Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
Dr umepoteza ladha kabisa.... Kwangu huu ni uthibitisho tu wa namna ulivyo mzandiki, ulivyokuwa na mipango haramu wewe na huyo Zitto wako... Umebaki kuwa muimbaji taarabu zaidi na kutunga tuhuma za kubuni na kipumb..vu dhidi ya CHADEMA.. Lakini nakuhakikishia unafinya punda. CHADEMA ni annointed party kukomboa taifa toka katika mgando wa mawazo kama ulionao wewe... How sh.ame 2 U.

wewe ni msukule kwa 100% - kwa hiyo yeyote anayeeleza ukwel juu ya upuuzi ni muimba taarabu?! stupid comment.................
 
Tanzania hatuna waandishi wa habari tuna makanjanja tu.

Huyu Ansbert Ngurumo ni kada wa Chadema hii taaluma ya habari kaivamia, unadhani unaweza kuwahoji Mbowe na Slaa hawezi kwa kuwa ni mabosi wako.

Kabakia kupambana na wale wote wanaopingana mitazamo na Chadema, hana tofauti na waandishi wa habari wa uhuru.
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila
Jamani tujifunze kwa watoto wachanga namna ya kuwa huru. Watoto wachanga wako huru kweli kweli. Mtoto mchanga akijisikia kutoa haja kubwa au ndogo hufanya hivyo bila kujiuliza kama ni vyema kumnyea au kumkojolea mtu kwenye suti yake ya Kariakoo ama la. Yeye haja ikifika anaitoa tena bila kujiuliza maswali mengi ambayo kwake hayana msingi wowote. Vile vile wakati fulani tujifunze kuvumilia mawazo ambayo siyo tunayoyataka na hiyo ndiyo dhana nzima ya demokrasia, kinyume chake ni udikteta tu!
Tumwache Dr. Kitila aseme anachotaka kusema na mwisho ktk huo tunaoita upuuzi tutapata la kujifunza. Si inasemwa hata kichaa ana mawazo mazuri sema tu hatujipi muda mzuri kumsikiliza! Sikusoma makala ya Ngurumo lkn mm ni muumini mzuri wa Mzee wa Maswli Magumu najua kuna kitu alitoa japo sikukisoma.
Wote nawakubali nawashauri tu twende pamoja maadam tunajenga nyumba moja ya demokrasia hatuna haja ya kugombania fito.
Napita tu wanangu.
 
Dr Kitila "Mwanasiasa" wetu enzi zile za bcs.........hongera kwa hoja.......ziko makini......kwa jinsi walivyo wachambuzi wengi hapa JF wale wa siku nyingi tangu enzi za nyenzi, bcs, EF.......ninawaweka kwenye kundi la "Wanaharakati" zaidi kuliko kuwemo kwenye vyama vya siasa........

...keep it up Dr Mkumbo.....mawazo na hoja zako zinahitajika sana ili kutoa fikra/miono mingine......kwa wale waliofungiwa kwenye "Boksi".......
 
Kama ni msomi makini asingjikita kufanya siasa anazozifanya sasa bali angejitokeza rasmi na kufungua chama ili wasomi wenzake wamfuate huko na aiache cdm na watu wake

kwa aina hii ya wanazi wa chadema mabadiliko ya kisiasa 2015 ni ndoto, kwa kuwa humpendi dr kitila kwa sababu ulizoaminishwa basi ndio hutaki kusumbua kichwa chako kumsoma hoja zake?!

"Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao".

binafsi, napenda mageuzi ila kwa sasa nalazimika kutafakari hawa viongozi wa chadema upyaaa!!
 
Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.

Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.

But it tells a lot.

Msemaji wa ufipa, em tudadavulie haya;

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.
 
Jamani tujifunze kwa watoto wachanga namna ya kuwa huru. Watoto wachanga wako huru kweli kweli. Mtoto mchanga akijisikia kutoa haja kubwa au ndogo hufanya hivyo bila kujiuliza kama ni vyema kumnyea au kumkojolea mtu kwenye suti yake ya Kariakoo ama la. Yeye haja ikifika anaitoa tena bila kujiuliza maswali mengi ambayo kwake hayana msingi wowote. Vile vile wakati fulani tujifunze kuvumilia mawazo ambayo siyo tunayoyataka na hiyo ndiyo dhana nzima ya demokrasia, kinyume chake ni udikteta tu!
Tumwache Dr. Kitila aseme anachotaka kusema na mwisho ktk huo tunaoita upuuzi tutapata la kujifunza. Si inasemwa hata kichaa ana mawazo mazuri sema tu hatujipi muda mzuri kumsikiliza! Sikusoma makala ya Ngurumo lkn mm ni muumini mzuri wa Mzee wa Maswli Magumu najua kuna kitu alitoa japo sikukisoma.
Wote nawakubali nawashauri tu twende pamoja maadam tunajenga nyumba moja ya demokrasia hatuna haja ya kugombania fito.
Napita tu wanangu.

Kitila amejikosea mwenyewe kwa kitendo cha kutaka kufanya mapinduzi kwa njia haramu kuliko hiki anachofanya sasa!!
 
Hivi KITILA MKUMBO , hana kingine cha kufanya ? Kila siku kulialia na cdm tu! umetimuliwa bado unang'ang'ania kitu gani tena ? MBONA MWIGAMBA amekubali yaishe ? MNALETA USALITI HUKU BADO mna mahaba na chama ! NAKARIBIA KUKUDHARAU KABISA !
 
Msomi mwenzangu hajui hata 2015 ni nini kitajili, hajui hata kuproject, kule kwake ilamba kulikuwa na uchaguzi, eti akashindwa kupeleka nguvu yake, badala yake Ali bananga ndiye akapeleka nguvu, watu wengi hupenda nadharia kuliko uhasilia, sasa hivi ukimuuliza Dr. Kitila amejenga ofisi ngapi za chama, atakuwa hana jibu, simbezi na simdharau, maneno yamekuwa mengi kuliko vitendo, tazama ni yeye na makala, akidhani ataiuwa nguvu ya chadema, msomi mzuri baada ya kufukuzwa angetafakari, kawadhalilisha wanyilamba wenzake, leo ukimuuliza tangu amefukuzwa amewahi kurudi ilamba? Hapa kuna mgogoro wa nafsi, najiuliza Dr. Angekuwa yeye ndiye Rowasa si yangemtoka mengi? Wamejiapiza kwamba ni lazima wataiua chadema yetu macho

kwa kuwa na wasomi kama wewe chadema lazima iwe na matatizo!!
kuandika hujui, kujenga hoja hujui, matumizi ya herufi L na R hujui - unachojua ni kuunga mkono maamuzi hata ya hovyo kwa kuwa tu kasema dr slaa au mbowe!
kwa mtaji huu ni bora maccm chongo kuliko chadema vipofu!!!!!!!!!
 
kitila na mwenzako ombeni mdahalo cc ndo 2toe hoja nyie mjibu coz najua hata ngurumo anaweza akaandika mengi juu ya kitila.

Mkuu aombe mdahalo makusudi! au kwani unadhani yeye na hao wenzake ni wajinga kiasi hicho!?,Wanachokifanya hawa ni sawa na mbinu ile ya mabwana zao wa ukoo ule wa panya.Waziri anaulizwa swali au kutakiwa atoe ufafanuzi wa jambo fulani nyeti (wakati yupo wizarani kwenye ofc yake)! Anaweza kukuambia naomba muda nalifuatilia nitakupa ufafanuzi au jibu wiki ijayo!.Wakati we unasubiria uitwe ukachukue jibu au ufanunuzi kule wizarani kushtuka mwenzako ameita press Lumumba na kuongea maneno ya kujilinda!.Sasa unashangaa! Huyu mh. nilimuendea ofisini kwake(ofc ya serikali) kumuomba ufafanuzi wa jambo hili na akaniahidi nivute subira analifuatilia soon ataniita akanipe ufafanuzi niliomuomba! Badala yake amenichenga na kukimbilia kuita press kwenye ofc za chama!.Kimsingi ninachomaanisha hapa watu wa aina hii kama akina mkumbo wanachenga kwa makusudi kwa wanajua fika hawana hoja endapo watasubiri waitwe sehemu sahihi na mbele ya watu sahihi kutoa huo uzushi wanaoupandikizs kwa watu wasioufahamu ukweli wao.Huku mtaani tunawaita watu wenye tabia ya ULALAMISHI! na mtu wanamna hii ni MNAFIKI aliyekubuhu.Kitila na washirika wenzake waende wakaanzishe chama chao na si kuendeleza huu utoto hapa.
 
Kitila amejikosea mwenyewe kwa kitendo cha kutaka kufanya mapinduzi kwa njia haramu kuliko hiki anachofanya sasa!!

KITILA kwisha kazi , imebaki story ! Kwetu huku TANDIKA MWEMBEYANGA KUNA kijimsemo uchwara kwamba , UKIONA MANYOYA ....... UJUE KALIWA .....!!!!
 
Kitila huna sifa ya kusema chochote mpaka utakapo kili kwamba waraka mliouandika ilikuwa ni kosa,inasikitisha sana elimu imekupa kiburi udr bila fedha unambwembwe hivyo je ungekuwa na fedha? siojabu unasikitika kuzaliwa na wazazi ambao hawana kiwango chako cha shule,masikin umeenda shule lakin haujaelimika! unafikiri kupangilia maneno kwa ustadi kwamba ndio unakifanya kile ulichokisema kuwa sahihi sikiliza kwa faida yako MAN IS NOT QUALIFICATION,MAN IS A CHARACTER
 
Hivi KITILA MKUMBO , hana kingine cha kufanya ? Kila siku kulialia na cdm tu! umetimuliwa bado unang'ang'ania kitu gani tena ? MBONA MWIGAMBA amekubali yaishe ? MNALETA USALITI HUKU BADO mna mahaba na chama ! NAKARIBIA KUKUDHARAU KABISA !

mkuu, naamini sote ni wanamageuzi ila napingana na ww kwamba dr kitila akae kimya - tusio wafuasi tunafurahi kuujua ukweli na kwa kuwa viongozi wa chadema wamo humu waje wapinge kwa ushahidi kwamba hakuwahi kuupinga / kuukosoa uongozi ndani ya vikao halali vya chama - tuache jazba, hii ndo hoja ya msingi tungependa kuona upande wa pili unasemaje kuhusu hili?!
baadhi yetu sio wafuasi, tunahoji na hakika so far dr ana hoja za msingi!!!!
 
Km kitila anaweza kunithibitishia hapa kwamba anaweza kuja na kujibu swali langu,aje aniruhusu nimuulize swali dogo tu lkn lenye faida elf 80.
 
Hakika Kitila Mkumbo ni mwiba kwa chadema.

Tukijaribu kuangalia hoja ya Ansbert ngurumo na majibu ya Kitila Mkumbo huhitaji kuwa profesa kuona kuwa Ansbert ngurumo amezidiwa mbali sana na KITILA kwenye kujenga hoja.

Yani AnsBERT NGURUMO anajaribu kuwa danganya wafuasi wa chadema na bavicha kuwa chadema hakina mapungufu na aliyo yasema kitila ni uongo na amesukumwa na hasira za kufukuzwa kitu ambacho kinaonekana si kweli kabisa.

Kitila amekuja na ushahidi unao onesha amekuwa akiki kosoa chadema akiwa ndani au nje na huu ndio mwiba ulio mzamisha Ansbert ngurumo kada mtiifu wa chadema na Mbowe.

Nataka Ansrbert ngurumo ajitokeze na yeye atuoneshe ni lini ameshawai kuandika makala ya kuhikosoa chadema au viongozi wake.

Ni wazi Ngurumo anaendeshwa na hisia kuliko ukweli na ndio maana anapigana kuukata ukweli kuwa kuna matatizo makubwa chadema.

Kitila Mkumbo amesema ukweli mtupu ambao kila leo watu wana uona kwa macho, Chadema wanafanya yanayofanywa na ccm alaf wanategemea kuhiondoa CCM madarakani.

Mambo aliyo ya orodhesha ni machache tuu ambayo yanafanywa na viongozi wa chadema ambao wana jiita wana ukombozi.

Ni wazi hakuna wa kupambana na Kitila Mkumbo ndani ya Chadema kwa hoja.

Ansbert ngurumo tuna kusubiri ujibu hoja za Kitila Mkumbo.

Hakika Kitila Mkumbo una stahili kuitwa KITILA MKOMBOZI WA FIKRA.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom