauti na vitu vengine kibao mnavyoyofautiana, kwaiyo ili muweze kuishi ni lazima mjifunze kukubaliana madhaifu yenu, kusikilizana (maana hakunaga mapenzi ya utemi yanayodumu), kupendana na muhimu zaidi kuwa na ‘commitment’ ya mahusiano yenu. Hapo mtaishi...

Lastly, iyo hali ni ya kawaida. Baada ya muda flani mapenzi yatarudi tena (lakini kama kweli mnapendana). Ukipata mwanamke anayeweza kuvumilia matatizo yako usimuache. Best wishes
 
Kama AY na mkewe waliachana bhasi kuna jambo gumu sana kuhusiana na kubadilisha mahusiano ya kawaida kuwa ndoa yani hata mambo madogo tu kuvumiliana ni shda. kuna muda unabaki njia panda maana ulishajicommit kwa mtoto wa watu utamuoa ila sasa ile love haipo tena yani.
 
Back
Top Bottom