Kinengunengu
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 1,719
- 4,309
Binafsi nakumbuka mara ya kwanza kuona video ilikuwa ni Late 1980"s na ilikuwa ni Sinema. Walikuja uwanjani kijijini kwetu wakihamasisha maendeleo. Waliwasha Sinema na Waliweka wimbo wa "Remmy Ongala" sikumbuki Jina ila Binafsi sikuwa najua tofauti ya Sinema na Muziki. Nikawa nacheza nikiamini ndio mziki na sio Sinema.
Baadae, Early 1990"s nikaja kuona video kwa mara ya kwanza. Kuna Askari mmoja alienda kusoma South Afrika akaja na TV/Video akawa anaweka Mikanda nasi tunaangalia kwa masharti ya kufanya/kusaidia kazi ndogondogo nyumba kwake kama kulima, kuosha vyombo n.k. Nakumbuka Mkanda wangu wa kwanza kuona ni Anord Shwazniger kuna picha moja amecheza anaenda mkomboa mwanae "Jane". Humo Anord anatumia Mabomu, Visu, Bunduki na Ndege kuangusha mabomu.
Sasa yale mabunduki na Jinsi alivyokuwa anaua watu nilijua ni kweli. Ile Jioni nimetoka angalia mkanda huo, Ndege iliyokuwa inamwaga Sumu kwa ajili ya kuua "quelea quelea " kwenye mashamba ya Mpunga ikapita. Hahaaa, nililia na kukimbia sana nikipiga kelele "Anord ananilipua/Ananiua"
Video yangu ya Pili kuangalia ni Marudio ya mechi ya Simba na Stela Abidjan.
Wewe je Mhenga, unakumbuka nini?