Kwa kuwa CHADEMA ndio chama kikuu, nashauri kampeni zake ziwe kama za Kiinjilisiti

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,938
4,116
Mimi nikiwa namba moja wa kujitolea kufanya kampeni hizo za kiinjilisiti, ambapo zitakuwa za nyumba hadi nyumba, mtu hadi mtu

Kampeni aina hiii huvuna wanachama kwa wingi, na uhakika wa kuwafikia wananchi wengi na kwa haraka zaidi, CCM anachapika vizuri mno na chepesi zaidi, ukweli ni kwamba, aliye na hamu na ccm ni hao viongozi wa ccm tu, lakini wananchi wanahasira mno na chama hiki

Hii inawapa watu wajue sera zako kwa undani na kwa wepesi, huwafanya wapiga kampeni kujibu maswali ya wananchi papo kwa papo na kuwaondolea hofu waliojazwa na kampeni chafu za CCM kwamba kubadiri chama na kukipa kura chama cha upinzani ni kusababisha kutoweka kwa amani

Ningekiomba chama hiki, kitoe nafasi ya kujitolea kwa vijana wasiopungua 1000 kwa kila wilaya ili kazi zianze mapeema kabisa

Kwa namna tulivyopigwa kimfumo na CCM, kama kijana, unangoja nini kujitolea kuelimisha wananchi ili kuachana na ccm isiyo na huruma na wananchi?

Kuikataa ccm ni moja ya sababu ya kuipenda nchi na maliasili zake
 
Back
Top Bottom