Mara ya mwisho kupigana ni chuo nikiwa 1St yr,
Yule mkaka mlokole alizidi kunifatilia, kila time ni kunidis, nlichoka nkamfata kistaarabu, eti ananileteaa wenge, najaribu kumueleza kwa staha, eti ananisukuma, wee nilimzaba bao la usoni, likaanza vurumahi pale, nikaapa leo nataka tuleteana heshima,
Anarusha ngumi nkakwepa, nikavuta mguu jamaa chini, nikamkalia acha nimpe makonde ya usoni 😂😂😂😂😂
Afu vimbwetani, watu wanashuhudia hapo, nilipandwa na hasira ile siku, sijui nilizitoa wapii. Toka palee heshima ilikuwepo sio kwa wakaka wala wadada, eti akawa anasema kwa watu hakubali, ama zake ama zangu, nkamuambia safarii hii nakuua. Niletee ujinga wako. 😂😂😂😂😂
Walikua wanamcheka, dume zima limebondwa 😂😂😂😂😂😂