Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
Dr.wa CCM huyu hana tofauti na fastjet!c ni kama wale wanafunzi wa kile chuo flan waliokuwa wanapewa degree kwa sbb tu ni wanamagamba

Ndio tatizo lenu chadema. Hamkubali ushauri! Ni matusi kwa kwenda mbele! Haya tuone mtafika wapi.
 
Wewe kama unazo hizo records tuwekee hapa, ni katika kikao kipi Kitila aliwahi kuelezea ushenzi walioandika kwenye waraka wao au ndugu yake Zitto pamoja na Mwigamba.

Mwigamba siku anatakwa makofi alikuwa anasifia uongozi mahili wa Mbunge Lema ndani ya kikao cha chama arusha huku anapost ushenzi JF wakati huo huo.

Kitila Mkumbo kabla waraka haujawekwa wazi siku hiyo hiyo alisifia report ya hesabu za chama.

Hawa ni wasaliti zaidi ya Yuda kama alivyosema Ngurumo, sababu Yuda alipokuwa na wenzake alikuwa kimyaaaaa, hata Yesu alipokuwa akiwauliza maswali yeye alikaa kimya, afadhali yeye alikuwa na aibu.

Hawa wahuni wanaingia kwenye vikao kusifia uongozi wakitoka wanaurushia kinyesi, hawa ni wahuni wakubwa hawa,

Kuhusu shule za kata
Kuhusu shule, usomi nilionao mimi wewe na ukoo wako itawachukua miaka kumi kutambua kwamba na nyie mnauhitaji, swala la kujielekeza kuupata nalo ni majaaliwa.
nimeipenda sentensi yako ya mwisho!
hiyo elimu ya uchawi uliyofundishwa na bibi yako ni kweli KUIPATA NI MAJAALIWA!!!!
You give the reason to love JF much more. thanx.
ila weledi wako ni wa kutiliwa shaka kwa sababu unaunga mkono wajinga(chadomo) na siku zote ndege wafananao huruka pamoja.
kamwe sitajadili kiwango chako cha elimu(kwetu hakuna wachawi) ila nitajadili kiwango chako cha kuelimika. unaweza ukawa na vyeti/shahada/stashahada zoooote ambazo mwanadamu anaweza kumiliki lakini ukawa mbumbumbu kuliko mimi mkulima wa vitunguu hapa RUAHA MBUYUNI. wewe ni mjinga na siku zote"MJINGA HUPENDA MAJIVUNO/MAJISIFU""
 
Badala ya kufanyia kazi hoja za Kitila, watu wamekazana kumjadili Kitila binafsi. Sitarajii kama viongozi wa CDM wawe na mitazamo hasi juu ya hoja za Mkumbo kama tunavyoshuhudia na kusoma humu.

Inaonekana kana kwamba kila mkosoaji ni mfuasi wa CCM, na wale wengine tulioamua kuwa neutral tukikosoa nasi twaitwa CCM.

Bila kubadilisha mbinu na bila kuyafanyia kazi mawazo mbadala kutoka kwa watu kama kina Kitila, CDM sahau kabisa kuitoa CCM madarakani.

Na sasa kipimo kingine kinakuja hivi punde (chalinze na Kalenga), safari hii mtawaambia nini washabiki wenu maana mmeamua kutia timu kwenye uwanja ule ule wenye marefarii walewale.
 
Kuna watu wanaona viongozi wa Chadema kama miungu watu hawakosei, hata siku wakisema mtuabudi watawaabudu bila kupinga, ikweli wao ni binaadamu kama sisi, wanakose, ila hawataki kukubali ndiyo maana chama hakiendi mbele, ndiyo viongozi aliosema Nyerere (RIP) mtu Ana lala nyumbani na kuchukua ushauri wa hawara yake na kuutolea maamuzi ktk chama au serikari, na watu wanawasapoti, ukipinga eti msariti, na 2015 mtapata majibu, wananchi wameshawajua na nyimbo zenu wamezichoka, tuombe uzima mtakuja kuona.

Binafsi hili mimi ndio linafanya nikae mbali na hiki chama, yani viongozi watakachosema ndio hicho hicho hakuna kuhoji na ukihoji tu imekula kwako, kama una kijinafasi kwenye chama watakuletea zengwe.

Mbaya zaidi ni hili tamko la Slaa kwamba tusinunue kazi za wasanii wanaokiunga mkono chama cha ccm, binafsi naona hii haijatulia.
 
Ndo walewale tu hawa wasomi njaa wachumia tumbo wanajifanya wanauchungu na matatizo ya hii nji lakini hakina kitu ise tumeqashtukia arifu.
 
Wakuu,

Hii makala ya Dr. Kitila ina ukali gani?

Mbona tumefikia mahali ambapo watu ndani ya vyama hata wataogopa kuandika yale wanayoyafikiria kweli kweli?

Tutabaki na hoja za kusifiana huku mambo yanaenda mrama.

Uandishi ni kama kioo na kinasaidia tu kukuonyesha ulivyo mchafu. Hata ukikuvunja kioo, uchafu hauondoki.

Dawa ni kurekebisha mapungufu yaliyopo.
 
kaka! inajulikana na kila mtu kwamba vikao vya chadema huedeshwa kibabe na havizingatii hoja wala weledi bali vinaangalia nani ni nani!!
na mpaka mpasuko ndani ya chadema unatokea ni idadi kubwa ya wajumbe wa vikao walikuwa hawahudhurii kwa sababu ya ukanjanja wa uendeshaji vikao.
kama alivyokwisha eleza Kitila, alijaribu(tena kwa ukali) kueleza mapungufu ya chama katika vikao lakini hakueleweka. unataka angefanya nini zaidi????
amini nakwambia!! CCM ni chama kinachoelekea kufa lakini hakijafa bado. na kinaweza kurudi na kuwa kipenzi cha wananchi kama wakitokeo viongozi wa kukiokoa.
lakini chadema kinakufa kabla hata hakijatimiza umri wa kubalehe. mlio na kili mufilisi hamtakubaliana na sisi kupitia humu, lakini deep in your hearts you the truth.Kitila anasimamia anachokiamini akiwa kama mtu huru asiyefungwa na itikadi zozote.lakini yeye ni muumini wa kile ninachokiamini kuwa""" tunahitaji MTU mwenye dhamira ya kweli ya kulikomboa hili taifa"" na huyo mtu asiwe wa kufikirika bali awe katoka miongoni mwetu na matendo yake yatushawishi kwamba YULE TUNAYEMTAKA NDIYE HUYU!!
kwake yeye kama nilivyo mimi, kamuona ZZK...Kosa lake li wapi!!
huu ujinga wa kuitana WASALITI,MAPANDIKIZI,---------- na misamiati mingine ya kijinga ni aina nyingine ya ukaburu ndani ya chadema. tulipambana na ukaburu wa SOUTH AFRICA, hatutashindwa kuwaangamiza makaburu wa ndani. nadhani mmeshaisoma kwenye uchaguzi wa madiwani uliopita hivi punde. nawahakikishia baada ya uchaguzi 2015 tutakifuta kabisa hiki chama. na mkumbuke baada ya 2015, raisi hatakuwa kikwete huyu anayewabeba na kuwavumilia[/QUOT

chadema haiwezi kufa kisa dr kitila au zitto kafukuzwa bali chadema itakufa pale ccm itadhubutu kuwapa unafuu wa maisha watanzania hata mara mbili ya sasa tofauti na hapo ni ndoto hata dr slaa akiondoka chama kitabaki watu wanataka ladha ya chama kingine ndugu,mark my word
 
Mkuu,
Mbona umemsahau Tundu Lissu?

Hivi wanajamvi, naomba tu kuuliza.

Mbona karibia watu woote wenye nafasi/vyeo na wasomi kutoka maeneo ya Singida wana MIDOMO sana? Mfano tu kwa uchache Nape, Mwigulu, Chiligati, Dr.Mkumbo etc

Hata niliosoma nao wako hivyo hivyo!!!

Tatizo liko wapi?????
 
unajua ukiachana na mpenzi wako visingizio huwa ni vingi vya kweli na uongo. yaani ujifungie ndani uroge na ukikamatwa useme eti naye huyo huwa ni mchawi! maajabu. zitto alikataa posho za bunge akijua kuwa ana pokea nyingi zaidi za kuhujumu chadema.
 
tanzania hatuna waandishi wa habari tuna makanjanja tu.

Huyu ansbert ngurumo ni kada wa chadema hii taaluma ya habari kaivamia, unadhani unaweza kuwahoji mbowe na slaa hawezi kwa kuwa ni mabosi wako.

Kabakia kupambana na wale wote wanaopingana mitazamo na chadema, hana tofauti na waandishi wa habari wa uhuru.

huyu ansbert hawezi kujibu hoja za kitila, yeye kazi yake ni kupambana na wanao hikosoa chadema.
 
Huna lolote Kitila, hizi zote ni njia unazotumia za kuipaka matope Chadema ili kukipaliliachama chenu cha ATC ambacho mnawasajili Wana Chadema wasiokuwa na uelewa kwa propaganda nyingi kwa mabilioni na maagizo mliyopewa na ccm.

Katibu Mkuu wa Chama chenu ni mnafiki mwenzako Mwigamba na Zitto ndiye anayefadhili mapesa huku yeye akiwa underground kama kawaida yake akiwatumia Ninyi na wengine kwa faida zake. Lakini ninachowahakikishia hata nyie hamtafika kwokwote.

Amina

Mueleze huyu .kwanza ukimwangalia Kitila anaonekana kama mpayukaji na mwenye hekima ya kulazimisha .nafikiri kama siyo alisomea saikolojia .hangekuwa bonge ya mshirikana fulani pale kijijini singida.
 
N vema Dr Kitila aachane na mambo ya siasa ajikite kwenye taaluma vimgimevyo atakosa yote
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

Mi nadhani Kitila unahoja ya msingi lkn tatizo ni kuwa ukosoaji wako umeongezeka sn baada ya matatizo yako na Chadema lkn pia unaposema tutafute mbadala wa CCM na Chadema wakati kukiwa na fununu wa uanzishwaji wa Chama ambacho inaaminika kuwa ni cha Zitto na group lake ukiwemo wewe huoni km unapigia debe Chama hicho kipya.
Na katika sababu ulizotaja zilizosababisha kuanguka kwa Chadema ktk uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita ni kwa nini hujagusia Daftari la wapiga kura wakati unajua wazi pasi na shaka kuwa mara ya mwisho watu kuandikishwa was 2010.
Na kwa mtu aliyekuwa na miaka 14 leo hii ana 18 na utafiti wa kawaida tu unaonyesha vijana wengi wanaipenda Chadema lkn hawana shahada za upigaji kura.
Nway siasa ngumu sn mm sijui wewe unafanya hayo kwa kutumiwa ama unaamini ni kwa maslahi ya Wananchi wazalendo.
Ahsante.
 
Dr Kitila, the reason you have busied yourself with writing scandalous articles about CDM is but revenge for being kicked out! If you were that bold, that paper about MM1 etc would have been in the open as these later articles! You are soliciting for public sympathy! You are dragging the win that was so near! Woe to you and your friend Zito
 
Wanahangaika hawa,mara CD, mara makala.................anajitibu kisaikolojia!,ha ha ha haa,rungu la Mwanasheria nguri LISSU lishawapiga,waende wakaanzishe iyo ACT yao!
 
unaposema cha mtu mavi unamaanisha nini?
kweli mwenye asili haachi asili.sasa hio chadema ambayo hutaki kitila mkumbo aikosoe ndio mavi ok,tunaomba ututajie mwenye mavi.

kauli hii haina tofauti na kusema chadema ina wenyewe.tunaomba ufafanuzi zaidi juu ya hayo MAVI.

Wewe unaaga mavi !? Au mpaka leo una nyeeshwa .au unatolewa mavi ndio maana ujui mavi ninini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom