Kwa Mara ya Kwanza nimeona Mafanikio ya Serikali kwenye suala la Machinga, Hongera Serikali ya Awamu ya Sita

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini


Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi


Naomba niishie hapa Kwa leo
 
Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
 
Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
Historia ipi hawajifunzi?

Kwani machinga wanapangwa kutokana na pesa?
 
Swala la machinga nampongeza Rais kwa kutoa maamuzi magumu machinga walishakuwa kero pia vibanda na uchafu ilikuwa aibu kwa majiji makubwa ilifanya tuonekane nchi ka ya vichaa, pia nimpongeze Makele jiji limeanza kuwa safi kuanzia Mwenge, ustawi na kwingine aisee vile vibanda plus mbao ulikuwa uchafu uliokubuhu Hadi nawaza kwanini machinga hawana aibu na hawajali usafi?
 
Huu kweli ulikuwa mfupa mgumu kiutendaji na kisiasa.
Nampongeza SSH na Bro Amos kwa kukifanya kieleweke bila furugu.
Nilikuwa napata shida sana nilivyokuwa naiona Dar kila siku inazidi kuwa chafu na ya hovyo.

Nilichoka mwaka jana nilipita Mlimani City nikakuta vibanda vya watu wanakaanga na kupika vyakula nje ya Mlimani City. Niliumia sana
 
Kama ilivyo kuwa vigumu kwa kiongozi kusema tusiendelee na mradi wa Bwawa la Nyerere au SGR ndo ilivyo vigumu kwa maamuzi ya machinga kufanyiwa reverse! Nimegundua hili jambo lilikuwa linawakera watanzania wengi sana Ila walikuwa hawana tu sehemu ya kuongelea.

Nimepita Posta watu wanasifia Kweli kwa sasa mji ulivyo msafi
Muda sio mrefu atakuja kiongozi atasema machinga warudi kwenye maeneo yao Kama zamani ni suala la muda tu
 
Swala la machinga nampongeza Rais kwa kutoa maamuzi magumu machinga walishakuwa kero pia vibanda na uchafu ilikuwa aibu kwa majiji makubwa ilifanya tuonekane nchi ka ya vichaa, pia nimpongeze Makele jiji limeanza kuwa safi kuanzia Mwenge, ustawi na kwingine aisee vile vibanda plus mbao ulikuwa uchafu uliokubuhu Hadi nawaza kwanini machinga hawana aibu na hawajali usafi?
Ilikuwa aibu! Tulikuwa tunaonekana wote ni nchi ya wajinga tusio wasafi na tusiofuata taratibu!

Kweli kwa hili naipongeza awamu ya sita! Wasirudi nyuma tu
 
Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
Machinga ni watumwa wa matajiri. Kwanza asilimia ya wamachinga wanaganga njaa ni wachache sana.

Wengi wana mitaji mikubwa sana ila wanajifanya machinga.
 
Kweli kabisa! Hili nimeliona!

Mtu anajenga kakibanda kabisa na anakuwa na bidhaa za karibu Mil 4-5 alafu anajiita machinga ili tu asilipe kodi
Nenda soko la Karume ( Mchikichini ) kila mmoja anajifanya machinga ila watu wana mitaji mpaka ya 200M hapo.

Na ndio maana hata kipindi kile soko limeungua walirudi kwa kasi kama hakikutokea kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom