Bwana Issa Michuzi alitoa maelezo marefu kuwa yeye hafungamani na upande wowote ingawa asilimia kubwa tunamjua ni kibaraka wa CCM ,informer fulani wa usalama .
Sasa hivi iko dhahiri kuwa anapigia debe CCM Kupitia blog yake ,Kuna CD ya JK 2010 anatangaza kwenye blog yake anauza na pia kama unataka kuwekewa milio ya simu ya JK ati usasiliane naye.
Kama mtu yeyote yule ana uhuru wa kuwa na chama chochote ni haki yake ila kwa nii aligoma at the first place na kuandika waraka mrefu kukanusha na kung'aka.
Ambao mlikuwa mnashangaa kwa nini taarifa za Chadema na mikutano yao inachelewa kuwekwa au haiwekwi kabisa hope jibu ndio hilo,huyo bwana ni kada wa CCM A.K.A mafisadi .Kwa hiyo ana sababu zote za kuwa baised ,habari za CCM hata ki halfa kidogo ,kura za maoni faster anaweka,ukiuliza chadema au vyama vingine unambiwa hii blog yeyote anaruhusiwa ku post alaaa ndio iko hivyo!!
ukitaka mambo yako yakunyokee jiunge na ccm - mzee rukhsa
"mnasahau yaliyomkuta Mrema".
Sitaki kumtetea Michuzi wala CCM. Kama sikosei yeye alisema hao vyama vingine mfano CHADEMA na wengineo hawana njia ya kufanya publicity ya vyama vyao na shughuli zao. Wao wanahisi kila mtu atawafuata. Asilimia karibu 98 za habari za CCM kwa Michuzi zinatumwa kwake, na hao wa CHADEMA mpaka aende mwenyewe (mfano siku Mbowe kamtangaza Dr Slaa kuwania Urais) yaani hata video aliweka.
Halafu wewe Mutu inaonesha umetumwa ama una chuki binafsi na Michuzi ambaye wala halipwi na wewe wala nini. Wewe umemkazania kuwa ni kada wa CCM kwani tatizo liko wapi? Hivi kuwa mjanja ama mtu sawa lazima mtu uwe CHADEMA.
Mnamfagilia Dr Slaam mnamkumbuka Mrema na NCCR yake alivyokuwa anasomba watu na siku ya siku ikawaje? Mnamkumbuka Nyerere aliwaambia watu Jangwani pale kama mtu anapenda kubebwa kama maiti mwacheni sio kosa, Dr Slaa kwa lipi hasa?? Hayo madesa ya EPA na RICHMOD ambayo tumeshachoka kusikia (hamna mengine) mbona yeye hatuzungumzii alivyotemwa na kanisa? Mnataka tumwage mtama hapa??
Nyie CHADEMA wachache wenye njaa msio ne kuwa CCM ni dhambi. Dhambi iko katika kuongozwa na NGO ya ukoo inayoitwa chama cha siasa. Upumavu tu umewajaa. Mumkome Michuzi wa watu.
Wewe kweli ni *****, ulikuwa na ulazima gani kufungua thread nyingine ilhali hii ipo?
Yuko kwenye msafara wa Kikwete Press 2010
Najua hili suala la MICHUZI kutoku-post habari za vyama vya upinzani limejadiliwa sana hapa Jamii Forums.Najua wengi wengi wetu hapa hatumuamini MICHUZI hasa inapofika katika kutoa habari za siasa bila upendeleo.
Pendekezo langu hapa ni moja,kwa kuwa MICHUZI ni moja ya blog ambazo zinatambulika na sehemu kubwa ya Watanzania walio nyumbani na ughaibuni na kwa kuwa kimekuwa moja ya chombo muhimu cha kupashana habari napenda tutafute namna ya kuwasiliana na MICHUZI ili aweke tamko kwenye blog yake juu ya msimamo wake kuhusu kuweka habari za siasa bila upendeleo hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Najua BLOG ni mali yake binafsi lakini blog si kitu kama yeye mmiliki hajaribu kukidhi haja za wasomaji wa blog yake.
Ndiyo maana nimesema yuko kwenye msafara wa JK ( double entendre)Hata akiwa kwenye msafara wa Kikwete. Mbona huwa akisafiri nje ya nchi bado blog inakuwa updated na habari za nyumbani?
Ana vijana anaofanya nao kazi.
Anaudhi sana Michuzi. Halafu kama mfanyakazi wa serikali anavaa na kupiga picha na vitambulishi vya CCM -picha aliyoweka akisema ni birthday yake, yuko Kigoma, amevaa cap ya CCM.
Ajitokeze tu wazi na kusema kuwa yeye ni kada na mwanachama wa CCM, kwani dhambi?
Najua hili suala la MICHUZI kutoku-post habari za vyama vya upinzani limejadiliwa sana hapa Jamii Forums.Najua wengi wengi wetu hapa hatumuamini MICHUZI hasa inapofika katika kutoa habari za siasa bila upendeleo.
Pendekezo langu hapa ni moja,kwa kuwa MICHUZI ni moja ya blog ambazo zinatambulika na sehemu kubwa ya Watanzania walio nyumbani na ughaibuni na kwa kuwa kimekuwa moja ya chombo muhimu cha kupashana habari napenda tutafute namna ya kuwasiliana na MICHUZI ili aweke tamko kwenye blog yake juu ya msimamo wake kuhusu kuweka habari za siasa bila upendeleo hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Najua BLOG ni mali yake binafsi lakini blog si kitu kama yeye mmiliki hajaribu kukidhi haja za wasomaji wa blog yake.
Tusikimbilie kulalama lalama tu kabla hata hatuja fanya uchunguzi wa kuotosha kuna picha za kumwaga hapa
Michuzi ni chombo binafsi na tafanya kazi zake kulingana na kile anachotaka lakini pia amekuwa msaada mkubwa sana katika kuleta mapinduzi ya habari hasa kwa njia ya mtandao, post anything to michuzi blog and you will see it in one or two days.
So far Kampeni za Chadema zimeanza leo tusingetegemea kuona habari ya CHADEMA before
Mnakuwa kama CCM AHMADA bwana!!!!!