Kwa matamshi haya kuhusiana na uchaguzi mdogo huko Zanzibar, Makamu wa Raisi Zanzibar kutoka ACT-Wazalenido kujiuzulu wakati wowote?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Haya kumekucha huko Zanzibar

Screenshot_20210719-222902_Twitter.jpg
 
Kitu ambacho sipendi ni muungano kuvunjika. Utawasikia baadhi wanaomba msaada na kulalamika kwa nchi za Ulaya ambazo nazo zimeungana. Ujerumani, Uingereza, Marekani bila kuungana zingekuwa na uwezo mdogo kuliko sasa
 
Si kweli. Uwezo mkubwa wa nchi hizo unatokana na kuwa na utawala bora na katiba/makubaliano imara yaliyojadiliwa na kuhitimishwa kikamilifu. Miungano yao imesimama kwenye nguzo imara za maelewano yaliyoainishwa ndani ya katiba na makubaliano husika.

Kwenye utata kama ilivyotokea katika suala la BREXIT na athari zake kwa Northern Ireland na Scotland (UK) wanaendelea kujadiliana kwa uwazi na kuchukua hatua muafaka ili kuhakikisha utangamano wa kitaifa na kiuchumi. Hakuna ubabe wala bla bla za kisiasa.
 
Kitu ambacho sipendi ni muungano kuvunjika. Utawasikia baadhi wanaomba msaada na kulalamika kwa nchi za Ulaya ambazo nazo zimeungana. Ujerumani, Uingereza, Marekani bila kuungana zingekuwa na uwezo mdogo kuliko sasa
Muungano wa Tanzania hauna tija kwa pande zote 2.
 
Kitu ambacho sipendi ni muungano kuvunjika. Utawasikia baadhi wanaomba msaada na kulalamika kwa nchi za Ulaya ambazo nazo zimeungana. Ujerumani, Uingereza, Marekani bila kuungana zingekuwa na uwezo mdogo kuliko sasa
Ulaya kulikuwa kuna nchi inaitwa Czechoslovakia. Sehemu moja ilipoona kuwa hairidhiki na hali ilivyo ikafanywa referendum kuhusu ushirika huo. Sharti likikuwa nchi itabaki ilivyo kama tu pande zote zitaridhia. Pande moja ikakataa, wakaheshimu maamuzi, wakapeana talaka. Matokeo ni nchi ya Czech na Slovakia. Mpaka sasa wanaishi kwa amani.

Huko huko kulikuwa na Yugoslavia. Slovenia na Croatia wakalalamika kuwa Serbia inawanyima haki zao na inajifanya yenyewe ndio Yugoslavia. Serbia wakakataa kuwasikiliza. Slovenia na Croatia zikajitangaza kuwa ni nchi huru. Serbia wakashambulia Croatia kupinga uamuzi huo. Matokeo ni vita ambamo raia wengi walipoteza maisha na unyama mkubwa ulifanyika. Hatimaye Yugoslavia ikasambaratika na sasa kuna Slovenia, Croatia, Serbia, Bosnia na Herzegovina, Macedonia ambazo kila moja ni nchi huru.

Uingereza mpaka leo kuna wa Scot wanaotaka waondokane na uUK . Spain hivyo hivyo.

Hauwezi kulazimisha umoja. Mmoja akichoka ni heri kutengana kwa amani kuliko kulazimishana.

Amandla...
 
Kwa hiyo wanataka wapewe ushindi wa huruma licha ya kushindwa?

ACT hovyo sana hawa watu
 
Back
Top Bottom