Kwa Mara ya Kwanza nimeona Mafanikio ya Serikali kwenye suala la Machinga, Hongera Serikali ya Awamu ya Sita

Kumbe unaongelea nadharia na sio uhalisia?

Kwa akili yako mtu kuwa kisutu unadhani anauza kisutu tu? Kwani hawezi kupikia chakula kisutu na kukipack kwenda kuwauzia wateja wake sehemu nyingine?

Nimekwenda Ofisi nyingi hapa Tanzania nimeona mama lishe wanawauzia watumishi chakula ambacho kinapikwa mbali na ofisi zao na usafi upo maintained.

Shule niliyokwenda na exposure niliyonayo inaniwezesha kuwa na upeo mkubwa wa kufikiri kuliko kilaza wewe!
Shule yako ni upuuzi mtupu. Na exposure unayodai unayo ni upuuzi mtupu. Usafi maintained!? That's a bullshit, kama hata chombo cha kuwekea takataka tu hapo Posta hakuna hata kimoja wala public toilet mpaka mtu aende kwenye migahawa au bar. Kumbe umeona mamalishe!? Mimi nilidhani umewahi kuongea nao kwa kina, hiyo exposure yako uchwara kawaambie akina makala.
 
Usimlaumu Lord denning kwa kukosa hizo dust bins na toilets mjini. Labda ulaumu culture na traditions za Watanzania.

Niko DSM kwa zaidi ya miaka 40, public toilets zilikuwapo na garbage bins zilikuwapo ila Watanzania wenyewe walizi abuse. Toilets zilibakia ni maeneo ya machafu ambayo hayaingiliki. Hata kama Municipal Authority lakini Watanzania walikuwa siyo wastaarabu, wanakunya ovyo kuanzia mlangoni hadi kwenye choo. Unakosa pa kukanyaga.

Waache hivi hivi waende vyoo vya kulipia au mahotelini
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
unaleta tatizo alafu unalitatua unasema ?
 
Namwambia kuhusu hiyo exposure aliyonayo!? Huko wanakoiga hayo hakuna hayo!?
 
Ila Tanzania sijui ina tatizo gani, naposikia hadi leo wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati, wazazi hawana uwezo wa kumudu kuwanunulia binti zao taulo za kike,vijijini huko watu wanatumia maji yasio salama hadi leo,gharama za matibabu imekuwa mzigo mkubwa kwa wananchi n.k
Nabaki najiuliza hivi haya matatizo sugu yataisha lini ili tusifie na sisi?
 
Kwa hiyo unataka kutuambia nini sisi watanzania kuhusu awamu ya Tano ?
 
Amani iwe nanyi wanabodi!

Wakati Mama Samia anatangaza mkakati wake wa kuwapanga upya machinga kwenye maeneo mbalimbali, nilibarikiwa kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutoa ushauri wangu humu!

Ushauri huu niliutoa kwenye Thread hii hapa chini

Wakati naandika hii thread nilitoa haya Mawazo nikiamini kuwa yakifanyiwa kazi yataleta matokeo!

Baadae Waziri Mkuu wa JMT Ndug Kassim Majaliwa alifanya kikao na Wakuu wa Mikoa na akatoa maagizo ambayo nashukuru Mungu Kwa sehemu fulani yalitoka kwenye thread niliyoiandika hapa JF

Nirudi kwenye mada!
Watu wengi walipoona Rais Samia anatoa yale maagizo walifikiri kuwa kamwe hayatofanikiwa, Kuna wengine walidhani kuwa ndo Kama maagizo ya siku zote ya wanasiasa wa Tanzania ambayo hayazingatiwi, Kuna wengine walidhani as long as ni mwanamke basi ni dhaifu hivyo maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi, Kuna kundi lingine ni kwa chuki zao tu walimkatisha tamaa Mama samia na kuongea maneno ya kejeli kumdhihaki ili kumfanya aone tu hatoweza!

Nimekuwa jijini Dar es Salaam kwa wiki sasa na nimetembea sana Jiji la posta na hata maeneo ya Ubungo na mwenge, napenda kusema kwa sauti kuu na moja
HONGERA MAMA SAMIA, ZOEZI LINAKWENDA VIZURI NA SURA YA MJI WETU WA DAR UNAOJENGWA KWA GHARAMA KUBWA NA SERIKALI IMEANZA RASMI KUONEKANA.

Nilisema humu na ninasema tena, suala la machinga kamwe, haliwezi kuwa mfupa mgumu kwa serikali, kilichokuwa kunasababisha kutokea yale tuliyokuwa tunayaona awamu ya tano kurudi nyuma ni

1. Viongozi kukosa commitment ya kushughulikia mambo ya msingi

2. Siasa ya kijinga, uvivu na uzembe kwa viongozi hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri

3. Ushamba na kukosa exposure

Kwa mwezi sasa tumeona viongozi wakikomaa kushughulikia suala la machinga na sasa imeanza kuonekana kuwa kumbe inawezekana Kwa machinga kupangwa na kufanya biashara kistaarabu

Kwa Mafanikio haya niliyoanza kuyaona sasa napenda kuishauri Serikali ya Awamu ya Sita kuzingatia haya

1. Msibweteke kwa mafanikio mliyoanza kuyapata hasa baada ya machinga wenyewe kukubali kupangwa baada ya serikali kuweka msisitizo! Maeneo Yaliyokuwa wazi sasa yawekewe ulinzi na utaratibu maalum ili kutoruhusu hali ya huko nyuma kujirudia tena

2. Kuwe na by laws za faini na hata kufanya kazi za kijamii kwa watu wanaokiuka taratibu na kurudi kwenye maeneo waliyoondolewa

3. Ziundwe kamati za wafanyabiashara wenyewe kusimamiana wenyewe ili kutoruhusu sheria kuvunjwa tena na hali kurudi Kama ilivyokuwa.
Mf. Kwa kariakoo Wafanyabiashara wa pale waunde kamati zao na vikundi vyao vya kusimamia usafi na ufanyaji biashara kwa kuzingatia taratibu . Kamati hizi sipewe meno na mamlaka ya kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe pale taratibu zilizowekwa zinapokiukwa

4. Kwa maeneo wanayopelekwa machinga! Naomba sasa mkazo uwekwe huko, miundombinu Bora na ya kisiasa ijengwe huko. Wafanyabiashara hawa wapangwe na kusimamiwa vizuri chini ya kamati za wao wenyewe watakaoziunda. Wapangwe kisasa na kistaarabu kwa kuzingatia aina ya biashara wanayofanya

Wafanyabiashara hawa wawekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kidogo kidogo na jamii ielekezwe kwenye kununua bidhaa kwenye maeneo hayo walikopangiwa wafanyabiashara hao. Vijengwe vituo vya mabasi kwenye maeneo hayo ili ununuzi wa bidhaa uwe rahisi

Naomba niishie hapa Kwa leo
Kwenye suala la USHAMBA na kukosa exposure nimekuelewa. Watu wasiokuwa na exposure wanaiona Tanzania kama ndio dunia yote iko hivyo.
 
Back
Top Bottom