Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
"Mimi najenga hoja ili kushawishi hadhira..kuna wanaokubali na wanaokataa...sina tatizo na wanaokataa...hadhira ipo hivyo na huwezi ibadilisha"- kitila
 
Utetezi wako hauna mashko wala hujajibu swali la msingi, Swali je hoja zako ulipeleka kamati kuu katika vikao vya ndani wote walipinga hadi mkaamua kuanza kuongea nje? jibu swali. na swali lingine nakuulza, Zitto hakuwahi kusema anaachana na siasa anaenda kufundisha vyuo, sasa huo uongo anaosema tatizo ni kugombea nafasi ya mwenyekiti ndani ya chama unatoka wapi? Msiwafanye watanzania Hawaelewi kiasi hicho. Huo ni usaliti no defence hapo.
 
Mimi nilikuwa namkubali sana Dr Kitila kama msomi anayejielewa, lakini kwa ushenzi alioufanya hastahili hata kuitwa Dr, anaidhalilisha elimu, halafu cha ajabu, ameharibu na bado anasimama mbele ya umma, eti alikuwa ana mpango mzuri, lile jamaa linatia aibu kweli, kenzie kazitto kameanza kutengeza cd, kanajiita kazarendo, kuutafuta umaarufu kazi, ila kuupoteza dakika moja.
 
Hivi wanajamvi, naomba tu kuuliza.

Mbona karibia watu woote wenye nafasi/vyeo na wasomi kutoka maeneo ya Singida wana MIDOMO sana? Mfano tu kwa uchache Nape, Mwigulu, Chiligati, Dr.Mkumbo etc

Hata niliosoma nao wako hivyo hivyo!!!

Tatizo liko wapi?????

Mbona Llsu humtaji au sio msingida
 
Naona anatafuta asisahaulike kama mwenzie zzk. Cha msingi ni kumchunia ili nae apotee kiaina
 
:smile-big::smile-big::smile-big:CHEZEA MKUMBO WW. HATAKI KUSAHAULIKA
 
hivi ccm leo wanafanya nini na walioonyesha nia ya kufanya nini vile...???
 
wasomi wetu hizi njaa zenu zinaliangamiza taifa
 
Baada ya kitila mkumbo kuvuliwa uanachama nadhani wengi tumeshuhudi ukosoaji na makala zake kupitia jf,magazeti na media zingine lakini nina mashaka na ukosoaji wake.

ni kweli kukosoa sisemi kwamba hastahili no!anapaswa kufanya hivyo na zaidi ila tatizo ni kwamba huo ukosoaji wake kwa sasa unafaa nini kwa chadema wakati si mwanachama wake.pili kama ni kweli mbona kasi ya ukosoaji ni kwa chadema tu na si vyama vingine.

Wakati akiwa kiongozi na mwanachama wa chadema ilikuwa rahisi kufanyia kazi ukosoaji wake na maoni yake lakini kwa leo hana tofauti na mkosoaji kutoka ccm,cuf na hata vyama vingune na atajibiwa kama wengine wanavyoweza jibiwa na hasa kuchukuliwa kama mchochezi kwa chadema.

swali langu ni je mkumbo sasa ana uchungu gani na chadema mpaka apoteze muda wake kuikosoa wakati hatasikika!

nimkumbushe kuwa cha mtu mavi ukikiona kipite.ni rahisi wengine kutoka vya vingine ila kwa yeye ambaye ni juzi tu amefukuzwa si rahisi kwa chadema kufanyia kazi maoni yake ni vema akae afanyr tathimini ya yaliyomkuta.


namshauri kwa kuwa popote pale ukifanya kitu kikatafsiriwa vibaya hata kama nii kizuri itachukua muda kuaminika kwa haraka kama chadema kuna matatizo asubiri waaibike ndio aseme kuwa aliwaambia wakamfukuza!

kwa kuwa alikuwa upinzani akipinga mfumo wa ccm na serikali yake basi ningemuona mwenye busara akiendelea kuelimisha watu juu ya mambo yanayohusu watz kama vile umasikini ,rushwa na ufisadi wa serikali lakini kuishambulia cdm ambayo si watanzania wote wanaoathirika na mgogoro wa cdm itakuwa upuuzi.

Kwa hiyo chadema ndio MAVI sio?

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

Well said Dr.
Lakini upofu wa kiakili, na utumwa wa kujitakia wa kupenda watu wa mlengo wautakao hata km ni weupe kimawazo katika kutafakari baadhi ya mambo, ndiyo gonjwa sugu linalowakabili opportunists waliopo Chama Tawala na Vyma vya upinzani sawia. Nchi inahitaji mawazo mbadala wa kuikwamua ilipo, na si ushabiki wa kambi za kisiasa.
 
Wao walijiamini kabisa kwamba mpango wao ungefanikiwa , sasa baada ya kufumaniwa na kisha kutimuliwa , IMEMSHITUA NA KUMUUMA sana ndugu KITILA , WACHUNGUZI wa mambo wanaamini kwamba kwa vile mhusika ameonyesha kuchanganyikiwa , huko mbele TUTEGEMEE MAANDISHI AMBAYO HATUTAWEZA KUYASOMA MBELE YA WATOTO !
 
Dr Kitila Mkumbo, ndoa ikivunjika ama kwa kufukuzana, talaka, au kufa kifo cha mende huwa kila mwanandoa anajitetea kivyake, ila wenye busara hukaa kimya kwani kipindi cha msukosuko ukisema neno linakuwa na jazba.

Kwa kweli sasa una uchungu, na unatamani kuona CDM inakufa sasa hivi. Kamanda hilo halitaka litokee leo au kesho, wengi wataingia na kutoka ila chama cha siasa kitaendelea kuwepo.

Naomba nikuulize mgomvi wako mkubwa na unaposema CDM unamaanisha nini? Je mwisho wako ni pale Kinondoni? Je unasahau hiki ni chama chenye wanachama wengi Tanzania na duniani.

Kama unavyoamini wewe upo sawa na wengine tunaamini tupo sawa kabisa kukutimua. Tunasubiri muanzishe huo mbadala is easy to say than do. Vitabu vipo vingi sana vyenye theory zilizofeli, ndio maana wengi waliofanikiwa duniani ni regular Jo kwani wana simple mind. You guys complicate everything.

Mtaandika sana, mtahama sana vyama, mtatumika sana, mtaishia kukosa heshima na hadhi kwani binadamu kaumbwa kuchukia ndumila kuwili.

Chadema imetoka mbali imefanikiwa sana na inakazi kubwa mbele tutafika salama, na tutazamisha yeyote mwenye anataka kutoboa mtumbwi au tutamtupa majini; haizami merikebu hapa.

Andikeni najua baada ya uchaguzi mkuu 2015 kalamu zenu zitakwenda likizo, kibaba cha mchele kitapokauka.

Dr Kitila, Zito kabwe ni msaliti wengi tunaushahidi sidhani kama unataka mabomba yaanze kumwaga maji, ninatamani sana mwende chama chochote au muanzishe chenu, kwani usaliti na majungu ya kiuongozi ni tabia. Tumieni elimu zenu kimaendeleo. Bill Gates aliweza kufanya kazi na maprofessa nguli yeye akiwa drop out, Dell aliweza kufanya kazi na wasomi nguli yeye akiwa drop out wasomi wale walielewa hawa jamaa wana mambo muhimu sana kwao na mafanikio yao, walimsikiliza na walielewana kwa miaka zaidi ya 30, ukishindwa kuelewa brain za wengine na kuwa na uwezo wa kushinda changamoto na kila siku kutaka mapinduzi haramu huwezi kufanikiwa.

Tumieni elimu zenu kufanikiwa katika maisha kiuongozi nk, kitendo cha ninyi kushindwa kutafiti risks, na faida zake pamoja na matokea yake mtalia sana.

Mimi nawaona mahayani, kwani huwezi kutuambia leo kunahitajika mbdala wakati jana ulikuwa unalia unaomba msamaha ili ubaki ndani ya chama kwanini usingejitoa na kudai mbadala wakati huna matatizo ya uhaini?
 
Yaani unatumia nguvu nyingi kutetea upuuzi....

Yaani wewe CCM eti unatumia nguvu nyingi kutuconvince sisi CDM, tukubali maneno ya Kitila ambaye tumeshamfukuza kwenye chama chetu.....

Yaani hapa nakuona kama ni m-pumba-vu tu ! Sikuoni kwamba wewe ni m-pumba-vu kwa hoja zako, bali kwa kuamini kwamba utatuconvince tumwamini Kitila pamoja na wewe.....



hapa Kitila Mkumbo ana jaribu kuonesha kuwa viongozi wa chadema hawashauriki na amethibitisha amekuwa akishauri lakini hawasikii? Hebu angalia hoja ya Kitila Mkumbo aliyo mjibu ansbert.

Nakushauri ukasome waraka wa kwanza wa kitila.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom