Kwa mara ya Kwanza nimepokea Call zaidi ya 500 na SMS 2076 ndani ya masaa 11; Vijana Nani kawaloga?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
Kwema Wakuu!

Simu yangu leo ilikuwa bize ungedhani ni Customer Care wa Voda, nimeiona, kihere here kimeniisha, hapa nimeblock all unknown Call ili simu yangu ipumzike Kwanza. Unaweza ona Masikhara lakini ndio ukweli wenyewe.

Kutokana na kile kilichotokea na kudaiwa kuwa video ya Msanii Oprah kuvuja, nikasema Acha nione nini kitatokea endapo nitaandika hivi; Anayehitaji connection ya Oprah anicheki Kwa namba 06********** nitamtumia tugawane dhambi"
Yaani nimemaliza tuu kupost haijaisha dakika moja simu na SMS zikaanza kuingia mfululizo, Kwa kweli nimestaajabu Sana.

Vijana wa kitanzania Nani aliyewaloga?
Connection ya uchi itakusaidia nini kwenye maisha yako?
Ukimuona Fulani akiwa uchi nini unapata au upuuzi tuu!

Ukiandika vya maana Mtandaoni Vijana hawana time navyo, andika upuuzi uone utavyoungwa Mkono, ninaushahidi Kwa Jambo hili Mimi binafsi.
Maandiko yenye kujenga hayapendelewi na vijana wa kitanzania, Ila andika matusi, chuki, kejeli au Stori za Mapenzi uone!

Nilikuwa napitia Ukurasa wa Kigogo2014 wa Facebook wiki hii niliona akipost angalau vitu vya maana vya kujenga jamii, kupost biashara za watu, akapost masuala ya umuhimu wa Biashara ya Fedha ya kidigitali, post zake zote zenye tija hakupata like hata Mia moja, lakini akipost matusi Kwa Viongozi au Jambo lolote negative Watanzania utaona like na comments za kutosha.

Hivi ni Nani aliwaloga Watanzania?
Ndio maana Dr. William wa Marekani anatumia mbinu ya Kutukana na kutoa maneno makali ili kupata uungwaji Mkono. Ajabu Sana hii!

Vijana wa kitanzania Nani amewaloga?

Connection sio zakuzifurahia Sana, ipo siku hapa itatokea aibu kubwa katika taifa letu Kama tabia hii haitakomeshwa, unachekelea kuona uchi wa wanawake wengine, siku ukimuona Mama yako, au Mkeo au binti yako ndio akili itawajilia.
Kuna mambo sio yakuyachekea hata kidogo.

Oooh! Aliyemuambia ajirekodi Uchi wake Nani, kwani alirekodi kwenye siku yako, wewe uliyepost uchi usiowako ndio unapaswa uchukuliwe hatua Kali za kinidhamu.

Sijui nini kinasababisha watu Kupenda wengine wakidhalilika na kuumia. Ni roho mbaya na chuki zisizo na maana.
Vijana wenye tabia hizi muache Kwa kweli. Jaribuni kujiweka katika nafasi za wahanga. Chukulia kuwa he huyo ingekuwa Mama yako ungefurahi, au angekuwa binti yako ungechekelea na kuomba Connection ya kuuona Uchi wa Mama yako au Binti Yako. Kama mmeshindwa kuwa na UTU basi kuweni hata Waungwana.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
0.1MPINA42.jpg
 
Ila hawa wasanii wajiheshimu...unajijua ww ni celebrity alafu unafanya mambo ya hovyoo...wacha mashabiki wamshabikie...
 
maana ya kupiga picha ukiwa uchi ni nini?
Maana ya kuchukuliwa video ukiwa uchi ni nini?

tunapoenda kulaumu wasaka connection tujitahidi pia kuiambia jamii iache tabia za hovyohovyo.

Mtu kujirekodi yeye mwenyewe kwenye simu yake sio tatizo.
Tatizo ni huyo mwizi wa kuchukua nyaraka za mtu mwingine na kuzihamisha bila ridhaa ya mhusika hiyo ndio sio haki.
 
Kwema Wakuu!

Simu yangu leo ilikuwa bize ungedhani ni Customer Care wa Voda, nimeiona, kihere here kimeniisha, hapa nimeblock all unknown Call ili simu yangu ipumzike Kwanza. Unaweza ona Masikhara lakini ndio ukweli wenyewe.

Kutokana na kile kilichotokea na kudaiwa kuwa video ya Msanii Oprah kuvuja, nikasema Acha nione nini kitatokea endapo nitaandika hivi; Anayehitaji connection ya Oprah anicheki Kwa namba 06********** nitamtumia tugawane dhambi"
Yaani nimemaliza tuu kupost haijaisha dakika moja simu na SMS zikaanza kuingia mfululizo, Kwa kweli nimestaajabu Sana.

Vijana wa kitanzania Nani aliyewaloga?
Connection ya uchi itakusaidia nini kwenye maisha yako?
Ukimuona Fulani akiwa uchi nini unapata au upuuzi tuu!

Ukiandika vya maana Mtandaoni Vijana hawana time navyo, andika upuuzi uone utavyoungwa Mkono, ninaushahidi Kwa Jambo hili Mimi binafsi.
Maandiko yenye kujenga hayapendelewi na vijana wa kitanzania, Ila andika matusi, chuki, kejeli au Stori za Mapenzi uone!

Nilikuwa napitia Ukurasa wa Kigogo2014 wa Facebook wiki hii niliona akipost angalau vitu vya maana vya kujenga jamii, kupost biashara za watu, akapost masuala ya umuhimu wa Biashara ya Fedha ya kidigitali, post zake zote zenye tija hakupata like hata Mia moja, lakini akipost matusi Kwa Viongozi au Jambo lolote negative Watanzania utaona like na comments za kutosha.

Hivi ni Nani aliwaloga Watanzania?
Ndio maana Dr. William wa Marekani anatumia mbinu ya Kutukana na kutoa maneno makali ili kupata uungwaji Mkono. Ajabu Sana hii!

Vijana wa kitanzania Nani amewaloga?

Connection sio zakuzifurahia Sana, ipo siku hapa itatokea aibu kubwa katika taifa letu Kama tabia hii haitakomeshwa, unachekelea kuona uchi wa wanawake wengine, siku ukimuona Mama yako, au Mkeo au binti yako ndio akili itawajilia.
Kuna mambo sio yakuyachekea hata kidogo.

Oooh! Aliyemuambia ajirekodi Uchi wake Nani, kwani alirekodi kwenye siku yako, wewe uliyepost uchi usiowako ndio unapaswa uchukuliwe hatua Kali za kinidhamu.

Sijui nini kinasababisha watu Kupenda wengine wakidhalilika na kuumia. Ni roho mbaya na chuki zisizo na maana.
Vijana wenye tabia hizi muache Kwa kweli. Jaribuni kujiweka katika nafasi za wahanga. Chukulia kuwa he huyo ingekuwa Mama yako ungefurahi, au angekuwa binti yako ungechekelea na kuomba Connection ya kuuona Uchi wa Mama yako au Binti Yako. Kama mmeshindwa kuwa na UTU basi kuweni hata Waungwana.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umewaroga wewe kwa kuwadanganya kuwa una connection kumbe huna..!! Uchawi si lazima upae kwa ungo..!! Hata kuwahadaa wenzio nao ni uchawi kama uchawi mwingine
 
Huu ugonjwa hauwezi kupona, 80% wanaenjoy kuangalia kuliko kupaza sauti kuwa KITENDO kilichofanywa si sawa, Jamii yetu IPO nyuma sana kwenye suala Zima la UDHALILISHAJI.
What happened isn't normal at all
 
Back
Top Bottom