Kwa mara ya kwanza niliijua maana halisi ya "Mtoto wa kishua" kupitia huyu dogo. Kuna watoto wamezikuta pesa aisee!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Nilikuwa nimeripoti chuoni mwaka 2011 kwa mara ya kwanza baada ya kuhihitimu form 6,

Nilifikia hostel mnakaa watu wawili kwenye chumba, nilimkuta dogo flani yeye kamaliza form 4, alikuwa ameshaanza form 5 lakini aliachana nayo ili asome chuo.

kwa haraka haraka tu nilijua kwamba huyu dogo nimemzidi umri ila siwezi kumsogelea hata robo ya uchumi wake, simu aliyokuwa anatumia ni bei mbaya mno. Blackberry bold touch 9900, simu nyingine ya ziada alikuwa haitumii sana ilikuwa i phone 4, dogo hakuwa na noma kuniazima niitumie mara, hii simu ilinipa sana title chuoni. Kiufupi kwenye uwanja wa masimu na matablet dogo alikuwa updated sana, anazibadilisha kama daladala.

Ukiwa huishi na huyu dogo ilikuwa ni ngumu sana kuyajua maisha yake kiuchumi, alikuwa anavaa kawaida tu, hana fujo ya pesa, haringishii alivyonavyo, huji kumsikia akisema baba yake ana cheo flani, n.k ni mpaka uishi nae ndio utamjua.

Pocket money yake ilikua laki 6 hadi 8 kwa enzi hizo hii ilikuwa pesa ndefu ssna, na hapo kati kati ya mwezi kuna laki 3 ya matumizi mengine, kila chuo kikifungwa alikuwa anatumiwa pesa ya tiket ya ndege, kuna kipindi niliwahi kumshawishi tiketi ya kurudi chuoni nilimwambia apande basi, atunze pesa kuna mradi nataka tuufanye, hio pesa yote iliishia kwenye nyama!!! alafu hata huo mradi wa mchongo aliuliziaga mara 2 tu, hadi leo akikumbushia mradi huwa tunacheka sana.

Alinitoa ushamba wa vitu vingi sana, nilizijua pizza kupitia yeye, nilizijua kumbi za sinema kupitia yeye, niliijua mitaa ya dar ambayo ipo kimya yenye nyumba kali kupitia yeye (sikumbuki jina la mtaa mimi sio mwenyeji dar), n.k kiukweli vilikuwa vitu vingi sana.

huo mda wote kaja kusoma chuoni ili tu apoteze mda aende zake kusomea nje, ada aliiacha na mitihani ya kumalizia muhula wa meisho hakufanya, yani nilibaki nashangaa sana, nilimshauri apige pepa achukue hata cheti ila alikomaa na mpiango yake.

Dem wake alimgeuza kuwa atm, nilikuwa natamani kumnasa vibao huyu dogo

Kuna kipindi dogo nusu nimzabue vibao 😂 kapata dem mjanja sio poa, kampanga dogo kwamba ana maisha magumu, dogo akawa anampa elf 50 kila baada ya siku 3 ama 4, nilipogundua nilikuwa napatwa sana hasira maana dogo alizidiwa sana akili hapa, nilimshauri sana dogo awe mjanja linapokuja swala la wanawake ila dogo kichwa kizito, siku dogo kasafiri weekend karudi kwao sijui alipangwa vipi, kanitumia laki 2 na nusu eti nikampe dem wake iwe kama sapraiz, kiukweli uso ulijaa ndita za hasira, yani laki 2 na nusu kiboya boya tu hivi dogo anapunwa mchana kweupe!! dogo mda huu nilimkaripia na kumfokea sana kwa hasira astuke anachezewa lakini yeye alikuwa anacheka tu, angekuwa karibu ile siku nilikuwa nampiga vibao, niliona dem wake kamwambia aje aongee na mimi nimpe pesa yake, dakika 5 si nyingi kashatia maguu, nilijituliza chumbani kimyaaa.

Aligonga hodi kama dakika 4 hivi siitiki simu nimeiweka silent, 😂 baadae sana nilimpa elf 80 tu, elf 20 niliikatia kwangu kupunguza hasira, hiyo nyingine nilimwambia dogo ampe mwenyewe siku akirudi, siku anaenda kumpa nilimsihi sana lakini wapi aisee, baada ya miezi miwili dogo ndio anakuja kustuka dem wake hajatulia ni mapepe mtoto wa mjini, dogo alikuwa hoi bin taaban kitandani siku 2, dogo aliumia sana ila liikuwa ni fundisho muhimu sana kwake maana alikuwa anachezewa kama mtoto.

Siku anaondoka nilimsindikiza hadi maeneo ya kusubiri gari ya airport, ile narudi kanitumia mesej "oya cheki chini ya blanket lako" nilidaka boda boda chap sana, kwenda kufunua, dogo aliniachia sim moja mashine sana samsung galaxy s2, hapo kuna ile iphone 4 ambayo niliificha ili machawa zake wasiione nilikuwa naitumia kisiri siri ila yeye ni kama aliipotezea mazima hana habari nayo, nami niliweza kuwa mini boss maana si kwa kushobokewa kwa zile mashine.

Dogo alienda nje kusoma, alirudi kipindi cha Magu, ajira zimebana si mchezo, lakini kama muujiza flani, fasta tu kakamata kazi nzuri tu huku akiwa mdogo tu, ana kazi nzuri lakini yeye hataki kuajiriwa, lengo lake aache kazi ili akuze miradi yake ambayo alishaianzisha kwa scale ndogo ila inapanuma mdogo mdogo. Kwa sehemu aliyopo mtu kama mimi na wengine ambao tupo mashirika/taasisi za kawaida, tukiingia hapo tushapiga bao msisha maana mishahara ni ni mizito, posho na allowance za kutosha, watu wanasomesha watoto hata watatu feza boys / girls kwa mpigo 😁😁

Mawasiliano yapo ila sio kivile sana maana hata mikoa ni tofauti, sana sana ni kuchekiana maisha kwenye status, kupeana heri za mwaka mpya, idi, pasaka, n.k. bila kusahau utani wa mpira kwa kila mechi mtani wa mwenzake akifungwa basi kuna kijembe hapo, kiufupi nlitegemea cheo, elimu ya Ulaya, status yake itamvuruga akili kama tulivyozoea wengi ila naona kwa hawa watoto waliozikuta washazoea haya mambo,

Kiufupi hii nchi kuna watu watu wana pesa sana, usije kuthubutu kusema hatuna pesa. cha ajabu ni kwamba nae alikuwa anajiona wa kawaida sana hajafikia level za wakishua, hapa ndipo nilikuwa nachoka aisee!
 
Nilikuwa nimeripoti chuoni mwaka 2011 kwa mara ya kwanza nikiwa nimehitimu form 6,

hostel kulikuwa na vyumba ambavyo mnakaa watu wawili wawili, Nilimkuta dogo flani yeye kamaliza form 4, alikuwa ameshaanza form 5 lakini aliachana nayo ili asome chuo

kwa haraka haraka tu nilijua kwamba huyu dogo nimemzidi umri ila siwezi kumsogelea hata robo ya uchumi wake, simu aliyokuwa ya bei mbaya mno. black berry bold touch 9900, simu nyingine alikuwa haitumii sana ilikuwa i phone 4 nakumbuka nilikuwa naitumia mara kwa mara, hii simu ilinipa sana title chuoni...yani dogo alikuwa ana badilisha simu karbu kila baada ya miezi miwili hadi sio poa.

Pocket money yake laki 6 hadi 8, hata uwe na boom husogelei kabisa, hapo kila chuo kikifungwa alikuwa anakatiwa tiket ya ndege, ile tiketi ya kurudi chuoni nilimwambia apande basi, atunze pesa kuna mradi nataka tuufanye, pesa yote iliishia kwenye nyama aisee, hadi leo tukikumbushana huwa tunacheka sana.

kuna kipindi alikuwa kakosana na girl friend wake sasa kanipa laki 2 na nusu niende kumpa gf wake,
Kumbe humjui Kiduku Lilo a.k.a Bill Lugano
 
Ndo hivyo mkuu Kuna madogo ukimhadisia life la ulikotoka anakushangaa,shida anasikiaga tu!! mm Kuna dogo tulisoma nae ss Kuna sku dogo akaamua kuja na semi trailer mpya kabisaa,tunashangaa semi imeleta nn ,kumbe dogo kaja nayo,halafu akashuka akaenda mpaka nyuma ya trailer akapanda na kutoa begi ya madaftari .kumbe dogo alifanya makusudi kisa Kuna siku alinyimwa lift na tcha .
 
Nilikuwa nimeripoti chuoni mwaka 2011 kwa mara ya kwanza nikiwa nimehitimu form 6,

hostel kulikuwa na vyumba ambavyo mnakaa watu wawili wawili, Nilimkuta dogo flani yeye kamaliza form 4, alikuwa ameshaanza form 5 lakini aliachana nayo ili asome chuo

kwa haraka haraka tu nilijua kwamba huyu dogo nimemzidi umri ila siwezi kumsogelea hata robo ya uchumi wake, simu aliyokuwa ya bei mbaya mno. black berry bold touch 9900, simu nyingine alikuwa haitumii sana ilikuwa i phone 4 nakumbuka nilikuwa naitumia mara kwa mara, hii simu ilinipa sana title chuoni...yani dogo alikuwa ana badilisha simu karbu kila baada ya miezi miwili hadi sio poa.

Pocket money yake laki 6 hadi 8, hata uwe na boom husogelei kabisa, hapo kila chuo kikifungwa alikuwa anakatiwa tiket ya ndege, ile tiketi ya kurudi chuoni nilimwambia apande basi, atunze pesa kuna mradi nataka tuufanye, pesa yote iliishia kwenye nyama aisee, hadi leo tukikumbushana huwa tunacheka sana.

Alinitoa ushamba wa vitu vingi sana, niliizijua pizza kupitia yeye, nilizijua kumbi za sinema kupitia yeye, nikiwa likizo nilienda dar na niliijua mitaa ya matajiri dar kupitia yeye (mimi sio mwnyeji sana Dar lakini mitaa anayoishi ilikuwa kimya sana na nyumba nyingi kali sana)

huo mda wote kaja kusoma chuoni ili tu apoteze mda kidogo aende zake kusomea nje, ada aliiacha na mitihani ya kualizia muhula hakufanya, yani nilibaki nashangaa sana, nilimshauri apige pepa achukue hata cheti ila alikomaa na mpiango yake.

Dem wake alimgeuza kuwa atm, nilikuwa natamani kumnasa vibao huyu dogo

Kuna kpindi dogo nusu nimzabue vibao kapata gf ni mjanja sio poa yani, kamanga dogo kwamba ana maisha magumu, dogo akawa anampa elf 50 kila baada ya siku 3 ama 4, nilikuwa napatwa hasira sana dogo anavyochezewa kiduani hivi, nilimshauri sana dogo awe mjanja linapokuja swala la wanawake ila dogo kichwa kizito, na kweli ile pisi ilikuwa kali sana si mchezo na ilijua kumzuzua dogo si kitoto, siku dogo kasafiri weekend karudi kwao sijui alipigwa tukio lipi, kanitumia laki2 na nusu et nikampe dem wake iwe kama sapraiz, kiukweli uso ulijaa ndita za hasira, yani laki 2 na nusu kiboya boya tu hivi dogo anapunwa kama boya, dogo mda huu nilimkaripia sana kwa hasira astuke anachezewa aisee, niliona dem wake kamwambia aje aongee na mimi nimtumie, yani dogo hajui hapo jinsi pesa zinavyotafutwa, niligngewa hodi kama dakika 4 hivi kimya aisee siitiki, uchungu wa pesa mnaujua au mnausikia aisee baadae sana nilimtumia huyo dem elf 80 tu, elf 20 nilienda kula nyama, hiyo nyingine nilimwambia dogo aje akampe mwenyewe akirudi, siku anaenda kumpa nilimsihi sana lakini wapi aisee, baada ya miezi miwili dogo ndio anakuja kustukadem wake hajatulia, siku 2 yupo kiyandani yani mawazo tele, dogo aliumia sana ila binafsi nilifurahi maana alikuwa anapigwa kizembe zembe sana.

siku anaondoka nilimsindikiza hadi maeneo ya kusubiri gari ya airport, ile narudi kanitumia mesej "oya cheki chini ya blanket lako" nilidaka boda boda chap sana, kwenda kufunua yani machozi yalinilenga, dogo aliniachia sim moja mashine sana samsung galaxy s2, hapo kuna ile iphone 4 ambayo niliificha ili machawa zake wasiione nilikuwa naitumia kisiri siri ila yeye ni kama aliipotezea mazima hana habari nayo, vilikaa basi ??

Kiufupi hii nchi kuna watu watu wana pesa sana, usije kuthubutu kusema hatuna pesa
Mpambe nuksi
 
Haya ya Pili toka mwisho.

Inayosema “Nikamsindikiza hadi wanaposubiria gari za Airport “

Imedhihirisha hii ni Chai. Ambayo haina Tangawizi wala Mdalasini
Una kila haki ya kutandikwa viboko kwa kujifanya mjuaji wa vitu usivyovijua.

Ndio nikuelimishe sasa!! kuna magari huwa yanapakia wateja waliokata tiketi wanaokutana sehem kama hotelini ili kusafirishwa kwenda airport, hufaamika kwa jina la shuttle.

Achana na zile gari ambazo zinawashusha abiria ndege ikitua, ili waende sehemu ya kubebea mizigo yao.
 
Una kila haki ya kutandikwa viboko kwa kujifanya mjuaji wa vitu usivyovijua.

Ndio nikuelimishe sasa!! kuna magari huwa yanapakia wateja waliokata tiketi wanaokutana sehem kama hotelini ili kusafirishwa kwenda airport, hufaamika kwa jina la shuttle.

Achana na zile gari ambazo zinawashusha abiria ndege ikitua, ili waende sehemu ya kubebea mizigo yao.
Goddamn right kabisa. Watu sometimes wanashindwa kutofautisha chai na habari za kweli. Rejea kusoma tu utaona ilivo na details nyingi, chai hazipo ivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom