Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
hivi mtoa mada anaposema cha mtu mavi huoni anamaani kwamba hiyo chadema ni cha watu fulani.
tunaomba ufafanuzi tujue kama ni watu tengeru au?

Ubishi wako ni wa kitoto sasa hapo usicho elewa ni kitu gani? watu wengine bwana hovyo kabisa.
 
Kwa hiyo wakisema samaki mkunje angali mbichi wanamanisha kambale, au au wakisema zimwi likujualo alikuli likakwisha wanamanisha mazimwi? Nakadhalika. kajifunze lugha na ujue methali nahau na semi mbali mbali siyo unakimbilia kutafsiri kila neno kwa maana ulijuavyo
unaposema cha mtu mavi unamaanisha nini?
kweli mwenye asili haachi asili.sasa hio chadema ambayo hutaki kitila mkumbo aikosoe ndio mavi ok,tunaomba ututajie mwenye mavi.

kauli hii haina tofauti na kusema chadema ina wenyewe.tunaomba ufafanuzi zaidi juu ya hayo MAVI.
 
Kitila ni mwana saikolojia. Kwenye saikolojia ukiona mwanaume/mwanamke amefukuzwa kwa mumewe/mkewe na bado huyo aliyeachika anamsemasema kwa ubaya tena hadharani huyo mwenza wake, ni wazi kuwa ALIYE ACHWA ANA MAPENZI MAKALI BADO KWA ALIYEMWACHA. Sasa kelele za Kitila zinavyoendelea kupuuzwa na viongozi wa Chadema ambao wote wana akili, naona dalili ya Kitila kujinyonga....
 
hivi unafikiri hizi kejeli ndio zitazima hoja iliyopo mezani?
Hata hivyo hakuna asiyejua mnapozidiwa mnaleta viroja.

Tunaomba mmwambie ansbert ngurumo au kiongozi yeyote wa chadema kuwa aje athubitishe kuwa yaliyo semwa ni uongo.

Dr.Kitila anyamaze maana hana tena uhalali wa kuijadili cdm.

kelele zake zinadhihirisha kuwa alikuwa anafanya usaliti kwa makusudi. Kinachomuumiza moyo ni kushindwa kukamilisha usaliti wake.

kelele zake ni sawa na kutuonesha manyoya kwamba ameshaliwa.

Kama anajiamini kuwa ni mkweli na ana akili kuliko waliomfukuza na kwamba watanzania wanamkubali aanzishe chama chake ataungwa mkono na wanaomwamini.

Akiishakijenga chama chake amkaribishe D.Kafulila na Zitto majibu tutayapata.

Dr.Mkumbo atulie azae maana kuendelea kuisakama cdm ni kuzidi kujidhalilisha mbele ya watanzania walioweka matumaini kwa cdm kama mkombozi wao.

Dr.Kitila ameshapoteza mvuto kwa wanaohitaji mabadiliko.Haaminiki kwa lolote maana hata elimu yake haionekani tena. Msaliti ni msaliti tu hata kama ataimba nyimbo zenye ujumbe mzuri watu hawatazisikiliza.

Dr Mkumbo nenda nenda dr nenda hatukutakiiiiiiiii

Kamshauri Prof.Kapuya
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba sikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila

Dr. KITILA uko sahihi kabisa.
 
hawo viongozi anaomaanisha kitila ni pamoja na zito kupata viti vichache vya udiwani ktk uchaguzi wa2010 ukilinganisha na umaarufu alionao zito
kwani kabla ya zito walikuwa na viti vingapi?
 
Dr Kitila Mkumbo, ndoa ikivunjika ama kwa kufukuzana, talaka, au kufa kifo cha mende huwa kila mwanandoa anajitetea kivyake, ila wenye busara hukaa kimya kwani kipindi cha msukosuko ukisema neno linakuwa na jazba.

Kwa kweli sasa una uchungu, na unatamani kuona CDM inakufa sasa hivi. Kamanda hilo halitaka litokee leo au kesho, wengi wataingia na kutoka ila chama cha siasa kitaendelea kuwepo.

Naomba nikuulize mgomvi wako mkubwa na unaposema CDM unamaanisha nini? Je mwisho wako ni pale Kinondoni? Je unasahau hiki ni chama chenye wanachama wengi Tanzania na duniani.

Kama unavyoamini wewe upo sawa na wengine tunaamini tupo sawa kabisa kukutimua. Tunasubiri muanzishe huo mbadala is easy to say than do. Vitabu vipo vingi sana vyenye theory zilizofeli, ndio maana wengi waliofanikiwa duniani ni regular Jo kwani wana simple mind. You guys complicate everything.

Mtaandika sana, mtahama sana vyama, mtatumika sana, mtaishia kukosa heshima na hadhi kwani binadamu kaumbwa kuchukia ndumila kuwili.

Chadema imetoka mbali imefanikiwa sana na inakazi kubwa mbele tutafika salama, na tutazamisha yeyote mwenye anataka kutoboa mtumbwi au tutamtupa majini; haizami merikebu hapa.

Andikeni najua baada ya uchaguzi mkuu 2015 kalamu zenu zitakwenda likizo, kibaba cha mchele kitapokauka.

Dr Kitila, Zito kabwe ni msaliti wengi tunaushahidi sidhani kama unataka mabomba yaanze kumwaga maji, ninatamani sana mwende chama chochote au muanzishe chenu, kwani usaliti na majungu ya kiuongozi ni tabia. Tumieni elimu zenu kimaendeleo. Bill Gates aliweza kufanya kazi na maprofessa nguli yeye akiwa drop out, Dell aliweza kufanya kazi na wasomi nguli yeye akiwa drop out wasomi wale walielewa hawa jamaa wana mambo muhimu sana kwao na mafanikio yao, walimsikiliza na walielewana kwa miaka zaidi ya 30, ukishindwa kuelewa brain za wengine na kuwa na uwezo wa kushinda changamoto na kila siku kutaka mapinduzi haramu huwezi kufanikiwa.

Tumieni elimu zenu kufanikiwa katika maisha kiuongozi nk, kitendo cha ninyi kushindwa kutafiti risks, na faida zake pamoja na matokea yake mtalia sana.

Mimi nawaona mahayani, kwani huwezi kutuambia leo kunahitajika mbdala wakati jana ulikuwa unalia unaomba msamaha ili ubaki ndani ya chama kwanini usingejitoa na kudai mbadala wakati huna matatizo ya uhaini?

Nime lazimika ku quote hii comment kwa vile ime nikosha sana mkuu Mkwawa kwa heshima zote chukua "LIKE"
 
Last edited by a moderator:
Mimi nilikuwa namkubali sana Dr Kitila kama msomi anayejielewa, lakini kwa ushenzi alioufanya hastahili hata kuitwa Dr, anaidhalilisha elimu, halafu cha ajabu, ameharibu na bado anasimama mbele ya umma, eti alikuwa ana mpango mzuri, lile jamaa linatia aibu kweli, kenzie kazitto kameanza kutengeza cd, kanajiita kazarendo, kuutafuta umaarufu kazi, ila kuupoteza dakika moja.

Mie mpaka sasa namkubali ila lazima ajue USALITI ​sio jambo zuri!!
 
Kitila ni mwana saikolojia. Kwenye saikolojia ukiona mwanaume/mwanamke amefukuzwa kwa mumewe/mkewe na bado huyo aliyeachika anamsemasema kwa ubaya tena hadharani huyo mwenza wake, ni wazi kuwa ALIYE ACHWA ANA MAPENZI MAKALI BADO KWA ALIYEMWACHA. Sasa kelele za Kitila zinavyoendelea kupuuzwa na viongozi wa Chadema ambao wote wana akili, naona dalili ya Kitila kujinyonga....

Kwi! Kwi! Kwi! Kwiiiiii !!!!!
 
Dr Kitila Mkumbo, ndoa ikivunjika ama kwa kufukuzana, talaka, au kufa kifo cha mende huwa kila mwanandoa anajitetea kivyake, ila wenye busara hukaa kimya kwani kipindi cha msukosuko ukisema neno linakuwa na jazba.

Kwa kweli sasa una uchungu, na unatamani kuona CDM inakufa sasa hivi. Kamanda hilo halitaka litokee leo au kesho, wengi wataingia na kutoka ila chama cha siasa kitaendelea kuwepo.

Naomba nikuulize mgomvi wako mkubwa na unaposema CDM unamaanisha nini? Je mwisho wako ni pale Kinondoni? Je unasahau hiki ni chama chenye wanachama wengi Tanzania na duniani.

Kama unavyoamini wewe upo sawa na wengine tunaamini tupo sawa kabisa kukutimua. Tunasubiri muanzishe huo mbadala is easy to say than do. Vitabu vipo vingi sana vyenye theory zilizofeli, ndio maana wengi waliofanikiwa duniani ni regular Jo kwani wana simple mind. You guys complicate everything.

Mtaandika sana, mtahama sana vyama, mtatumika sana, mtaishia kukosa heshima na hadhi kwani binadamu kaumbwa kuchukia ndumila kuwili.

Chadema imetoka mbali imefanikiwa sana na inakazi kubwa mbele tutafika salama, na tutazamisha yeyote mwenye anataka kutoboa mtumbwi au tutamtupa majini; haizami merikebu hapa.

Andikeni najua baada ya uchaguzi mkuu 2015 kalamu zenu zitakwenda likizo, kibaba cha mchele kitapokauka.

Dr Kitila, Zito kabwe ni msaliti wengi tunaushahidi sidhani kama unataka mabomba yaanze kumwaga maji, ninatamani sana mwende chama chochote au muanzishe chenu, kwani usaliti na majungu ya kiuongozi ni tabia. Tumieni elimu zenu kimaendeleo. Bill Gates aliweza kufanya kazi na maprofessa nguli yeye akiwa drop out, Dell aliweza kufanya kazi na wasomi nguli yeye akiwa drop out wasomi wale walielewa hawa jamaa wana mambo muhimu sana kwao na mafanikio yao, walimsikiliza na walielewana kwa miaka zaidi ya 30, ukishindwa kuelewa brain za wengine na kuwa na uwezo wa kushinda changamoto na kila siku kutaka mapinduzi haramu huwezi kufanikiwa.

Tumieni elimu zenu kufanikiwa katika maisha kiuongozi nk, kitendo cha ninyi kushindwa kutafiti risks, na faida zake pamoja na matokea yake mtalia sana.

Mimi nawaona mahayani, kwani huwezi kutuambia leo kunahitajika mbdala wakati jana ulikuwa unalia unaomba msamaha ili ubaki ndani ya chama kwanini usingejitoa na kudai mbadala wakati huna matatizo ya uhaini?

Nime lazimika ku quote hii comment kwa vile ime nikosha sana mkuu Mkwawa kwa heshima zote chukua "LIKE"
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu Kitila Mkumbo ni Dr wa binaadamu, mifugo au falsafa? Hoja kuu ya ngurumo ni kwamba Hakuna records zinazoonyesha aliwahi kuwakosoa viongozi wa chama wala chama katika vikao stahiki ndani ya chama, yeye anakuja na hoja ya kuandika kwenye magazeti.

Ngurumo anasema kwa nini Kitila hakutumia fursa ya kutakiwa kujieleza kwenye kamati kuu kuelezea udhaifu na Ufisadi waliouandika kwenye waraka wao wa kishenzi kama kweli alikuwa na nia njema na chama chake, Alishindwa, ikiwa na maana kwamba ni muoga , muongo, mzandiki,pandikizi,mnafiki na msaliti.

swala la kuandika kwenye magazeti hata sisi tunaandika hapa JF.

DR Gani huyu Jamani, Hawezi kuelewa hata analalamikiwa kivipi, nadhani Ngurumo alikosea kutambua usomi wake.
kaka! inajulikana na kila mtu kwamba vikao vya chadema huedeshwa kibabe na havizingatii hoja wala weledi bali vinaangalia nani ni nani!!
na mpaka mpasuko ndani ya chadema unatokea ni idadi kubwa ya wajumbe wa vikao walikuwa hawahudhurii kwa sababu ya ukanjanja wa uendeshaji vikao.
kama alivyokwisha eleza Kitila, alijaribu(tena kwa ukali) kueleza mapungufu ya chama katika vikao lakini hakueleweka. unataka angefanya nini zaidi????
amini nakwambia!! CCM ni chama kinachoelekea kufa lakini hakijafa bado. na kinaweza kurudi na kuwa kipenzi cha wananchi kama wakitokeo viongozi wa kukiokoa.
lakini chadema kinakufa kabla hata hakijatimiza umri wa kubalehe. mlio na kili mufilisi hamtakubaliana na sisi kupitia humu, lakini deep in your hearts you the truth.Kitila anasimamia anachokiamini akiwa kama mtu huru asiyefungwa na itikadi zozote.lakini yeye ni muumini wa kile ninachokiamini kuwa""" tunahitaji MTU mwenye dhamira ya kweli ya kulikomboa hili taifa"" na huyo mtu asiwe wa kufikirika bali awe katoka miongoni mwetu na matendo yake yatushawishi kwamba YULE TUNAYEMTAKA NDIYE HUYU!!
kwake yeye kama nilivyo mimi, kamuona ZZK...Kosa lake li wapi!!
huu ujinga wa kuitana WASALITI,MAPANDIKIZI,---------- na misamiati mingine ya kijinga ni aina nyingine ya ukaburu ndani ya chadema. tulipambana na ukaburu wa SOUTH AFRICA, hatutashindwa kuwaangamiza makaburu wa ndani. nadhani mmeshaisoma kwenye uchaguzi wa madiwani uliopita hivi punde. nawahakikishia baada ya uchaguzi 2015 tutakifuta kabisa hiki chama. na mkumbuke baada ya 2015, raisi hatakuwa kikwete huyu anayewabeba na kuwavumilia
 
unaposema cha mtu mavi unamaanisha nini?
kweli mwenye asili haachi asili.sasa hio chadema ambayo hutaki kitila mkumbo aikosoe ndio mavi ok,tunaomba ututajie mwenye mavi.

kauli hii haina tofauti na kusema chadema ina wenyewe.tunaomba ufafanuzi zaidi juu ya hayo MAVI.

wenyewe ni sisi wanachama watiifu kwa chama tusio wasaliti!!!!
 
Toa hoja kwanza. Mbona Freeman alivyochukua hela kwa Mkono na Rostam ili wakihujumu chama ktk uchaguzi haukusema? au hiyo ilikuwa ni sahihi? Achenu kulea ugonjwa hapa.

Mkono kasema hajawahi kutoa hela kwa Mbowe, Rostam alisema hizi ni siasa za majitaka. Zito aliyeliibua hata kwenye facebook yake alifuta siku hiyo hiyo, wewe umelishikilia kwa nanufaa gani?
 
chadema pro chagaz!
badilikeni nyie wajinga.stop barking and start doing politics.
 
Dr. Mkumbo ndiye alitakiwa awe tochi ya wenzake kuwashauri vizuri hata kama walikuwa na mkakati wao walitakiwa wawe watulivu kama wanachama wa CCM walioitwa kuhojiwa na kamati ya maadili unawaona wametunza siri ya kilichooongelewa sasa wao walitaka kushindana na viongozi wa chama kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa maelezo yako huyu jamaa yuko kwenye situation tunayoiita "Trauma" kama Tanzania na wasomi wetu wangekuwa makini wangemsaidia mwenzao kwa wataalamu wa Counselling. Kibinadamu suala lililompata hawezi kuepuka hali hii, Ajitahidi sana kuandika na kusema sema ndiyo inaweza kumsaidia vinginevyo anaweza ku develop matatizo mengine kama ya Pressure na kisukari.

Haiwezekani kabisa kwa msomi wa kiwango chake kuandika mkakati wa siri afu udanganye UMMA kwamba ulikuwa ni kwa maslahi ya CHADEMA. Namsikitikia sana maana hii ni ya Karne kama siyo ya Mwaka. Kama kweli walilipwa basi wao watanue tu na hiyo mihela ya bure lakini mission yao imekwama na kufa kisayansi. Pole Dr. Pole sana bahatisha tena kwingine maana kwa hawa jamaa mkakati umebumbuluka.
 
Maneno sawa kabisa kutoka kwa dr Mkumbo.
Ngurumo anamtumikia kafiri ili apate mradi wake wakati Mkumbo yuko huru, hafungwi na minyororo ya itikadi kwa sasa!.
Hivi ngrumo haoni jinsi Wabunge wa CHADEMA kama kina Lema wanavyotumia nguvu kuhalalisha posho za kijinga.
Hivi Ngurumo haoni jinsi wabunge wa CHADEMA wanavyobehave kama wabunge wa CCM pindi linapokuja suala la mijihela?

mbona kuna ushahid wa waz sana kuwa zito alikataa posho bungen lakn akapokea kwenye kamati milion 100 pamoja na akina msekwa. hilo mbona hilo akina kitilya hawalisemei hili. zito kachukua posho mwanza kwenye kikao watu wameweka mpaka risiti wewe bado unataka kutuaminisha zito ni mwaminifu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom