Dr Nkwasi: CCM hawana jipya, wanatafuta kiki kwa kutumia umbumbumbu wa wananchi

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,838
18,250
Siku hizi wanasiasa na chawa wa CCM wakipanda majukwaani wanatumia muda mwingi sana kumsifia Rais Samia hata kwa mambo yasiyokuwepo hadi wanatia kichefuchefu. Utasikia "Rais katoa pesa kujenga bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, kajenga SGR na mirai mingi sana na anawalipa wafanyakazi mishahara". Utajiuliza: hivi mshahara wa Rais ni mkubwa kiasi gani hadi autumie kufanya haya yote anayosifiwa kwayo? Nisimalize uhondo wote, hebu msome Dr Nkwasi (kada wa CCM asiyekuwa na chembe ya unafiki) kwenye andiko lake hapa chini:
. CcM inapofyatua kiki kutufyatua kitikiki

MAONI YANGU
Rais na serikali yake wanatumia kodi za wananchi kutanua na kiasi kidogo kinachobaki ndicho kinachoenda kujenga hiyo miradi uchwara ambayo chawa wanaitumia kumsifia kila siku utadhani fedha anazotumia zinatoka mfukoni mwake.

Sasa kwanini michawa ituumize masikio kila siku kumsifia mtu ambaye hatumii fedha zake kujenga miradi? Na isitoshe hicho ni kiasi kidogo sana cha mabaki anachotumia kujenga hiyo miradi. Kiasi kikubwa cha fedha kinafisadiwa na mafisadi wa CCM na machawa wa mama waliotapakaa kila kona ya nchi hii.

Kujenga barabara, SGR, mwendokasi, nk ni wajibu serikali kwani wananchi wanalipa kodi ili zitumie kuwaletea maendeleo na si vinginevyo. Pamoja na kuwa kiasi kikubwa cha kodi yao kinafisadiwa, wanaopaswa kupewa heko na pongezi ni walipakodi (wananchi) na sio Rais wala mwanasiasa yeyote anayesubiri wananchi walipe kodi halafu atumie kodi hiyo kutafuta kiki kwa wananchi haohao wanaolipa kodi. Na kibaya zaidi anawahadaa kwamba yeye ndiye amewajengea barabara, SGR, nk wakati hata mshahara wake haukatwi kodi. Wanasiasa na chawa wa nchi hii wanachekesha sana.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom