Hivi wanajamvi, naomba tu kuuliza.
Mbona karibia watu woote wenye nafasi/vyeo na wasomi kutoka maeneo ya Singida wana MIDOMO sana? Mfano tu kwa uchache Nape, Mwigulu, Chiligati, Dr.Mkumbo etc
Hata niliosoma nao wako hivyo hivyo!!!
Tatizo liko wapi?????
Kitila ktk wasomi walionihuzunisha ni wewe badala ya kuwa chachu ya mabadiliko wewe unakuwa msaliti. Kwa kweli wewe umeshushia hadhi usomi wako.Ndugu Ngurumo,
Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.
Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.
Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.
i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.
ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.
iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.
Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.
Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.
Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.
Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?
Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.
Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!
Ahsante
Kitila
Akili yako nyepesi kama jiyu! Wewe ukiambiwa mke wa mtu sumu huelewi!Analogy nyingine, kwa hiyo CHADEMA imegeuka kinyesi?
Kinyesi cha nani sasa?
JF hii hii itakuja kuhukumu maana kila andiko litabaki hapa.
Sawa, Chadema ina mapungufu tena makubwa tu na si ya juzi, lakini kwanini kasi ya makala, kukosoa kumepamba moto sasa? Hivi leo Kitila anataka kutuambia alipokuwa anakosoa tulikuwa hatujui? Kwanini haya maneno makali makali wanazidi kuyakuza kipindi hiki?
Hivi huyu Kitila kama angekuwa anakosoa kwa kasi hii hii kabla hajafukuzwa si angejenga heshima kama mtu mwenye misimamo? Zitto aliposimama sasa ndipo alipo siku zote na tunamfahamu kwa hilo na hawezi kutushtua kwa kauli na matendo yake sasa, hata Kitila atafute justification za kiwango gani bado anazidi kutufanya tuzidi kumuweka kwenye kundi lile lile ..........
Kitila umeharibu, umekubali umeharibu, tulia tafakari hatma yako ya kisiasa ujijenge kwa namna mpya na si hii inayoonesha umejaa hasira tu za kufukuzwa na si hasira za kutaka mabadiliko.
Sorry brother....
Dr. Mkumbo amechanganyikiwa haswa alipojikuta kapigwa 2-0, kwani Chadema ilimsimamisha na baadaye kumfukuza uanachama hafu Udsm wakampokonya cheo cha Dean huko Duce kwa hali hiyo inamaana ulaji ulipungua na ambition alizokuwa nazo zikatoweka.
Hapo ni sawa na mtu aliyezungukwa na uji wa volcano pande zote hivyo hajui kama atasalimika au atakufa na huo uji.
Ndugu Ngurumo,
Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.
Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.
Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.
i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.
ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.
iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.
Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.
Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.
Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.
Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?
Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.
Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!
Ahsante
Kitila
Hakika Kitila Mkumbo ni mwiba kwa chadema.
Tukijaribu kuangalia hoja ya Ansbert ngurumo na majibu ya Kitila Mkumbo huhitaji kuwa profesa kuona kuwa Ansbert ngurumo amezidiwa mbali sana na KITILA kwenye kujenga hoja.
Yani AnsBERT NGURUMO anajaribu kuwa danganya wafuasi wa chadema na bavicha kuwa chadema hakina mapungufu na aliyo yasema kitila ni uongo na amesukumwa na hasira za kufukuzwa kitu ambacho kinaonekana si kweli kabisa.
Kitila amekuja na ushahidi unao onesha amekuwa akiki kosoa chadema akiwa ndani au nje na huu ndio mwiba ulio mzamisha Ansbert ngurumo kada mtiifu wa chadema na Mbowe.
Nataka Ansrbert ngurumo ajitokeze na yeye atuoneshe ni lini ameshawai kuandika makala ya kuhikosoa chadema au viongozi wake.
Ni wazi Ngurumo anaendeshwa na hisia kuliko ukweli na ndio maana anapigana kuukata ukweli kuwa kuna matatizo makubwa chadema.
Kitila Mkumbo amesema ukweli mtupu ambao kila leo watu wana uona kwa macho, Chadema wanafanya yanayofanywa na ccm alaf wanategemea kuhiondoa CCM madarakani.
Mambo aliyo ya orodhesha ni machache tuu ambayo yanafanywa na viongozi wa chadema ambao wana jiita wana ukombozi.
Ni wazi hakuna wa kupambana na Kitila Mkumbo ndani ya Chadema kwa hoja.
Ansbert ngurumo tuna kusubiri ujibu hoja za Kitila Mkumbo.
Hakika Kitila Mkumbo una stahili kuitwa KITILA MKOMBOZI WA FIKRA.
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.
Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.
Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.
Soma vizuri makala ya Kitila. Kama unakipenda chama basi zingatia yaliyosemwa. Acheni tabia ya kuwa mabingwa wa kukebehi tu.
Kitila, nakuheshimu sana ndugu yangu, na nitaendelea kukuheshimu. Mutasemwa sana na wenzetu, lakini musikate tamaa. Ipo siku hao wote watajua makosa yao.
Nae kashapewa buku saba as usual. Kitila umechuja
Akili yako nyepesi kama jiyu! Wewe ukiambiwa mke wa mtu sumu huelewi!
mkuu, naamini sote ni wanamageuzi ila napingana na ww kwamba dr kitila akae kimya - tusio wafuasi tunafurahi kuujua ukweli na kwa kuwa viongozi wa chadema wamo humu waje wapinge kwa ushahidi kwamba hakuwahi kuupinga / kuukosoa uongozi ndani ya vikao halali vya chama - tuache jazba, hii ndo hoja ya msingi tungependa kuona upande wa pili unasemaje kuhusu hili?!
baadhi yetu sio wafuasi, tunahoji na hakika so far dr ana hoja za msingi!!!!
===>Tulishawahi kumwambia kuwa tutamkanya akirudi,kwa sababu alikataa kusikia la mkuu!Baada ya kitila mkumbo kuvuliwa uanachama nadhani wengi tumeshuhudi ukosoaji na makala zake kupitia jf,magazeti na media zingine lakini nina mashaka na ukosoaji wake.
ni kweli kukosoa sisemi kwamba hastahili no!anapaswa kufanya hivyo na zaidi ila tatizo ni kwamba huo ukosoaji wake kwa sasa unafaa nini kwa chadema wakati si mwanachama wake.pili kama ni kweli mbona kasi ya ukosoaji ni kwa chadema tu na si vyama vingine.
Wakati akiwa kiongozi na mwanachama wa chadema ilikuwa rahisi kufanyia kazi ukosoaji wake na maoni yake lakini kwa leo hana tofauti na mkosoaji kutoka ccm,cuf na hata vyama vingune na atajibiwa kama wengine wanavyoweza jibiwa na hasa kuchukuliwa kama mchochezi kwa chadema.
swali langu ni je mkumbo sasa ana uchungu gani na chadema mpaka apoteze muda wake kuikosoa wakati hatasikika!
nimkumbushe kuwa cha mtu mavi ukikiona kipite.ni rahisi wengine kutoka vya vingine ila kwa yeye ambaye ni juzi tu amefukuzwa si rahisi kwa chadema kufanyia kazi maoni yake ni vema akae afanyr tathimini ya yaliyomkuta.
namshauri kwa kuwa popote pale ukifanya kitu kikatafsiriwa vibaya hata kama nii kizuri itachukua muda kuaminika kwa haraka kama chadema kuna matatizo asubiri waaibike ndio aseme kuwa aliwaambia wakamfukuza!
kwa kuwa alikuwa upinzani akipinga mfumo wa ccm na serikali yake basi ningemuona mwenye busara akiendelea kuelimisha watu juu ya mambo yanayohusu watz kama vile umasikini ,rushwa na ufisadi wa serikali lakini kuishambulia cdm ambayo si watanzania wote wanaoathirika na mgogoro wa cdm itakuwa upuuzi.