Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
hakuna haja ya kuhangaika na mtu ambaye kwa sasa yuko nje ya cdm , nguvu zetu tunazielekeza huko KALENGA .

mkuu, kwa kukwepa hoja zenye ukweli daima chama hakitafanya vizuri, tutajikausha na kukimbilia huko kalenga badala yake matokeo yakitoka tunapata kichapo kisha tunarudi tena hapa jamvini kama kawaida yetu na visingizio vile vile...............tusikwepe tatazo, tulikabili!!
 
mkuu.

Umenikumbusha kitu cha msingi sana! Mwaka 2012 kule iramba kuifanyika uchaguzi wa kata ya ulugu, msimamizi wa operation wa karibu kwenye kampeni zile alikuwa huyuhuyu dr m1, lakini kwa kuwa nadharia za uandishi nyuma ya kipakatwa haziendani na uhalisia kwenye field, ccm walishinda uchaguzi ule na dr m1 huyuhuyu akishuhudia kata ikiende ccm, anakumbuka sana lakini kwa kuwa ameandika akiwa na frustrations katika kipindi hiki kigumu kwake ni bahati mbaya kwamba anayo andika hayawezi kuwa na mashiko kwa kuwa ni amekiri ana hasira.

kama umefatilia toka mwanzo wa huu mjadala utagundua kuwa haya ni majibu kwa ansbert baada ya kujibu waraka wa kitila ulio jaribu kuonesha kuwa chadema kuna matatizo mengi na yamechangiwa na viongozi wenyewe kuto sikiliza na kuto penda kukusolewa.

Na hapa leo amejaribu kuonesha kuwa alisha jaribu kushauri na kukikosoa chama chenu akiwa ndani na nje.

Matokeo ya juzi.ni matunda ya viongozi wenu wasio penda kusikia au kukosolewa.

Naomba ujibu hoja, hatutegemei chadema kuchukua kata zote lakini kupata kata 3 kati ya 27 kuna tatizo sehemu.
 
Mkuu.

Umenikumbusha kitu cha msingi sana! mwaka 2012 kule Iramba kuifanyika uchaguzi wa kata ya Ulugu, msimamizi wa operation wa karibu kwenye kampeni zile alikuwa huyuhuyu Dr M1, lakini kwa kuwa nadharia za uandishi nyuma ya kipakatwa haziendani na uhalisia kwenye Field, CCM walishinda uchaguzi ule na Dr M1 huyuhuyu akishuhudia kata ikiende CCM, Anakumbuka sana lakini kwa kuwa ameandika akiwa na frustrations katika kipindi hiki kigumu kwake ni bahati mbaya kwamba anayo andika hayawezi kuwa na mashiko kwa kuwa ni amekiri ana hasira.

Haya ndio ninayozungumza, hawa walikuwepo kwenye chama na kama wanavyojinadi wenyewe wamesaidia kuifikisha Chadema ilipo! Sasa mtu anayesema ametoa mchango mkubwa hadi chama kilipofikia alafu huyo huyo anasema chama hiki ni kama CCM utaelewa nini.

Yaani kila mtu anayewajibishwa Chadema ni Slaa na Mbowe! Kuna watu wanajiona kama malaika usinyanyue mdomo kwao! Usomi wetu wa Kibongo umejaa ushamba! Huwezi kusikia haya nchi zilizoendelea degrees za mtu kumfanya aone yeye yuko sahihi kila anachofikiria.

Kwanza hawa wasomi wetu wamejaa malalamiko kuliko kuchukua hatua kama Kitila anavyolalamika akisubiri "vilaza" waanzishe vyama alafu baada aje awalalamike kuwa si wasomi na hawawezi kuongoza.
 
Baada ya kitila mkumbo kuvuliwa uanachama nadhani wengi tumeshuhudi ukosoaji na makala zake kupitia jf,magazeti na media zingine lakini nina mashaka na ukosoaji wake.

ni kweli kukosoa sisemi kwamba hastahili no!anapaswa kufanya hivyo na zaidi ila tatizo ni kwamba huo ukosoaji wake kwa sasa unafaa nini kwa chadema wakati si mwanachama wake.pili kama ni kweli mbona kasi ya ukosoaji ni kwa chadema tu na si vyama vingine.

Wakati akiwa kiongozi na mwanachama wa chadema ilikuwa rahisi kufanyia kazi ukosoaji wake na maoni yake lakini kwa leo hana tofauti na mkosoaji kutoka ccm,cuf na hata vyama vingune na atajibiwa kama wengine wanavyoweza jibiwa na hasa kuchukuliwa kama mchochezi kwa chadema.

swali langu ni je mkumbo sasa ana uchungu gani na chadema mpaka apoteze muda wake kuikosoa wakati hatasikika!

nimkumbushe kuwa cha mtu mavi ukikiona kipite.ni rahisi wengine kutoka vya vingine ila kwa yeye ambaye ni juzi tu amefukuzwa si rahisi kwa chadema kufanyia kazi maoni yake ni vema akae afanyr tathimini ya yaliyomkuta.

namshauri kwa kuwa popote pale ukifanya kitu kikatafsiriwa vibaya hata kama nii kizuri itachukua muda kuaminika kwa haraka kama chadema kuna matatizo asubiri waaibike ndio aseme kuwa aliwaambia wakamfukuza!

kwa kuwa alikuwa upinzani akipinga mfumo wa ccm na serikali yake basi ningemuona mwenye busara akiendelea kuelimisha watu juu ya mambo yanayohusu watz kama vile umasikini ,rushwa na ufisadi wa serikali lakini kuishambulia cdm ambayo si watanzania wote wanaoathirika na mgogoro wa cdm itakuwa upuuzi.
 
dr. Kitila tumbo hapo tu ana elimu lkn hajitambui sijui angekuwaje kama angekuwa hajasoma.

Watu wenye safari moja hamuwezi kufichana jambo la kuwafikisha salama mnapotarajia kufika.

hivi unafikiri hizi kejeli ndio zitazima hoja iliyopo mezani?
Hata hivyo hakuna asiyejua mnapozidiwa mnaleta viroja.

Tunaomba mmwambie ansbert ngurumo au kiongozi yeyote wa chadema kuwa aje athubitishe kuwa yaliyo semwa ni uongo.
 
kama umefatilia toka mwanzo wa huu mjadala utagundua kuwa haya ni majibu kwa ansbert baada ya kujibu waraka wa kitila ulio jaribu kuonesha kuwa chadema kuna matatizo mengi na yamechangiwa na viongozi wenyewe kuto sikiliza na kuto penda kukusolewa.

Na hapa leo amejaribu kuonesha kuwa alisha jaribu kushauri na kukikosoa chama chenu akiwa ndani na nje.

Matokeo ya juzi.ni matunda ya viongozi wenu wasio penda kusikia au kukosolewa.

Naomba ujibu hoja, hatutegemei chadema kuchukua kata zote lakini kupata kata 3 kati ya 27 kuna tatizo sehemu.

Unajua Kitila alikuwa na nafasi gani Chadema na kwa muda gani? Kwa kile cheo chake anaweza kutuwekea hapa paper zake alizowahi kuziwasilisha kwa uongozi kama ushauri wake uliofanyiwa utafiti wa kutosha na haukupokelewa? Au ndio zile makala za magazetini ndio tunaambiwa "niliwashauri sana Mbowe na Slaa"
 
Mkuu, kosa la Mkumbo ni ujinga na upuuzi wa kutengeneza waraka nje ya vikao na taratibu za chama. Kama unaona hiyo ni sahihi basi wachukue wakusaidie kwenye kujenga demokrasia kwenu

Sijawahi kuona sehemu yoyote duniani eti mtu anaomba kibali cha kutengeneza mkakati wa ushindi kutoka kwa mpinzani wake. Only in Chadema.
 
Baada ya kitila mkumbo kuvuliwa uanachama nadhani wengi tumeshuhudi ukosoaji na makala zake kupitia jf,magazeti na media zingine lakini nina mashaka na ukosoaji wake.

ni kweli kukosoa sisemi kwamba hastahili no!anapaswa kufanya hivyo na zaidi ila tatizo ni kwamba huo ukosoaji wake kwa sasa unafaa nini kwa chadema wakati si mwanachama wake.pili kama ni kweli mbona kasi ya ukosoaji ni kwa chadema tu na si vyama vingine.

Wakati akiwa kiongozi na mwanachama wa chadema ilikuwa rahisi kufanyia kazi ukosoaji wake na maoni yake lakini kwa leo hana tofauti na mkosoaji kutoka ccm,cuf na hata vyama vingune na atajibiwa kama wengine wanavyoweza jibiwa na hasa kuchukuliwa kama mchochezi kwa chadema.

swali langu ni je mkumbo sasa ana uchungu gani na chadema mpaka apoteze muda wake kuikosoa wakati hatasikika!

nimkumbushe kuwa cha mtu mavi ukikiona kipite.ni rahisi wengine kutoka vya vingine ila kwa yeye ambaye ni juzi tu amefukuzwa si rahisi kwa chadema kufanyia kazi maoni yake ni vema akae afanyr tathimini ya yaliyomkuta.

namshauri kwa kuwa popote pale ukifanya kitu kikatafsiriwa vibaya hata kama nii kizuri itachukua muda kuaminika kwa haraka kama chadema kuna matatizo asubiri waaibike ndio aseme kuwa aliwaambia wakamfukuza!

kwa kuwa alikuwa upinzani akipinga mfumo wa ccm na serikali yake basi ningemuona mwenye busara akiendelea kuelimisha watu juu ya mambo yanayohusu watz kama vile umasikini ,rushwa na ufisadi wa serikali lakini kuishambulia cdm ambayo si watanzania wote wanaoathirika na mgogoro wa cdm itakuwa upuuzi.

Asante kwa ushauri mzuri, Mie nakuunga mkono. Alikuwa wapi kuandika kabla hajafukuzwa? Kuendelelea kuandika na kukosoa kosoa kunatuthibitishia wazi wazi kwamba hawa jamaa walikuwa na kazi maalum waliyotumwa kufanya sasa walishtukiwa kabla hawajkamilisha, sasa inabidi kuwaonyesha wenye kuwatuma kwamba bado kazi wanaimudu na kwamba watafaniikiwa tu.
 
Kitila You know the words but you miss their meaning! kushawishi umma kwa mbinu za kisaliti! please Kitila give me a break!
Yawezekana ulijaribu kushauri na kukosoa CDM from within and without; lakini kula njama wazi wazi kwa kuandika na kuhariri document ya kisaliti hiyo sio "evidence based writting" ni usaliti per se.
Wengi wetu hatuhitaji kuwa Wole Soyinka au the late Chinua Achebe kulitambua hilo, na wala makala zako hazihitaji shahada ya uzamivu kuzidadavua.
kwa hiyo Bwana Kitila endelea kujiliwaza kwa kuandika makala ndefu; just to while away your time; enzi zako za ushawihi katika jamii hii kwishnei! Ulikubali akili ndogo za Zitto na Mwigamba zitawale akili yako kubwa; you only have yourself to blame sio Ansbert Ngurumo. Sishawishiki n'go!
Utabakia kuwa nostalgic.
Kitila kama Zitto; aliruhusu umaarufu kujenga ukungu katika ubongo wake, akaridhika kwamba yeye ni msomi gwiji hakuna mfano wake Nji hii!!!!!!!!
 
Mkumbo has the right in telling his mind to his readers.He only lacks the truth.The truth if he will tell will set him free.
 
Mkuu.

Umenikumbusha kitu cha msingi sana! mwaka 2012 kule Iramba kuifanyika uchaguzi wa kata ya Ulugu, msimamizi wa operation wa karibu kwenye kampeni zile alikuwa huyuhuyu Dr M1, lakini kwa kuwa nadharia za uandishi nyuma ya kipakatwa haziendani na uhalisia kwenye Field, CCM walishinda uchaguzi ule na Dr M1 huyuhuyu akishuhudia kata ikiende CCM, Anakumbuka sana lakini kwa kuwa ameandika akiwa na frustrations katika kipindi hiki kigumu kwake ni bahati mbaya kwamba anayo andika hayawezi kuwa na mashiko kwa kuwa ni amekiri ana hasira.
Wewe unamsema Dr.Kitila, wakati wewe kwenye kata uliyozaliwa juzi tu kwenye Uchaguzi wa Madiwani CCM wamepita bila kupingwa.

Wewe mwenyewe haukubaliki kwenu umeshindwa hata kugombea kwa kuogopa aibu.

Bavicha bana.
 
sina tatizo na hoja za kitila mkumbo ila tatizo langu ni kuwa yeye si mwanachama tena sasa anauchungu wa nini kwa cdm?angeanzisha mradi mwingine afanye.

huhitaji kuwa mwana chama wa chama chochote kuyasema aliyo yasema Kitila Mkumbo.
 
Last edited by a moderator:
Hata cc mateja na wavuta bangi tunaheshimu taratibu, kanuni na sheria tunazojiwekea gheto na maskani na akijitokeza mnafiki/msaliti adhabu atakayopata ni kali na ikiwezekana kifo kabisa

Asante Ndugu yangu Naloli kwakweli hili nikiri sikulijua kwamba hata hapo pana utaratibu,next time sitatumia mfano huo tenakwa muda ili nifanye kautafiti kidogo kuhusiana na hii post yako umenipa kitu kipya kidogo kwani iwapo hapo pana utaratibu na unaheshimiwa ....itakuwa funzo hata kwa viongozi wetu wa Bunge...
 
Dr. Mkumbo amechanganyikiwa haswa alipojikuta kapigwa 2-0, kwani Chadema ilimsimamisha na baadaye kumfukuza uanachama hafu Udsm wakampokonya cheo cha Dean huko Duce kwa hali hiyo inamaana ulaji ulipungua na ambition alizokuwa nazo zikatoweka.
Hapo ni sawa na mtu aliyezungukwa na uji wa volcano pande zote hivyo hajui kama atasalimika au atakufa na huo uji.

Baada ya kitila mkumbo kuvuliwa uanachama nadhani wengi tumeshuhudi ukosoaji na makala zake kupitia jf,magazeti na media zingine lakini nina mashaka na ukosoaji wake.

ni kweli kukosoa sisemi kwamba hastahili no!anapaswa kufanya hivyo na zaidi ila tatizo ni kwamba huo ukosoaji wake kwa sasa unafaa nini kwa chadema wakati si mwanachama wake.pili kama ni kweli mbona kasi ya ukosoaji ni kwa chadema tu na si vyama vingine.

Wakati akiwa kiongozi na mwanachama wa chadema ilikuwa rahisi kufanyia kazi ukosoaji wake na maoni yake lakini kwa leo hana tofauti na mkosoaji kutoka ccm,cuf na hata vyama vingune na atajibiwa kama wengine wanavyoweza jibiwa na hasa kuchukuliwa kama mchochezi kwa chadema.

swali langu ni je mkumbo sasa ana uchungu gani na chadema mpaka apoteze muda wake kuikosoa wakati hatasikika!

nimkumbushe kuwa cha mtu mavi ukikiona kipite.ni rahisi wengine kutoka vya vingine ila kwa yeye ambaye ni juzi tu amefukuzwa si rahisi kwa chadema kufanyia kazi maoni yake ni vema akae afanyr tathimini ya yaliyomkuta.

namshauri kwa kuwa popote pale ukifanya kitu kikatafsiriwa vibaya hata kama nii kizuri itachukua muda kuaminika kwa haraka kama chadema kuna matatizo asubiri waaibike ndio aseme kuwa aliwaambia wakamfukuza!

kwa kuwa alikuwa upinzani akipinga mfumo wa ccm na serikali yake basi ningemuona mwenye busara akiendelea kuelimisha watu juu ya mambo yanayohusu watz kama vile umasikini ,rushwa na ufisadi wa serikali lakini kuishambulia cdm ambayo si watanzania wote wanaoathirika na mgogoro wa cdm itakuwa upuuzi.
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

Huna lolote Kitila, hizi zote ni njia unazotumia za kuipaka matope Chadema ili kukipaliliachama chenu cha ATC ambacho mnawasajili Wana Chadema wasiokuwa na uelewa kwa propaganda nyingi kwa mabilioni na maagizo mliyopewa na ccm.

Katibu Mkuu wa Chama chenu ni mnafiki mwenzako Mwigamba na Zitto ndiye anayefadhili mapesa huku yeye akiwa underground kama kawaida yake akiwatumia Ninyi na wengine kwa faida zake. Lakini ninachowahakikishia hata nyie hamtafika kwokwote.

Amina
 
Unajua Kitila alikuwa na nafasi gani Chadema na kwa muda gani? Kwa kile cheo chake anaweza kutuwekea hapa paper zake alizowahi kuziwasilisha kwa uongozi kama ushauri wake uliofanyiwa utafiti wa kutosha na haukupokelewa? Au ndio zile makala za magazetini ndio tunaambiwa "niliwashauri sana Mbowe na Slaa"

kweli kazi ipo, kwa hiyo kulikuwa na makubaliano ya kisheria kati ya dr na cc ya chadema kwamba ushauri wake ni lazima uwasilishwe kama 'papers'?!
kamanda hii kali, sasa nabaki kuwa msomaji tu ktk uzi huu...........................
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.

dr kitila tia akili mukichwa, shtuka pale unapoona wafuasi wa ccm wanakusifu na kukupamba,

hawana jema hao wamemgeuza best yako zito km k....ndomu sasa wamembwaga, hawezi tena kupanda jukwaani amebaki ktoa CDs kama muimba taarabu
 
hapa Kitila Mkumbo ana jaribu kuonesha kuwa viongozi wa chadema hawashauriki na amethibitisha amekuwa akishauri lakini hawasikii? Hebu angalia hoja ya Kitila Mkumbo aliyo mjibu ansbert.

Nakushauri ukasome waraka wa kwanza wa kitila.

hawo viongozi anaomaanisha kitila ni pamoja na Zito kupata viti vichache vya udiwani ktk uchaguzi wa2010 ukilinganisha na umaarufu alionao zito
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom