Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

Hivi Mr Kitila mkumbo!!? Kama baba yako anataka kujenga nyumba ya familia na ukafanikiwa kuuona mchoro wa nyumba, je! utaenda kuchora mchoro mwingine wa nyumba bila baba yako kuujua au utamwelekeza kuwa mchoro wa nyumba na hasa sehemu iliyokosewa haijakaa sawa!? na je ukienda kuchora mchoro mwingine wa nyumba ukakuta baba ameshaaanza nyumba na tayari imepauliwa, itasaidia kweli!!!??? vinginevyo kama hata kama baba yako atakubaliana na wewe itabidi kubomoa nyumba yote na kuanza upya!!! KITILA HUKUWA NA NIA NJEMA NA CDM, mimi ni mwanaccm mwaminifu sana lkn nakuhakikishia hata kama ulikuwa hujui kuwa nia yako ni ovu, nia yako haikuwa njema, ulitaka kuleta zile siasa za vyuoni kama ulivyokuwa ukifanya pale UD za kufitiana kwa siri kwa lengo la kubomoa, Nakumbuka kuna siku moja wakati tukiwa wote Pugu Secondari wewe ukiwa mwenyekiti wa bweni letu la Azimio tulipanga kugoma tena tukiwa ofisini kwako pale Azimio lkn ulitugeuka na ukaenda kumwambia Marehemu Mnyabuso kidogo tufukuzwe shule, nakumbuka tulikula mboko za kutosha za akina Charwe na Mtera na walituambia kuwa wewe ndo umesema, tena tukasodolewa mbaya kwamba eti tunajifanya kupanga mgomo kwamba ni siri kumbe tunapanga na wanafunzi wanaowapenda waalimu, kama unakumbuka ile issue Form 4 walitaka kukuchapa mpaka siku moja ukaenda kulala kwa head prefect kwa kuogopa, kulikuwa na fununu kuwa vijana walitaka kukula tigo kabisaaa kwa kuwasaliti, na aliyeongoza hii issue kama unakumbuka ni Jamaa mmoja aliitwa Peter Nolasko au Jaa galaganzi jina la utani.
KITILA wewe ni msaliti na ninajua hata hao waliokutuma utakuja kuwasaliti tu, Tatizo lako kitila una kiburi sana na unajiona wewe ni mwerevu sana na huamini wala kukubali kuwa wapo watu wanaoweza kuwa hawajasoma lkn wakawa na akili za mambo kuliko hata wewe, na ninajua kinachokusumbua ni historia yako pia na ulipotoka na mazingira uliyokulia, Kitila wewe ni Mnafiki sana na hauaminiki na kama hutaki kukubali we endelea na mipasho yako mwisho wake utaona.
 
Kuna watu wanaona viongozi wa Chadema kama miungu watu hawakosei, hata siku wakisema mtuabudi watawaabudu bila kupinga, ikweli wao ni binaadamu kama sisi, wanakose, ila hawataki kukubali ndiyo maana chama hakiendi mbele, ndiyo viongozi aliosema Nyerere (RIP) mtu Ana lala nyumbani na kuchukua ushauri wa hawara yake na kuutolea maamuzi ktk chama au serikari, na watu wanawasapoti, ukipinga eti msariti, na 2015 mtapata majibu, wananchi wameshawajua na nyimbo zenu wamezichoka, tuombe uzima mtakuja kuona.
 
Ni upuuzi kuhubiri demokrasia majukwaani halaf mnashindwa kuitekeleza ndan ya chama.Dk Kitila yupo sahihi acheni ulimbuken kwa kutetea ujinga ndan ya chama.
Ugonjwa wa wanasiasa ni kwamba hawawezi kujiangalia wenyewe,kosa daima liko kwa wengine
 
Bado Dakatri hujatujibu kwa ufasaha sisi wenye akili za kawaida, sijaelewa hivi HAKI hutafutwa gizani, hivi demokrasia inatafutwa gizani? yaani nje ya mfumo unaoelewaka wa kitaasisi- hivi ni kweli daktari unataka kutuaminisha kwamba kwamba utaratibu huo uliotumia kwa kuandika waraka wa SIRI ni sahihi na ULIKOSA kabisa njia nyingine ya kupenyeza mawazo yako ndani ya chama chako tena ukizingatia wewe ulikuwa mshauri wa chama kwenye haya haya mambo ya siasa, hii fursa iligoma kabisa, kabisa, kabisa hadi kuamua kujiunga na hao wengine kuratibu WARAKA huo kwenye giza totoro?

Hivi ni nini maudhui ya kitu kuandaliwa GIZANI, naamini hata kama ni kitu kizuri lakini watu lazima wakitilie shaka!! ni sawa na baba mwenye nyumba kukutwa anadokoa mboga kwenye chungu jikoni then ukasema hilo ni jambo la kawaida sababu mboga yenyewe kanunua yeye. hapa lazima kutakuwa na tatizo tena kubwa mno kati ya baba mwenye nyumba au familia yake kwa ujumla.

Sitaki kukuchocha najua wewe ni mwerevu sana, HOJA kuu kwa sisi watanzania wa elimu ya kawaida tunataka kujua ni kwa nini daktari ukaamua kufanya mambo GIZANI wakati ulikuwa na fursa ya kuyafanya hayo kwenye NURU? tena ukuwa na fursa tele ndani ya chama?

Mbona vikao vya chama havifanyiki Barazani kama hakuna siri
 
Hivi huyu Kitila Mkumbo ni Dr wa binaadamu, mifugo au falsafa? Hoja kuu ya ngurumo ni kwamba Hakuna records zinazoonyesha aliwahi kuwakosoa viongozi wa chama wala chama katika vikao stahiki ndani ya chama, yeye anakuja na hoja ya kuandika kwenye magazeti.

Ngurumo anasema kwa nini Kitila hakutumia fursa ya kutakiwa kujieleza kwenye kamati kuu kuelezea udhaifu na Ufisadi waliouandika kwenye waraka wao wa kishenzi kama kweli alikuwa na nia njema na chama chake, Alishindwa, ikiwa na maana kwamba ni muoga , muongo, mzandiki,pandikizi,mnafiki na msaliti.

swala la kuandika kwenye magazeti hata sisi tunaandika hapa JF.

DR Gani huyu Jamani, Hawezi kuelewa hata analalamikiwa kivipi, nadhani Ngurumo alikosea kutambua usomi wake.

Ugonjwa wa wanasiasa ni kwamba hawawezi kujiangalia wenyewe,kosa daima liko kwa wengine
 
Haya ni baadhi ya maneno yaliyoko kwenye mada ya Kitila mkumbo:

"Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache".

vikao gani zaidi ulitaka aikosoe CHADEMA?

Hivi kwanini watu wanajitoa akili.
Kitila aliwahi kugusia jambo lolote lililo kwenye waraka kwenye vikao vya chama? yeye ndio aandike tena huko raia mwema na kueleza ni kikao kipi na aliwasilishaje hoja zake za mapungufu hayo likiwemo na swala la uzinzi wa mwenyekiti wake.
 
kitila ndo unakata roho kisiasa afu pia sio lazima ufanye siasa japo siasa ni maisha kwa sasa unatapatapa tu huna hoja umepanic tulia kwanza ujipange ndipo uanze kuandika makala zako kwa sasa una hasira na chadema huwezi kuandika chochote kizuri juu ya chadema kama mimi vile ninavokuchukia kwa kuwa msaliti siwez kukuongelea mahali popote kwa mazuri.na kibaya zaidi dili yako imekufa huko ccm pia napenda ujue kuwa wewe ni muoga sana ndiyo maana mara m2 mara mapango wa mabadiliko kwa kificho
 
Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.

Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.

But it tells a lot.

Siku CHADEMA ikizikwa rasmi, MAKENE utalala njaa endelea kutetea uovu
 
Wewe kama unazo hizo records tuwekee hapa, ni katika kikao kipi Kitila aliwahi kuelezea ushenzi walioandika kwenye waraka wao au ndugu yake Zitto pamoja na Mwigamba.

Mwigamba siku anatakwa makofi alikuwa anasifia uongozi mahili wa Mbunge Lema ndani ya kikao cha chama arusha huku anapost ushenzi JF wakati huo huo.

Kitila Mkumbo kabla waraka haujawekwa wazi siku hiyo hiyo alisifia report ya hesabu za chama.

Hawa ni wasaliti zaidi ya Yuda kama alivyosema Ngurumo, sababu Yuda alipokuwa na wenzake alikuwa kimyaaaaa, hata Yesu alipokuwa akiwauliza maswali yeye alikaa kimya, afadhali yeye alikuwa na aibu.

Hawa wahuni wanaingia kwenye vikao kusifia uongozi wakitoka wanaurushia kinyesi, hawa ni wahuni wakubwa hawa,

Kuhusu shule za kata
Kuhusu shule, usomi nilionao mimi wewe na ukoo wako itawachukua miaka kumi kutambua kwamba na nyie mnauhitaji, swala la kujielekeza kuupata nalo ni majaaliwa.

Kuna faida gani kuwa msomi wakati huwezi kujieleza? ni bora ambae hajaenda shule lakini anaweza kujieleza. Na kama unajua udhaifu wako kuwa huwezi kujieleza kwa nini anakuwa wa kwanza kuhoji PhD ya Dr. Mkumbo?

Bado unonesha jinsi husivyoweza kujenga hoja, Dr. Mkumbo tayari ametoa ushahidi kwa kutaja tarehe jinsi aivyotoa ushauri kwenye vikao vya ndani vya chama. Hivyo wewe ndio unatakiwa kuleta ushaidi mwingine kuonesha kuwa Dr. anasema uwongo na siyo kuomba ushaidi mwingine wakati uliopo haujapingwa.

Nimefuahi kuona kuwa ulikuwepo kwenye kikao ambacho kilimpiga Mwigamba na kumnyanganya laptop yake, kama kiongozi wa chama anapigwa mchana kweupe mbele ya Mwenyekiti unawezaje kukana video ya Lwakatare?
 
kitila ndo unakata roho kisiasa afu pia sio lazima ufanye siasa japo siasa ni maisha kwa sasa unatapatapa tu huna hoja umepanic tulia kwanza ujipange ndipo uanze kuandika makala zako kwa sasa una hasira na chadema huwezi kuandika chochote kizuri juu ya chadema kama mimi vile ninavokuchukia kwa kuwa msaliti siwez kukuongelea mahali popote kwa mazuri.na kibaya zaidi dili yako imekufa huko ccm pia napenda ujue kuwa wewe ni muoga sana ndiyo maana mara m2 mara mapango wa mabadiliko kwa kificho

"Tabia ya hadhira ipo hivi na hatuwezi kuibadilisha"- Kitila
 
Ni uungwana na jambo la kistaarabu inapotolewa hoja inayokulenga uijibu kwa uzito wa hoja iliyotolewa. Kwa hiyo ulitaka hoja ya Ngurumo ipite bila kujibiwa ili ionekana anachosema ndicho? Uungwana ni kuacha hoja zote zitolewe ili watu wapime uzito wa hoja zote mbili. Hii tabia inayoibuka ya kupenda kusikiliza yale tu tunayotaka kuyasikia tena kutoka upande mmoja tu haitatusaidia kujenga jamii inayoheshimu uhuru wa kutoa maoni kama msingi wa demokrasia. NINAUKATAA USHAURI WAKO CATEGORICALLY!

Dr Kitila. Dalili za mkosaji ni pamoja na kutumia muda mwingi kujitetea ingawa sio wote wanaofanya hivyo ni wakosaji. Ni kama vile ukiona mtu anahitaji sabuni nyingi na maji mengi wakati wa kuoga basi ujue yawezekana kachafuka sana na kweli akawa kachafuka kwa sababu hakuwa anafanya kazi au anacheza katika mazingira yaliyo safi. Na mfamaji haachi kutapa tapa. Natumaini utanielewa
 
Kuna faida gani kuwa msomi wakati huwezi kujieleza? ni bora ambae hajaenda shule lakini anaweza kujieleza. Na kama unajua udhaifu wako kuwa huwezi kujieleza kwa nini anakuwa wa kwanza kuhoji PhD ya Dr. Mkumbo?

Bado unonesha jinsi husivyoweza kujenga hoja, Dr. Mkumbo tayari ametoa ushahidi kwa kutaja tarehe jinsi aivyotoa ushauri kwenye vikao vya ndani vya chama. Hivyo wewe ndio unatakiwa kuleta ushaidi mwingine kuonesha kuwa Dr. anasema uwongo na siyo kuomba ushaidi mwingine wakati uliopo haujapingwa.

Nimefuahi kuona kuwa ulikuwepo kwenye kikao ambacho kilimpiga Mwigamba na kumnyanganya laptop yake, kama kiongozi wa chama anapigwa mchana kweupe mbele ya Mwenyekiti unawezaje kukana video ya Lwakatare?

Tarehe alizoziandika ni za maandiko yake kwenye magazeti, nazungumzia vikao vya chama tusipotezeane muda.
 
wengine mnasema kachanganyikiwa mbishieni kwa hoja basi.mbona mnazingua tu,inaonyesha hamjui wapi mlipo.
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante
Usituchanganye kitila.umeumia sana na jamaa zako mliofukuzwa chadema ndio maana unaongea pumba.embu kaa kimya
 
Kuna watu wanaona viongozi wa Chadema kama miungu watu hawakosei, hata siku wakisema mtuabudi watawaabudu bila kupinga, ikweli wao ni binaadamu kama sisi, wanakose, ila hawataki kukubali ndiyo maana chama hakiendi mbele, ndiyo viongozi aliosema Nyerere (RIP) mtu Ana lala nyumbani na kuchukua ushauri wa hawara yake na kuutolea maamuzi ktk chama au serikari, na watu wanawasapoti, ukipinga eti msariti, na 2015 mtapata majibu, wananchi wameshawajua na nyimbo zenu wamezichoka, tuombe uzima mtakuja kuona.
 
Kejeli ni kitu cha mwisho kabisa ambacho binadamu mwenye njaa ya elimu anaweza kumtendea mtu aisyekubaliana naye. Usichanganye kabisa usomi wa Dk Kitila na hizi takataka zenu za siasa. Never try this.

Dk. Kitila namfahamu vizuri kama mwalimu wangu at Graduate level. Ni mtu very competent mno. Tena kwenye Shule Kuu ya Elimu (SOED) ninathubutu kusema hakuna mtu unayeweza kupambana naye kwa competency na commitment ya kazi. Huyu jamaa anaipenda sana kazi yake na wanafunzi tunamkubali.

Hakupata Udaktari muda mrefu, hana umri mkubwa kivile lakini kwa bidii yake ya kazi (tafiti na maandiko yake mengi ya kitaaluma ndani ya muda mfupi) sasa hivi ni mtu anayetegemewa SOED. Tena nikwambie hata kama walijaribu kumsimamisha baada ya haya makandokando ya siasa, HAWATAWEZA KUTHUBUTU kumwacha. Time will tell. Kwa hiyo usijaribu kuhusianisha siasa na usomi wake. Hilo haliwezakani.

Hata hivyo, naamini naye ni binadamu. Katika mambo ya siasa kuna mahali aliteleza kama binadamu. Mimi ningemshauri atulie. Aachane na bidii ya kutetea EGO (of course naelewa kwa nini inabidi afanye hivi kama binadamu mwenye heshima miongoni mwa wanataaluma wenzake) lakini angetulia kwanza. Ajikite kwenye shughuli zake za kitaaluma anazoziweza ipasavyo. Baadae, achague wapi pa kwenda. Tena inaweza kuwa hata CHADEMA akionyesha kutulia. Asichukue hatua zinazofanana na zile za wale vijana Mtela Mwampamba na Shonza ambao mtu unaweza kuelewa kwa nini midomo yao haina breki. Shule na njaa ni tatizo kwao but not to a prominent academician kama wewe unayepatikana kote iwe google.scholar na kwenye machapisho ya kitaaluma yenye hadhi ya kimataifa.

Dk Kitila, haya ni mapito. Utapita. Hasira na uchungu vitapita. Ni mapito.

Wewe kama kweli ni wa graduate programme lazima umebebwa yaani unaweza kuongea upu..mba..vu eti Kitila ni zaidi ya wote pale SoED!!! Duuu yaani maprofesa wote na hata PhDs zote unaona bure. Nikuambie kitu Kitila anapenda kujipendekeza kwa wanafunzu wa.ji..nga kama wewe, lakini yeye mweupe mno TENA USALITI HAJAANZA LEO, ameanza toka ni raisi wa wanafunzi UDSM 1998/99 alipotugeuka wanafunzi wote na kuungana na utawala.

Isitoshe kwaajili ya USALITI wake akaajiriwa kama ADMINISTRATOR kwenye ofisi ya CADO (sasa DVC-Administration). Wakati yeye hakiwa sio mwalimu/mhadhiri alikataa kuhidhinisha PESA YA KUJIKIMU (SUBSISTENCE ALLOWANCE) ya waalimu wote walioajiriwa miaka ya 2002-2005. Baadae akahamishwa kuwa mwalimu kama SADAKA ya watawala na kuwa MAKAMU MWENYEKITI WA UDASA, hakuna wakati ambapo UDASA UMEKUWA DORMANT KAMA KIPINDI CHAKE. In short Mkumbo is no body, he is a grand hypocrite and immature populist
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.

Mm sio pro chadema ila natofautiana kimtazamo na kitila
 
Masikini DK wangu kapanick kazi yake ni kujibizana na watu kwenye mitandao,siamini kama KITILA mfuata MKUMBO amekwisha namna hii,namsihii aendelee na kazi ya kusahihisha test pale UDSM,duh! naendelea kuamini "Intelligence is nothing to do with education"
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.

Nasubiri majibu ya Lowasa leo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom