Kila ninapofanya jambo hili napata amani sana Moyoni

Von Bismarck

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
3,074
6,254
Habari Watanzania?

Moja kwa moja kwenye mada!

Nimekuwa nachangia damu mara kwa mara kadiri ninapojisikia bila hata shinikizo au ushawishi wowote.

Hii tabia niliianza nikiwa nasoma kidato cha nne mpaka leo.

Ukweli ni kwamba kila ninapochangia Damu, moyo wangu unapata amani achilia mbali amani naona nimeokoa maisha ya mama zetu wakiwa leba, ndugu zetu waliopata ajali, wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.

Kwangu najiona nimetoa Sadaka isiyo ya kinafiki kwa Mungu, sadaka yenye upendo, huruma na thamani sana.

NB: Mungu azidi kuwafanyia wepesi watu wanaopitia mateso na maumivu ya magonjwa au ajali.

Ndugu zangu uhai ni zawadi tunayopewa na mwenyezi Mungu, leo tupo lakini kesho yetu ni fumbo kubwa sana hatuwezi kulifumbua.

Tulio na nafasi yakufanya jambo hili( kuchangia damu) Tafadhari sana tujitoe kwa upendo wa ndugu zetu.

Jamii yetu inahitaji kusaidiana, hivyo tunaweza tusiwe na pesa ya kusaidia, au chakula lakini tukachangia damu zetu kama Sadaka.

Damu ni uhai unapochangia umejitoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine. Mungu hawezi kukuacha kamwe.

IMG_20240212_124634.jpg
 
Jambo zuri...

Kwa upande wangu Napenda sana kufanya kazi bila kushinikizwa au kulazimishwa na mtu.. Huwa inanipa amani sana
upo sahihi, hata jambo lenyewe unalifanya kwa upendo na kwania ya dhati, na ufanisi wake unakuwa madhubuti.
 
Umefanya vema mkuu tuliongezewa damu tuwashukuru sana wachangiagji. Mungu awabariki ni kwa kuwa haturuhusiwi kuchangia hata mm ningependa kutoa damu yangu ili isaidie wengine.
 
Back
Top Bottom