Maana halisi ya Futari na daku

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
KWA HISANI YA USTAADH
Etugrul Bey
Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.

Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.

Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.

Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.

Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.

Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.

Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.

Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.

Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.

Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.

Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.

Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.

Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.

Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.

Arrow roots ni magimbi kwa msio jua

Ni hayo tu!
 
Attachments

  • Cassava.png
    Cassava.png
    125.6 KB · Views: 1
  • Arrow roots.png
    Arrow roots.png
    235 KB · Views: 1

Hili darasa linawahusu zaidi waislamu maana wengi hawana ufahamu na hiki ulichoandika hapa.

Mtu anakula daku ya Biriani Saa 11 sasa huwa najiuliza hapa watu wanafunga kitu gani?
 
una maana ya saa 11 asubuhi au jioni Dr
Ila nadhani inahusu watu wote kujua tu maana ya kufuturu
 
Hio post ya mwaka jana umekuja kuijibu mwaka huu aiseeeeee
 
Back
Top Bottom