Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
kitila yuko sahihi. Tatizo wanaompinga wanampinga kwa hisia zaidi na sio kwa hoja. CHADEMA wasimame wakatae kuwa kwenye ilani na kampeni na walivyoingia bungeni hawakutangaza kuacha kupokea posho za vikao; wakatae kuwa mbowe hakurudisha shangingi la serikali na akalirudia; wakatae kuwa wabunge wao hawatumii mashanagingi; wakatae kuwa slaa aliahidi akishinda urais atatumia landcruiser mkonge lakini leo hii anatumia shangingi la chama; wakate kuwa kitaifa wanajilipa mamilioni huku majimbni wakifa njaa. Nadhani wakisema ukweli katika haya ndipo tutaona kuwa hawako sawa na wauza tembo. Wakati ccm wanauza tembo chadema wanatumia jasho la wafuasi wao kujipatia ruzuku inayoishia kwenye akaunti zao. Naunga mkono hoja tunahitaji mbadala
 
sasa kama kitila ni foreseer kama anavyoona 2015 si aanzishe chama chake kiwe mbadala ya hiyo ccm? kanyang'anywa tonge mdomoni analialia tu. ama kweli mshahara wa dhambi....... yameshamfika!!!
 
Kitila, huna la maana na nikigundua unamsomesha mwanangu namhamisha chuo! Kwa taarifa yako umesoma haukuelimika, siasa unayoiongea si kwa Tanzania wala Afrika ni ya kufikirika na itafanyika miaka 150 ijayo. Wewe ulikuwa mjumbe wa cc ya CDM halafu unashindwa kujenga hoja ndani ya cc unaandika mikakati ya mageuzi? haufai na siasa hauijui na utaishia hapo ulipofika!

Mkuu umemaliza yote, Kitila alikuwa CHADEMAkwa mpango maalumu, masikini alituchota akili tuka muamini, lakini Mungu mkubwa wameumbuka kabla ya kufaniksha azma yao ! Mungu na awapatilize kwa nia zenu ovu

 
Hizi story za kila siku baada ya chaguzi za kusema tumeibiwa kura, NEC ni sehemu ya CCM, Polisi wanashirikiana na CCM ni kutafuta sympathy na kichaka cha kuficha aibu kwenye umma. Kuanzia mwaka 1995 tunasikia story hizi hizi kutoka kwa wapinzani kiasi kwamba badala ya kudhani kama niza kweli kwa sasa zinakuwa ni kichaka cha kuficha mapungufu ya wapinzani katika chaguzi.

Kwa sasa wapinzani tayari wameishaanza kutafuta wagombea kwenye majimbo ya uchaguzi Kalenga na Chalinze kwenye uchaguzi ambao mazingira ni yaleyale ambayo wanapiga kelele kila mara baada ya kushindwa chaguzi.

Kwa nini wanaenda kwenye chaguzi ambazo wanafahamu kama mazingira katika mchakato wa uchaguzi siyo equal and conducive kwa wagombea wote.

Wamefanya nini katika kupambana na hali hasi wanayodai inawafanya washindwe katika chaguzi kwa sababu kwa sasa zimepita chaguzi kuu nne and countless by-election.

Kwenda kwenye chaguzi ina maana umekubaliana na outcome ya uchaguzi, kwa maana kuwa kuna kushinda na kushindwa.

They need do something or stop whining.
 
Chopa tatu viti vitatu ndo habari ya mjini,hiv CCM haina pesa za kukodi Chopa???Wachaga wanapesa!!!
 
Je, ni mwanzo wa mwisho wa Zitto?

05/02/2014 | Posted by Nkwazi Nkuzi | Makala | 0 comments | 502 views


YAMEISHAANDIKWA mengi kuhusiana na hatima ya kisiasa ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe.

Kitu kimoja tu hakijaandikwa. Nacho ni kuandika tanzia yake kisiasa.

Ukiangalia uzito wa hali ya mpapariko na mparaganyiko aliyomo Kabwe, unashawishika kuandika tanzia. Hata hivyo, siandiki hii tanzia. Wengine watafanya hivyo.

Leo nitaongelea mgogoro wa CHADEMA. Rejea kile kilichoitwa Waraka wa Kuhujumu Chama wa Kitila – Zitto – Mwigamba. Sitaki kudurusu kesi iliyoko mahakamani kama ilivyofunguliwa na Kabwe kwa vile naheshimu mahakama sana.

Ninachoweza kusema ni kwamba ubunge wa Kabwe kwa sasa unatokana na mahakama na si chama chake. Hivyo, punde si punde, Kabwe atakuwa historia ndani ya CHADEMA na sasa nyingine kwenye duru za kisiasa nchini, vinginevyo itokee miujiza.

Wengi wanahoji Kabwe atakwenda wapi baada ya kutimuliwa toka CHADEMA? Nadhani Ansbert Ngurumo alitoa jibu la swali hili kwenye safu yake ya Maswali Magumu ya tarehe 12 Januari.

Sitaki nirudie alichoandika Ngurumo. Ila naweza kusema kuwa darasa lake la walipo wale wanasiasa machachari, tena wengine toka CHADEMA hiyo hiyo wakiwa na vyeo vikubwa kuliko vya Kabwe, ni jibu tosha kwa Kabwe ambaye linapaswa kumfikirisha ili ajiandae kisaikolojia kwa pigo na anguko hili la ghafla.

Kwanini nasema Kabwe au Mkumbo waandike tanzia yao kisiasa?

Kwanza, kukiri kwa Mkumbo Kitila ndiyo ushahidi utakaotumika kumfukuza Kabwe uanachama.

Kwa kukubali kuwa waliandika waraka uliokuwa na lengo la kuhujumu chama, watatu hawa walifanya kile ambacho Wahindi huita ‘suttee’ ambapo mara nyingi wanawake waliochoka na maisha hujichoma moto.

Pili, kile kitendo cha Mkumbo kusema waraka wao haukuwa kosa, lakini akaomba msamaha, ni ushahidi wa kutapatapa ambao ulisaidia CHADEMA kumtimua uanachama. Na hawawezi kusema walionewa. Walifungwa kwa maneno yao wenyewe.

Tatu, kama wenzake Kabwe wamevuliwa uanachama kwa kosa lile lile atanusurika vipi?

Nne, hakuna kitu kiliwavua nguo wahusika na kuwaonyesha kama wababaishaji kama kitendo cha kutaka kujiuzulu ili waondoke kwa heshima.

Wengi walihoji: Kama walichotenda si kosa walitaka kujiuzulu kwa sababu gani?

Tano, wapo waliodhani kuwa Kabwe na wenzake “wangemwaga mtama” kwa maana ya kufichua maovu ya CHADEMA. Bahati nzuri, japo nia ya namna hii ilikuwapo, hapakuwapo na “mtama” wa kumwaga ikizingatiwa kuwa CHADEMA wanafanya mambo yao wazi wazi kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Kwa ngoa na usongo alivyonavyo Kabwe, kama kungekuwa na maovu yoyote yaliyotendwa na chama au viongozi wake, bila shaka asingeyataja tu bali angeyaimba kama shairi ili angalau kujifariji baada ya kupata lililompata.

Waswahili walisema: Ivumayo haidumu (hasa inapovumishwa pale isipostahiki kuvuma). Emma Bombeck katika kitabu chake “At Wit’s End”, aliwahi kusema; “Don’t confuse fame with success – usichanganye umaarufu na mafanikio.”

Naye Oprah Winfrey amewahi kusema; “If you come to fame not understanding who you are, it will define who you are – Kama ukiwa maarufu bila kujijua umaarufu utakuumbua.”

Nadhani hili ndilo linawasumbua wengi wanaokabiliwa na hali kama ya Kabwe. Hufiki mbali. Kutojitambua ni sehemu ya utoto ambao si kuvaa nepi bali kutenda kitoto, hata atendaye hivyo awe mtu mzima vipi.

Kabwe kweli alivuma kutokana na sababu mbaya tu. Au tuseme ajali ya kisiasa. Alivuma pale alipojitokeza kuwa mpambanaji mzuri na mtetezi wa haki za wananchi. Baada ya sifa kuingia kichwani, alifikia mahali kusema eti angetaja majina ya vigogo walioficha pesa ughaibuni. Baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kumvua nguo, Kabwe aliishia kunywea kwa aibu ya kuongopa na kuzua. Hadi kesho tunauliza: Yako wapi majina ya majambazi na mafisadi walioficha pesa yetu nje?

Kitu kingine kilichommaliza Kabwe ni ile hali ya kudai kuwa asingegombea ubunge kwa mara ya pili. Badala yake angwenda kufanya kazi anayopenda ya kufundisha chuoni.

Msimu wa uchaguzi ulipowadia, Kabwe aligombea huku akisahau aliyokuwa ameahidi. Kwa wapiga kura hili lilikuwa pigo kubwa. Nadhani hata CHADEMA waliliona hili na kulihofu. Wenye busara walihofu na kuhoji hili.

Yanini kupayuka wakati unaweza kujiondokea kimya kimya au kutangaza kutorejea siasa wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea? Kupenda sifa kwingine kwaweza kuwa kitanzi kwa mhusika.

Pigo jingine kwa Kabwe ni ile hali ya kushutumiwa kuwa anatumiwa na CCM na asikanushe na kutoa majibu mujarabu. Wapo wanaoona kama ni ukweli. Maana ungekuwa uongo Kabwe, bingwa wa kuongea, asingekaa kimya.

Ukiunganisha na uvumi kuwa Kabwe atarejea kwao CCM, unaona ukweli japo kwa wanaojua mizengwe ya CCM, akifanya kosa akajirejesha kule, watamtema kama ganda la mua.

Kwa waliosikia nukuu za Januari Makamba kuwa kiongozi wa nchi awe ni mtu mwenye kujua kutunza familia yake, walishajua kuwa Kabwe hawezi kukatiza pale ikizingatiwa kuwa neno mke au mtoto bado ni msamiati mgumu tu japo nasikia ana mtoto.

Alioa lini? Watamchunguza kuanzia dada zake hadi mama yake ili wamchafue. Huu ni ushahidi kuwa huko CCM nako hakubaliki. Wameishamtumia. Hawamuhitaji tena ili asiwachafue. Kama amewasaliti wenzake, atashindwa nini kuwasaliti waliomtumia, tena kwa kumlipa jambo ambalo hajakanusha?

Licha ya ushiriki wa Kabwe kwenye kuandaa waraka husika, hakuna kilichomuumbua kama kudai kuwa hakuwa na taarifa za mpango huu mzima.

Alichodai Kabwe ilikuwa sawa na kumficha msichana unayetaka kumuoa uchumba halafu bado ukasema una mpango wa kumuoa.

Ushahidi wa kimazingira ni kwamba Kabwe alijua na kuratibu kila kitu. Kuna wanaoona kama hapa kilichokuwa kikifanyika ni kutumiana yaani wawili kumtumia Kabwe naye kuwatumia.

Hata hivyo, tuseme CHADEMA imekuwa na subira kupita kiasi, hasa kwa Kabwe na siasa zake tatanishi. Nadhani kwa uamuzi waliochukua dhidi ya Mkumbo na Mwigamba na hatimaye Kabwe utakuwa somo kwa wengine kuwa kumbe CHADEMA inaweza kung’ata, tena kwa makali zaidi.

Tumalizie kwa kumpa Kabwe nasaha fupi ya Kilatini; Consilio, quod respuitur, nullum subest auxilium – asiyekubali kushauriwa hawezi kusaidiwa.

Hivyo kaka, Acta est fabula, plaudit – mchezo kwishnei kwa lugha ya watoto wa mjini. Huo ni ushauri huenda unaweza kukusaidia kama utakubali kushauriwa.
 
Huyu ndiye Samson Mwigamba wa zamani..... akimpa onyo/ushauri Zitto Kabwe



Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009

NAKUHURUMIA ZITTO KABWE


MHESHIMIWA Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, salaam.

Awali ya yote naomba kama nianze kwa kutangaza mgongano wa kimaslahi kama ilivyo kawaida kwa wabunge kufuatana na
Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la Mwaka 2007.

Mgongano wa kimaslahi ni kwamba ninakuandikia waraka huu nikitaka kujadili machache juu ya mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA, mambo ambayo yanakugusa kila wakati nikitaka kujaribu, kwa faida ya wasomaji, kuangalia kulikoni na wakati huohuo nikijua kwamba wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na ambaye tumekuwa pamoja tukikubaliana kwa mambo karibu yote, wakati wote.

Mheshimiwa unajua urafiki wetu ni wa muda mrefu na kwa kweli nilikupenda kabla wewe hujanifahamu; nikakuhesabu kama rafiki kabla hujanifahamu na kwa bahati nzuri sana uliponifahamu ukakubali kuwa rafiki yangu.

Nimekuunga mkono katika matukio, maamuzi na hata mitazamo yako mingi kwa muda mrefu. Nilikuwa upande wako katika kupiga vita ufisadi na hata uliposimamishwa ubunge wakati wa hoja ya Buzwagi nilikuwa upande wako.

Nilikuwa upande wako ulipotoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga utaratibu wa kuwachagua wabunge wa Afrika Mashariki na hata katika kile ulichokiita ‘bifu’ kati yako na Spika wa Bunge, lililotokana na hatua yako ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge na maneno uliyoyatoa nje ya ukumbi huo kuhusu uwezo wa spika kusimamia kanuni za Bunge.

Nilikuwa pia upande wako uliposimama kumtetea Spika kuhusu hoja iliyotolewa na mwandishi mmoja akipinga uwepo wa Kamati ya Bunge ya Kutunga Sheria katika kanuni mpya za Bunge.

Nilikuwa upande wako pale ulipounga mkono maelezo ya kitaalam ya TANESCO kununua mitambo ya Dowans na hili unalifahamu zaidi maana tulikuwa tukiwasiliana sana na huenda mimi na Absalom Kibanda ni miongoni mwa waandishi wachache sana
tuliodiriki kusema waziwazi kupitia kalamu zetu kwamba tunaunga mkono msimamo wako wa kununua mitambo ya Dowans.

Utakumbuka pia siku moja tulipishana mtazamo tulipokuwa tukichangia kwenye mtandao mmoja wa intaneti hoja ya utafiti
wa taasisi moja iliyoonyesha kwamba bado Kikwete na CCM ni maarufu kuliko vyama vya upinzani kwa mbali sana. Unakumbuka kwamba mimi nilitofautiana na wewe kwa hoja za kitaalam zinazohusu utafiti.

Lakini baada ya kutoa hoja zako na mimi nikatoa hoja zangu na wewe ukazijibu nilikubaliana na wewe na hatimaye nikawa upande wako.

Lakini katika siku za karibuni nimejikuta nikiwa katika mfululizo wa matukio, mitazamo na maamuzi ya mimi kutokubaliana na wewe.

Utakumbuka nilianza kutokubaliana na wewe kuhusu uamuzi wako wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa taifa wa CHADEMA.

Nilikutumia barua pepe ndefu sana nikipinga uamuzi huo na kukuomba kwamba ujitoe kwa hoja nyingi ambazo najua unazikumbuka vema. Kwa bahati mbaya hukujibu ile barua pepe, lakini sikukata tamaa, nikaambiwa nipitie kwa msaidizi wako David Kafulila.

Nikafanya hivyo na Kafulila akanihakikishia kwamba kila tunachoongea anakufikishia na kwamba unampa majibu ya kunipatia. Lakini mheshimiwa unakumbuka kwamba mwishoni kabisa majibu yako yalikuwa ni kwamba hoja zangu zote ulikuwa unazikubali lakini ulishazizingatia kabla hujaamua kujitosa kwenye kugombea uenyekiti na hivyo usingejitoa.

Nashukuru kwamba baadaye uliamua kujitoa japo ulikuwa umechelewa. Mheshimiwa Zitto, nilitofautiana na wewe pia kwa kauli zako ulizokuwa unazitumia kutaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kujiondoa.

Katika moja ya taarifa za habari ulinukuliwa ukisema unatofautiana na Mbowe kwa sababu wewe ni mjamaa wakati yeye ni bepari. Nikawaza na kukumbuka kwamba Agosti 13, 2006 wakati chama chenu kinazinduliwa upya ulikuwepo na ninaamini ulishiriki kikamilifu katika kufanya utafiti, kuchambua na hatimaye kuja na katiba mpya iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu siku hiyo na kupitishwa kuwa katiba mpya ya chama hicho.

Na kwamba maneno haya yanayosomeka kwenye utangulizi wa katiba hiyo mpya ya CHADEMA yakiwa yametamkwa kwa kunyanyua
mikono na wajumbe wa mkutano huo mkuu, basi yalikuwa ni yako pia:

“Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika Agosti 13, 2006, mjini Dar es Salaam, tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha siasa kitanachoitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya Nguvu na Mamlaka ya Umma na Dira na Dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea.

“Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitavyotungwa kwa mujibu wa Katiba ili kuimarisha kutetea, kudumisha, na kuendeleza Demokrasia ya kweli na hatimaye kuweza
kuleta maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jamii nzima ya taifa la Tanzania.”

Kama na wewe ni miongoni mwa wana CHADEMA waliotamka maneno hayo siku hiyo kwamba: “Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitakavyotungwa kwa mujibu wa Katiba hii” nilitegemea uwe umeisoma katiba yenyewe na kuona kwamba ibara ya 3 ya katiba hiyo, ibara ndogo ya 3.B. kifungu cha 3.1.1 kinasema “CHADEMA ni chama cha itikadi ya Mrengo wa kati (center party)”.

Hata kwa elimu ndogo tu maelezo haya yanatosha kuonyesha kwamba chama hiki kinaongozwa kwa itikadi iliyoandikwa ndani ya katiba ambayo ni Mrengo wa Kati na wala si itikadi binafsi ya Mbowe ya ubepari ama ya Zitto.

Kwa imani niliyokuwa nayo kwako na nikizingatia elimu kubwa uliyokuwa nayo, nafsi yangu ikanituma kufikiria kwamba labda ‘wamekunukuu vibaya’. Nilihudhuria mkutano wenu na waandishi wa habari uliokusudia kuzika tofauti zenu na Mbowe na kusonga mbele kama chama.

Pale ulipoulizwa swali na mwandishi mmoja kwamba utawezaje kufanya kazi na Mbowe wakati wewe ni mjamaa na yeye ni bepari; ukajibu kwa namna ambayo haikukata kiu yangu ndipo nikaamini kwamba kumbe hukunukuliwa vibaya bali ni kweli ulisema maneno hayo.

Nilipingana na wewe pia pale ulipoamua kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana CHADEMA
(BAVICHA). Unakumbuka kwamba nilialikwa katika uchaguzi huo miongoni mwa wageni wachache wanafunzi, wanahabari, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali walioalikwa kushuhudia uchaguzi ule.

Wakati wa uchaguzi wenyewe utakumbuka mimi na wewe tulikaa meza moja na tulitenganishwa na mtu mmoja tu (Mkurugenzi wa Uenezi Taifa wa CHADEMA, Erasto Tumbo). Nilitegemea mambo yasiyoendana na sera na kauli mbiu za chama chenu ambazo zinatangazwa hata katika jina la chama (DEMOKRASIA na MAENDELEO) ambayo yalifanyika pale ukumbini uliyaona.

Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule.

Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza.

Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje?

Na mwisho nilipingana na wewe pale ulipopinga kwenye vyombo vya habari kuvuliwa wadhifa kwa David Kafulila. Kwanza ulionekana umeweka ubaguzi kwa sababu katika maneno yote uliyonukuliwa ulisisitiza juu ya Kafulila peke yake na hukumgusia kabisa Danda Juju wakati wote walivuliwa kwa sababu zinazofanana.

Lakini kwa sababu Kafulila ni rafiki yako sana, umemwandaa kuwa mbunge na unamuunga mkono katika harakati zake, na ni mbunge mtarajiwa kwa kuwa anakubalika sana jimboni basi ukamtetea na kumsahau ‘mhanga’ mwenzake.

Hilo tu linafanya tutofautiane na zaidi sana tunatofautiana kwa kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu wako nje ya vikao, maamuzi aliyoyachukua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

Najua yote haya umeamua kuwa kimya hujayatolea kauli yako ikiwa ni pamoja na yale ya kumfadhili Kafulila kwenda Kigoma kuichafua vizuri CHADEMA. Lakini kama ni kweli, napingana na wewe na kama unaendelea kukaa kimya nitaamini kwamba ni kweli.

Sasa limeibuka la kusema kwamba unatembea na barua ya kujiuzulu nyadhifa zako zote ndani ya CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge. Bado pia sijapata kauli yako, narudia kusema kwa kuendelea kunyamaza unanifanya niamini kuwa ni kweli.

Na kama ni kweli, nakuhurumia sana Zitto Kabwe. Sasa naona kile nilichokuambia wakati nikikushauri ujitoe kugombea
uenyekiti kinatimia. Nilikuambia ujitoe haraka tena kimyakimya kwa kumweleza tu Katibu Mkuu aweke fomu yako pembeni lakini hukutaka kunisikia.

Lakini utakumbuka moja ya sentesi zangu ilikuonya kwamba uking’ang’ania kugombea iwe umeshinda uenyekiti ama umeshindwa utapata shida kubwa. Nilikueleza kwamba hutaaminika tena na Watanzania na kila kitu utakachofanya utaonekana kama ulikuwa ni mamluki ndani ya chama.

Ni kwa bahati kwamba umetokea kuwa na viongozi wenye busara sana kina Freeman Mbowe na kina Dk. Wilbrod Slaa wakisaidiwa na hekima na kamati ya wazee. Hawa wakaamua kukurejesha kwenye unaibu katibu mkuu.

Nilishuhudia siku ile wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyoshangilia uteuzi wako na wa Dk. Slaa na Hamad Yusuph kama wakuu wa Sekretarieti ya chama. Nilidhani sasa ungetulia na kufanya kazi ya kujenga chama chenu na kusonga mbele lakini haikuwa hivyo.

Baada ya kushauriana sana wakati ule ulipotaka kugombea uenyekiti niliamua kutafuta habari za kiuchunguzi ndani ya
CHADEMA. Nimeongea na viongozi mbalimbali na maofisa wa CHADEMA makao makuu, nimeongea sana na David Kafulila
na hata niliwahi kumsikiliza yako mzazi akiongea na watu ambao sikuwafahamu.

Nimegundua kitu kimoja tu: kwamba kama mambo haya huyafanyi kwa makusudi na kwa malengo maalumu, basi watu uliowaamini sana ndani ya CHADEMA hata kama walikuwa na nyadhifa ndogo, walikubali kutumiwa ili wakutumie wewe kuimaliza CHADEMA na wewe ukaingia mkenge.

Ukakubali kugombanishwa na viongozi wenzako wa ngazi za juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe ili malengo ya watu hao yatimie. Sasa nakuonea huruma.

Nakuonea huruma kwa sababu kama ni malengo ya hao watu kukutumia kukimaliza chama hawatafanikiwa na badala yake watakumaliza wewe bure na utakuja kushtuka ukiwa umekwisha kisiasa.

Kama ni malengo yako kwa utashi wako umeamua kutumika kukimaliza chama, nakuhurumia kwa sababu utajimaliza wewe na CHADEMA itaendelea kuimarika bila wewe wala Kafulila. Ukitaka kujua ninachokisema, tuulize sisi waandishi tunaopata
mawazo ya Watanzania moja kwa moja.

Kwa kuanzia muulize tu Edward Kinabo kwamba Jumatano iliyopita alipoandika makala ya “Simwelewi Zitto Kabwe” aliungwa mkono na wasomaji wangapi na walikuwa na mawazo gani juu yako. Hapo ndipo utakapoelewa kile ninachokisema.

Namalizia kwa ujumbe wa msomaji wangu mmoja tu kati ya wengi. Huyu aliniambia anaitwa Meshack na yuko Korogwe. Aliniambia, “Sisi tulishajua kwamba Zitto anaondoka CHADEMA na kwamba anachosubiri tu ni pensheni yake ya ubunge ambayo huwa inatolewa baada ya Bunge kuvunjwa.

Naomba Mwigamba kwa sababu unaweza kuongea na viongozi wakuu wa CHADEMA, waambie kwamba wasije wakafanya kosa la kumvua Zitto uongozi wala kumvua uanachama.

Sisi hatutaki apate kisingizio cha kuondoka CHADEMA. Waambie wamuache tu mpaka atakapoondoka mwenyewe ili Watanzania wazidi kumfahamu,” mwisho wa kunukuu.

Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi. Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako.

Katika yote nakutakia kila heri!
 
KITILA, Sikujua kuwa ulikuwa mjumbe mzigo wa cc ya chadema. Yaani na usomi huo haujui kwa nini ccm inashinda hata mahali ambapo haina wapenzi au hata wanachama? Kumbe hukuisaidia chadema kuangalia tatizo la kura za maruhani zilizoidhoofisha cuf mpaka wakaamua kujiunga na ccm? Leo kwa unafiki wako unasema cdm imeshindwa wakati ulitakiwa ujue kuwa tume ya uchaguzi imefunga ndoa isiyokuwa na taraka na ccm, vyombo vya ulinzi na usalama na wageni wanaoangamiza Taifa hili, na pia kuwa rejista ya kura inamilikiwa na nec na ccm?. Kama hujui haya yote hata hicho chama chenu ACT kitakuwa kama ATC !

Je chadema walijua haya kabla ya uchaguzi? kama ndio Kitila yuko sahihi

kama hawakujua basi ni mbumbumbu na afadhali washindwe hakuna wanachojua
 
ebu atueleze akili ndogn iliyokuwa inatawala akili kubwa ni ya nani.? Je too local uswahili wa viongozi wake ni upi ? Na elimu ya mangumashi ya viongozi wake ni iPi ? Ni ile ya fom 6 ?Au std 7 ? By waraka .Ungejisiaje ungekuwa ni wewe ?
 
Ningekuwa mshauri wa Kitila Mkumbo ningemwambia anyamaze tu maana kwa usomi wake kila anapozidi kauandika kuishambulia chadema anadhihirisha Usaliti wake pamoja na kundi lake kwa chadema. hoja ni mmoja tu kwamba wewe ulikua mjumbe wa kamati kuu kama yale uliyoyaandika kwenye waraka wako wa siri unayaamini kwanini hukuwahi kuyaweka wazi kwenye vikao ili yajadiliwe? Kitila acha unafiki wa kutumika. Watanzania tuna akili ya kutosha fanya kazi ya kujenga hicho chama chako mlichoanzisha tuone uwezo wako huo unaotaka tuamini kama umetoka mbinguni,kama hawa ndio walimu wetu wa vyuo hii nchi inaelekea kuzimu.
 
Hivi huyu Kitila kama angekuwa anakosoa kwa kasi hii hii kabla hajafukuzwa si angejenga heshima kama mtu mwenye misimamo? Zitto aliposimama sasa ndipo alipo siku zo.

Mkuu uko sawa kabisa kuhusu huyu jamaa, Anapoandika kwamba CHADEMA SI CHAMA MBADALA hatumwelewi. Kwanini hakusema toka zamani kwamba CDM si mbadala au ndo yale yale ya kujifanya na mwenzie kuwa ndo vinara wa CDM wao ndo wameishikilia, afie mbali kabisa hukooo si si e mu
 
NaAmini DK KITILA ANAPOSEMA KUWA VIONGOZI WA CDM WANANUNUA MASHANGINGI KAMA YA SERIKALI KWA PESA YA UMMA WANAYOPEWA ANAMJUMUISHA PIA ZZK KWA SABABU NA YEYE ANA MAGARI KAMA HAYO.
VILE VILE NAAMINI DK KITILA ANAJUA ZZK ANATOA WAPI PESA YA MATUMIZI MAKUBWA HIVYO BILA KUPOKEA POSHO YA KUKAA BUNGENI

Bro kimsing tukirudi kwe hoja,kitendo cha wabunge wa chdma kuendelea kubaliki yaleyale wanayo ya pinga(matumizi mabaya ya pesa),kwanza ni kutudharau ss wananch ambao kila sik wanatufanyia maigizo. Kiongozi bora lazima aeneshe mfano,tusikimbilie kuisapot chadema hata kwa mabaya!
 
Majibu ya Dr.Kitila ni majibu ya kisomi na ya ujenzi yanaitaji nguvu ya hoja kuyajibu.

Dr.Kitila, umetimiza wajibu wako watanzania wanakusoma.

Najua kabisa majibu ya pro-Chadema yatakuwa kebehi na kejeli dhidi yako kama ulivyosema.

Watu wakisifiasifia ccm na hasa kale kakitengo kalikofutwa kwa muda (redet) ndo mnapenda! wanaokosoa ccm mnaonaga sio wasomi! Shame on you!
 
KITILA, Sikujua kuwa ulikuwa mjumbe mzigo wa cc ya chadema. Yaani na usomi huo haujui kwa nini ccm inashinda hata mahali ambapo haina wapenzi au hata wanachama? Kumbe hukuisaidia chadema kuangalia tatizo la kura za maruhani zilizoidhoofisha cuf mpaka wakaamua kujiunga na ccm? Leo kwa unafiki wako unasema cdm imeshindwa wakati ulitakiwa ujue kuwa tume ya uchaguzi imefunga ndoa isiyokuwa na taraka na ccm, vyombo vya ulinzi na usalama na wageni wanaoangamiza Taifa hili, na pia kuwa rejista ya kura inamilikiwa na nec na ccm?. Kama hujui haya yote hata hicho chama chenu ACT kitakuwa kama ATC !
Mbona maeneo mengine CDM wanashinda,inamaanakuna NEC nyingine au vyombo vya usalama vingine?. Usiwe mwepesi wa kudanganywa na propanganda zisizo na tija!
 
Kitila unaandika ushuzi wa hasirs unapoteza hata maana ya usomi wako. Ni kweli hoja zako ni hoja za nguvu sio nguvu za hoja unalazimisha kile ambacho kinawavuta kwenda ktk uccm wako ukiokuwa. Tulio nje twaona umepotoka tu au tunaona bado ile bilion 3 inafanya kazi yake kwa nguvu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom