Landson Tz
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 295
- 221
Katiba ya sasa ina mapungufu makubwa sana ambayo yanazuia nchi yetu kupiga hatua za maendeleo na kufanya watanzania wengi kuishi katika ufukara wa kutisha. Takwimu zinaonyesha kuwa 96.6% ya watanzania wanaishi chini ya $2 (TSH.4600) na zaidi ya 86% wanaishi chini ya msitari wa umaskini yaani dola 1.25 (2,875).
Turudi kwenye katiba, katiba hii imenyakua madaraka karibia yote na kuyapachika kwa Rais na wateule wake. Lakini kwa bahati mbaya wateule wa Rais walio wengi bado wana angalia matumbo yao na familia zao wanaacha wananchi wakijihangaikia kwa njia za asili kama wanyama pori wasio kuwa na mchungaji!
Ukiacha madaraka, nchi inanuka rushwa na wizi. Kama hadi tume ya uchaguzi inashiriki kuiba (rushwa) kura tutawezaje kupata viongozi wa kutuvusha hapa tulipo. Katiba yetu kupitia tume mbovu ya uchaguzi imezuia mfumo wa vyama vingi kutupatia viongozi mahili mbadala wa chama tawala kwa kuendekeza wizi wa kura pamoja na vitisho vya dola. Na huko chama tawala rushwa imetamalaki na kuzalisha viongozi wabovu .
Imefika hatua hata vijana wetu wasomi wanakosa ajira, wakati hata serikalini upungufu wa wafanyakazi ni mkubwa! Kisingizio ni ukosefu wa fedha kama huna uwezo wa kutafuta fedha za kulipa wafanyakazi kwa nini uchukue fomu kugombea nafasi ya uongozi wakati hauna uwezo wa kutatua changamoto zao!!
Kwa leo naishia hapa nitaendelea ………