Kwa mara nyingine leo hili jambo limenifanya nijisikie vibaya sana moyoni

Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea vyema.

kwa wale wenye changamoto, ni maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu kwamba atufanyie wepesi hasa katika kipindi hiki tunapomalizia mfungo wa Kwaresma na tunapoendelea na Ramadhani wengine.

Ni jambo nimelishuhudia kituo cha dala dala leo asubuh katika harakati za kuwahi kutafuta mkate wangu wa siku.

Nikiwa tayari ndani ya dala dala baada ya kugombania sanaa na jasho kunitoka almanusura nivunje laptop yangu kwenye bag, sasa nikawa nime relax nimeshika bomba chuma ya muhindi, Eicher ikawa anataka kutoka kituoni, kisha nikapiga jicho nje kuwatazama watanzania wenzagu watumiaji wa usafiri wa umma. Jicho langu likatua kwa watu watano (5) ambao kwa experience yangu nikatambua hii lazima ni Familia.

Alikua mwanaume 1 kala kanzu safi na barakhashia yake, dada mmoja makamo, watoto wawil (mmoja binti na mmoja mtoto tu kama mwangu wa 3 kuzaliwa nilipomfananisha, like 5 years). Huyu mama na hawa mabinti wamekula baibui sao safii na Hijab.
Ustadh (tumwite hivyo) yeye kwa nyongeza alikua amebena mtoto mdogo wa mwaka hivi kwa makadirio.

Wako kituoni (nisitaje pande gani, msije mkatuponda sie wakaz wa Kilwa road) , kituo kimetapakaa tope zitoo kutokana na mvua zilizonyesha hapo siku mbili nyuma. Ao unatembea kwa tahadhari kubwa kuepa kuchafuka kama sio kuchafuliwa kwa kurushiwa tope na raia au madereva daladala waliokosa ustaarabu.

Hawa watu (hii family nzuri) wanaonekana wapo hapo kwa ajili ya usafirbwa daladala wawahi wanakowahi.

Kiukwel kwa wale watumiaji wa dala dala tunaelewa ilivyo mtihani kupata usafiri wa kutokea nje ya mji kwenda mjini kati kwa mida ya asubuh. Huwa ni wa kugombania sana sana. Sasa nikajikuta nawaza sana kiubinadamu na kumuonea huruma mwamba, kama mwanaume mwenzangu, na kujikuta nafika mbali na kuona kama hii ni kadhia kubwa. Unapandaje na watu wa 5 tena wanawake katika usafiri wa kugombania. Dahh nikajiskia vibaya sana na kuona huruma na nilipo imagine na kujiweka kwenye picha hakika nikaumia zaid na kujiona kama nadharirika sana.

Ukiwa alone fresh tu, ila ukishakua na family kama hiv kiukwel inakupa teso la kihisia. Kukanyagana na kugumiana humo, wife na watoto wako plus lugha za kukera kwenye daladala ,matusi kwakifupi huwapangii watu cha kuzungumza

Mfano mzuri ni daladala za feri, wale wauza samaki utasema wanajuanaga maana wakianzaga kupiga soga unaweza sema wamekaa barazani kumbe tuko na sie wengine humo ndani ambao tume staarabika kidogo.

Nikawaza kwakwel ukishajua una oiting kama hiz na whole family, ni muhimu kujiweka sawa kama baba pale inapobidi lakini (maana maisha tunatofautiana na sio kosa) , bas angalau uwe hata na kahela ka bajaji, mmefika zenu mbagala, chukua bajaji yako, shuka steshen au kariakoo unakokwenda. Au lah subir bas angalau mida kuanzia saa 5 asubuh ambapo msongamano sio mkubwa kama una safar na family yote angalau mnaweza tumia usafir wa dala dala kwa amani kidogo bila bugudha.

MImi sio mpenz wa kutumia sana gari binafsi kuja na kurudi kazini, kwakua kwa kanuni za uchumi wangu naona sio lazima sana. Pia nature ya majukum yangu muda mwingi katika week hua ni kufika na kukaa ofisin so napendelea zaid kutumia daladala kuja na kuondoka home.

Pia kwakua kijiweni kwangu ni saa 12 nimeingia, so saa 11 alfajiri huwa hakuna adha kubwa kama ya kuanzia saa 12 ikikukuta kituoni. Pia natoka late sana around saa 2 usiku, muda ambao dala dala ni usafir comfortable kabisa time hizo ukiondoa foleni ambao hata wanaotumia magar binafsi tunakua pamoja barabarani, haya yoote hunifanya kupaki tu gari.

Lakini moja ya vitu vilinifanya kuona gari kama chombo au zana muhimu ya usafiri, ni baada ya kupanuka familia. I have four kids, na kuna momemt we have to get together going some places, kwakwel kutumia usagir wa daladala ni moja kati ya vitu vilifanya kuona nanyanyasika sana na kuwanyanyasa mke na wanangu, so i had to have one.

SAsa leo hii nilipoona wale ndugu pale kituoni, rohoni kiukwel nikajisikia vibaya sana kama mwanaume na mtu mwenye familia..

Anyway, najua kwel hayanihusu ila mdio hivyo tena sio vibaya ku feel for others.Tujitahid wanaume wenzangu, japo huwa sipend sana ule msemo wa "tutafute pesa" , ila kiukwel pale inapobid tunatakiwa kufanya hivyo.

Ahsanteni
Kuwaonea huruma wengine ni viwango vya juu zaiidi vya kiutu
 
Gari kwa DSM ni hitaji la msingi.
Hasa kwa Wenye familia.

Baba+Mama + watoto kwenye Daladala kwa kweli haileti picha nzuri. Ukizingatia màadili yalivyoporomoka. Sio ajabu ukashangaa mkeo akibambiwa
 
Ila Mungu alivyokua wa ajabu utakuta hao jamaa hata hawaoni shida.

Lakini kiungwana inaleta Hali ya fedheha, Kila mwanaume anapenda heshima hasa anapokua na familia yake.

Nilikutana na jamaa wa Afghanistan akasema ni kosa lajinai kukubali kufedheheka mbele ya Mke wako, Bora upambane hadi ufe.

Ukiwa peke Yako kutumia usafiri wa umma kwanza ni gharama ndogo na vile vile hauumizi kichwa unapaki wapi au purukushani za uendeshaji.

Nimeiwaza hiyo familia kupata daladala ni mtihani wa kwanza, pili kupata vitu wazi wakae wote Kwa utulivu.

Hata hivyo unaubinadam sana, kuwawazia wengine na kujiweka kwenye nafasi yao.

Hii pia inatukumbusha kushukuru Kwa kile tulichojaliwa na kutupa nguvu kuendelea kutafuta zaidi.
 
Gari kwa DSM ni hitaji la msingi.
Hasa kwa Wenye familia.

Baba+Mama + watoto kwenye Daladala kwa kweli haileti picha nzuri. Ukizingatia màadili yalivyoporomoka. Sio ajabu ukashangaa mkeo akibambiwa
Uko sahihi Mtibeli, mimi napanda sana daladala,si mpenz wa ku drive but inapofika suala la kutoka pamoja na family, siwez kutumia public transport. Siwez aisee. Huwi comfortable halaf pia kama baba lazima utajisikia vibaya sana. Imagine mkeo anabambiana kwa ule mbanano wa daladala ambao hauepukiki, it makes u feel so bad.
Nilijiskia huruma sana jana
 
Ila Mungu alivyokua wa ajabu utakuta hao jamaa hata hawaoni shida.

Lakini kiungwana inaleta Hali ya fedheha, Kila mwanaume anapenda heshima hasa anapokua na familia yake.

Nilikutana na jamaa wa Afghanistan akasema ni kosa lajinai kukubali kufedheheka mbele ya Mke wako, Bora upambane hadi ufe.

Ukiwa peke Yako kutumia usafiri wa umma kwanza ni gharama ndogo na vile vile hauumizi kichwa unapaki wapi au purukushani za uendeshaji.

Nimeiwaza hiyo familia kupata daladala ni mtihani wa kwanza, pili kupata vitu wazi wakae wote Kwa utulivu.

Hata hivyo unaubinadam sana, kuwawazia wengine na kujiweka kwenye nafasi yao.

Hii pia inatukumbusha kushukuru Kwa kile tulichojaliwa na kutupa nguvu kuendelea kutafuta zaidi.
Ni sahihi usemayo mkuu
 
Usafiri wa umma na hasa daladala ni kero na laana kubwa sana. Ni basi tu hatuna magari binafsi ila asubuhi ukifika stand ya daladala unatamani kurudi home.
 
Usafiri wa umma na hasa daladala ni kero na laana kubwa sana. Ni basi tu hatuna magari binafsi ila asubuhi ukifika stand ya daladala unatamani kurudi home.
Na hamna kitu sipendelei kama kuoanda boda boda.
 
Kwa kweli hapa ni changamoto na mateso makubwa, mie wa Mkoani nilikuja hapo kikazi imagine kwa siku mbili tu nikaona mwaka, nikawaza ivi ningekuwa mkazi wa hapa na hawa wanangu (pacha) siku waumwe ikanilazimu kuwa hospital asubuhi na dada wa kazi hapa tunapandaje haya madude ? Leo umenikumbusha siku ile.
 
Nilipofikisha watoto 4 na mdada wa kazi 1 ndio nikaona umubimu wa kutafuta gari. Ni kero kweli kisafiri kwa usafiri wa umma mkiwa wengi. Inaumiza na kusikitisha.
 
Kwa kweli hapa ni changamoto na mateso makubwa, mie wa Mkoani nilikuja hapo kikazi imagine kwa siku mbili tu nikaona mwaka, nikawaza ivi ningekuwa mkazi wa hapa na hawa wanangu (pacha) siku waumwe ikanilazimu kuwa hospital asubuhi na dada wa kazi hapa tunapandaje haya madude ? Leo umenikumbusha siku ile.
Mungu atusaidie sister, ule mji ni kero sana kama huna pesa.
 
Kwa kweli hapa ni changamoto na mateso makubwa, mie wa Mkoani nilikuja hapo kikazi imagine kwa siku mbili tu nikaona mwaka, nikawaza ivi ningekuwa mkazi wa hapa na hawa wanangu (pacha) siku waumwe ikanilazimu kuwa hospital asubuhi na dada wa kazi hapa tunapandaje haya madude ? Leo umenikumbusha siku ile.
Usemacho ni kwel kabisaa. Mazingira hapo yanakua magum sana. Usafiri (japo wa kawaida tu) unasaidia kukiondolea adha kama hizi
 
Back
Top Bottom