Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa

Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa

mshana jr huna haja ya kuhangaika na Dr Slaa.
Washashughulikiwa hawa na wote wenye kupanga hila za kutaka kuliangamiza taifa hili. Watapotea kwenye uso wa dunia kwa haraka sana na wala mali zao walizojilimbikizia kwa njia zisizo halali hazitawasaidia kamwe.
Malizia na AMINA kwenye huu uzi ili sala ikamilike.

Aaamen hekimatele
 
Last edited by a moderator:
mshana jr

Acha kupotosha watu, kanisa katoriki lina sheria zake, ukiwa mtawa/Padre unaruhusiwa kuendelea na huduma maisha yako yote au unaruhusiwa kuomba kumpumzika na kuendelea maisha ya kawaida kama muumini mwingine wa kawaida. Dr Slaa aliomba kustaafu upadre kabla ya ujio wa Papa John II kuja tanzania miaka ya 1999 wakati huo akiwa na katibu wa TEC lkn kanisa lilimwomba asipumzike mpaka ziara ya PAPA ikamilike, kama ingekuwa ni dhambi basi kanisa lisinge mwomba kuendelea. baada ya ziara ya PAPA nchini Dr Slaa alikubaliwa na makao makuu kustaafu na kuagwa na kanisa kwa sherehe kubwa. Baada ya kustaafu Dr. Slaa alirudi kwao Karatu na kuanzisha miradi ya jamii, aliweza kupata wafadhiri mbalimbali hivyo kufanikiwa kuleta maendeleao Karatu. Baada ya wananchi kuona mafanikio yake, walimwomba agombee ubunge, na kweli akagombea kupitia CCM, CCM waliona kama ni mgeni katika siasa wakakata jina lake na kumpa mshindi wa tatu aliyekuwa mbunge wakati huo. Hivyo basi wananchi wakamshawishi kuhamia chama cha upinzani na kuwa wangempa kura, Dr Slaa akahamia CHADEMA wakati huo CHADEMA hakina umaarufu kama sasa, chama kilichikuwa maarufu kilikuwa ni NCCR mageuzi. Dr Slaa akashinda kwa kishindo na kuwa mbunge wa kwanza kutoka CHADEMA na Dr Warid Kabour kutoka jimbo la Kigoma mjini.

Kwa wasio jua Dr Slaa ndiye aliyeanziasha taasisi ya tiba ya CCBRT na ni mkurugenzi wa board. Nafikiri ni taasisi peke hapa nchini inayotoa tiba ya ulemavu wa viungo na macho kwa gharama nafuu.

In 1994: With the support of CBM, Dr. Willbrod Slaa, (still on the CCBRT Board) and Geert Vanneste founded CCBRT. Their mission was to contribute towards poverty alleviation by making rehabilitative services accessible and affordable to people with disabilities. In 1994, CCBRT was registered as a private Non-Governmental Tanzanian Society (NGO), under the Tanzanian Societies Act, No SO8261.
Wewe umemaliza ubishi wote. Hakuna cha laana ya kiapo wala nini.
 
Last edited by a moderator:
mshana jr umesema kila kitu kwa mtazamo halisi kiroho. Na kila aliye wa rohoni au mjuzi wa masuala ya viapo (nadhiri) hawezi kupunguza neno katika andiko lako, zaidi mtu anaweza kuongeza kwa mifano kama ambavyo baadhi wamefanya..
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa hata kiblia ipo hivyo, tunaona pale Daudi alipokua anakwepa kumuangamiza Mfalme Sauli, Daudi alijua yule ni mpakwa mafuta wa Bwana ( Biblia inasema usimguse mpakwa mafuta wangu ), ingawa Mfalme Sauli ali hasi ( sariti imani ) ila utumishi ( yale mafuta bado yalikua ndani yake ) bado utumishi ulikua ndani yake. Ndio maana ile roho mbaya ilipo kua ikimuingia Daudi alikua napiga kinubi basi Mfalme Sauli akawa anapata ahueni.. Tumuombee huyu mzee, chance bado anayo yakupona maana hiki ni kipindi cha neema, ila condition awe mpole tu

Ni kwakuwa ile roho ya kiapo chake bado iko live kabisa na alitamka bila kutegemea...kwa nje kajichanganya na dunia nje ya kiapo chake lakini wito aliouwekea nadhiri bado uko moyoni na hili ndio tatizo
 
mshana jr
Kwanza tufahamu kuwa yaliyotokea na yanayotokea hayana budi kutokea na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Nakubaliana nawe kwamba hatuna uwezo wa kuzuia kila kitu kila wakati! Iwe ni kwa utashi wetu au la!

Pili yote anayoyafanya Kwasasa Slaa hana hiari nayo si kwa maana ya ccm au wale wanaomfadhili kwa sasa bali ni laana ya kiapo na nadhiri zake...hawa wanaomfadhili ni kiambishi tu cha nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu .

Slaa anateswa na haiba na kiapo, nadhiri na ahadi ya kutumikia kiapo.. Nimekutana na viapo Nimeishi maisha ya viapo lakini SIKUAPA. viapo ni vibaya na viapo havifi na kuviuwa kunahitaji mlolongo mrefu na wenye mambo mengi.
Hili la pili napenda kutofautiana nawe kwa kusema Slaa hana hiari kwa anayoyafanya, kwanza tafsiri ya kutokuwa na hiari maana yake kuna shuruti, lakini pia kama hakuna hiari maana yake hakuna ufadhili kwa sababu utafadhiriwa lipi ikiwa mwenyewe huna hiari nalo?

Mwisho sijui umetumia kifungu kipi kuhukumu kuwa Slaa ana laana!.. Ikiwa ni Upadri ni daraja unalosikikwa na sio kuapishwa, unasimikwa na askofu kwa kukuwekea mikono kichwani, kwamba ukawe mwalimu kwa wote.

Kwa mfano wa wale mitume kumi na wawili wa Kristo, unapo simikwa unaweka nadhiri kuwa mtume wa kristo kwa watu wote. Nadhiri ni dhamira ya kweli uliyonayo kwa hiari yako lakini sio kiapo, maana huapishwi au kujiapisha kwa kuwa kiapo ni ahadi ya lazima.

Slaa Aliitwa kwa wito kuonyesha na kutumia vipawa vyake kwa njia ya upadri akakubali na kupokea mpaka daraja la upadirisho mbele ya mimbari takatifu...aliingia mkataba na Mungu na kukamilisha wito. Bahati mbaya sana akakengeuka nakuanguka moja kwa moja na tangu hapo viapo nadhiri na laana vikaanza kumuandama. Siasa sio dini siasa ni propaganda siasa ni unafiki siasa haina kweli na Siasa haiongozwi na roho mtakatifu.

Ni kweli aliingia mkataba na Mungu tena sio wa kulazimishwa bali voluntary agreement, kuwa padri hulazimishwi. Ikiwa umekuwa pdr na ukafikia mahali ukaona siwezi kutimiza utume wangu kwa kutumia madhabau unafanyaje?

Ukizingatia Siasa sio Dini hivyo ili uweze kuwatumikia hawa unao ona bado wamefungwa kwenye minyororo ya utumwa kifikra unafanyaje? Rejea Mwl Nyerere alitambua siasa sio dini na akabaki Siasani lakini alitembea na vitabu viwili Azimioa la Arusha na Biblia.

Usiopotoshe kazi za roho mtakatifu, huyu tuliachiwa na Kristo ili atuongoze katika yote yenye kweli ndani yake.

Kwa laana ile ya kiapo na nadhiri akajikuta anaangukia kwenye Ulimwengu wa mapepo na roho za kutangatanga.. Na tangu hapo ameendelea kutangatanga kuanzia kwenye mahusiano mpaka kwenye maisha.
Hakuna ambacho ameweza kufanya kikakamilika, amekosa ndoa takatifu amekosa maisha ya kudumu Kwenye siasa amekosa Kuacha Heshima na historia ya kutukuka kwenye lolote alilolifanya.
Kila alipoanza alianza vizuri kwa mafanikio na kupendwa sana lakini mwishoni kila kitu kikaenda kombo na kugeuka ubatili.... Kiapo kinamtesa.. Na haya ndio atakuwa maisha yake mpaka kaburini .

Kwa hili sina jibu maana sina ushaidi kwa kauliza za kudhania tu.. Assumption maana hata wewe nikikuuliza utoe ushahidi wa hili huna zaidi ya kujaribu kuunga unga tu. Ila rejea kauli za Kristo Yesu nabii hathaminiwi kwao.

Ina maana pana sana kwa CDM na watanzania wote yaani nataka tu kusema kwamba watu tumedanganywa mpaka tumefikia mahali hatuutaki tena ukweli eti tunadai tumeshaamua… kweli tumefika mwisho wetu…soma.

2Thimothi 4:3-5

Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

Slaa bado anaendelea na utume kwa kutupa elimu sisi tuliokengeuka.

Viapo ni vibaya hakikisha unatengua kama hutaki kuendelea nacho viapo vina roho na roho haifi, mengi mabaya yatamtokea Dr na hii ni kanuni ya kidunia katika Ulimwengu wa roho.

Ulimwengu wa Roho hauchangamani na kanuni za kidunia rudi usome upya theolojia.
 
Kwanza tufahamu kuwa yaliyotokea na yanayotokea hayana budi kutokea na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Pili yote anayoyafanya Kwasasa Slaa hana hiari nayo si kwa maana ya ccm au wale wanaomfadhili kwa sasa bali ni laana ya kiapo na nadhiri zake...hawa wanaomfadhili ni kiambishi tu cha nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu .

Slaa anateswa na haiba na kiapo, nadhiri na ahadi ya kutumikia kiapo.. Nimekutana na viapo Nimeishi maisha ya viapo lakini SIKUAPA. viapo ni vibaya na viapo havifi na kuviuwa kunahitaji mlolongo mrefu na wenye mambo mengi.

Slaa Aliitwa kwa wito kuonyesha na kutumia vipawa vyake kwa njia ya upadri akakubali na kupokea mpaka daraja la upadirisho mbele ya mimbari takatifu...aliingia mkataba na Mungu na kukamilisha wito.

Bahati mbaya sana akakengeuka nakuanguka moja kwa moja na tangu hapo viapo nadhiri na laana vikaanza kumuandama.

Siasa sio dini siasa ni propaganda siasa ni unafiki siasa haina kweli na Siasa haiongozwi na roho mtakatifu.

Umenifunza kitu mkuu, Asante.
 
mshana jr

Nakubaliana nawe kwamba hatuna uwezo wa kuzuia kila kitu kila wakati! Iwe ni kwa utashi wetu au la!

Hili la pili napenda kutofautiana nawe kwa kusema Slaa hana hiari kwa anayoyafanya, kwanza tafsiri ya kutokuwa na hiari maana yake kuna shuruti, lakini pia kama hakuna hiari maana yake hakuna ufadhili kwa sababu utafadhiriwa lipi ikiwa mwenyewe huna hiari nalo?

Mwisho sijui umetumia kifungu kipi kuhukumu kuwa Slaa ana laana!.. Ikiwa ni Upadri ni daraja unalosikikwa na sio kuapishwa, unasimikwa na askofu kwa kukuwekea mikono kichwani, kwamba ukawe mwalimu kwa wote.

Kwa mfano wa wale mitume kumi na wawili wa Kristo, unapo simikwa unaweka nadhiri kuwa mtume wa kristo kwa watu wote. Nadhiri ni dhamira ya kweli uliyonayo kwa hiari yako lakini sio kiapo, maana huapishwi au kujiapisha kwa kuwa kiapo ni ahadi ya lazima.

Ni kweli aliingia mkataba na Mungu tena sio wa kulazimishwa bali voluntary agreement, kuwa padri hulazimishwi. Ikiwa umekuwa pdr na ukafikia mahali ukaona siwezi kutimiza utume wangu kwa kutumia madhabau unafanyaje?

Ukizingatia Siasa sio Dini hivyo ili uweze kuwatumikia hawa unao ona bado wamefungwa kwenye minyororo ya utumwa kifikra unafanyaje? Rejea Mwl Nyerere alitambua siasa sio dini na akabaki Siasani lakini alitembea na vitabu viwili Azimioa la Arusha na Biblia.

Usiopotoshe kazi za roho mtakatifu, huyu tuliachiwa na Kristo ili atuongoze katika yote yenye kweli ndani yake.

Kwa hili sina jibu maana sina ushaidi kwa kauliza za kudhania tu.. Assumption maana hata wewe nikikuuliza utoe ushahidi wa hili huna zaidi ya kujaribu kuunga unga tu. Ila rejea kauli za Kristo Yesu nabii hathaminiwi kwao.

Ina maana pana sana kwa CDM na watanzania wote yaani nataka tu kusema kwamba watu tumedanganywa mpaka tumefikia mahali hatuutaki tena ukweli eti tunadai tumeshaamua… kweli tumefika mwisho wetu…soma.

2Thimothi 4:3-5

Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

Slaa bado anaendelea na utume kwa kutupa elimu sisi tuliokengeuka.

Ulimwengu wa Roho hauchangamani na kanuni za kidunia rudi usome upya theolojia.

Asante kwa kuisasambua post yangu vilivyo sasa naomba uingie huku, ukachote yenye kuwiana na nilichoandika
Oath of fidelity
Oath of allegiance
Priest oath
Confirmation oath
Kiapo ni kiapo na hakuna kiapo kibaya kama cha hiari
Na hili la kusema kuwa Ulimwengu wa kiroho hauchangamani na kanuni za kidunia si kweli kabisa ingekuwa ni hivyo basi ingekuwa haina maana mwili uharibikao kuwa makazi ya kiroho
 
Laana hiyo, na tatizo la laana wewe uliyelaaniwa hujijui kama unatembea na laana hata angetokea mtu akueleza ukweli huo utaendelea kubisha na kujiona uko poa tu
Ebu hii ifanye kuwa kinyume chake....mi naamini wewe unajiona uko poa bila shaka lakini hakika una laana!
 
Umeangukia kulekule kwenye kuhukumu nilidhani utasimamia maneno yako... Na huu ndio uhalisia wetu kuamini tusichokifanya na kufanya tusichokiamini
 
nimeanza kwa kumwambia aifanye hii kuwa kinyume chake.... maana yake aanze kupima maneno yake sijamuhukumu bado.
 
Kwanza tufahamu kuwa yaliyotokea na yanayotokea hayana budi kutokea na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Pili yote anayoyafanya Kwasasa Slaa hana hiari nayo si kwa maana ya ccm au wale wanaomfadhili kwa sasa bali ni laana ya kiapo na nadhiri zake...hawa wanaomfadhili ni kiambishi tu cha nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu .

Slaa anateswa na haiba na kiapo, nadhiri na ahadi ya kutumikia kiapo.. Nimekutana na viapo Nimeishi maisha ya viapo lakini SIKUAPA. viapo ni vibaya na viapo havifi na kuviuwa kunahitaji mlolongo mrefu na wenye mambo mengi.

Slaa Aliitwa kwa wito kuonyesha na kutumia vipawa vyake kwa njia ya upadri akakubali na kupokea mpaka daraja la upadirisho mbele ya mimbari takatifu...aliingia mkataba na Mungu na kukamilisha wito.

Bahati mbaya sana akakengeuka nakuanguka moja kwa moja na tangu hapo viapo nadhiri na laana vikaanza kumuandama.

Siasa sio dini siasa ni propaganda siasa ni unafiki siasa haina kweli na Siasa haiongozwi na roho mtakatifu.

Kwa laana ile ya kiapo na nadhiri akajikuta anaangukia kwenye Ulimwengu wa mapepo na roho za kutangatanga.. Na tangu hapo ameendelea kutangatanga kuanzia kwenye mahusiano mpaka kwenye maisha.

Hakuna ambacho ameweza kufanya kikakamilika, amekosa ndoa takatifu amekosa maisha ya kudumu Kwenye siasa amekosa Kuacha Heshima na historia ya kutukuka kwenye lolote alilolifanya.

Kila alipoanza alianza vizuri kwa mafanikio na kupendwa sana lakini mwishoni kila kitu kikaenda kombo na kugeuka ubatili.... Kiapo kinamtesa.. Na haya ndio atakuwa maisha yake mpaka kaburini .

Viapo ni vibaya hakikisha unatengua kama hutaki kuendelea nacho viapo vina roho na roho haifi, mengi mabaya yatamtokea Dr na hii ni kanuni ya kidunia katika Ulimwengu wa roho.

well said....
Mwenye masikio na asikie
mwenye macho na aone...
11949272_993541010695916_3044781653470782265_n.jpg
 
nimeanza kwa kumwambia aifanye hii kuwa kinyume chake.... maana yake aanze kupima maneno yake sijamuhukumu bado.

Hapana hebu soma ile sentensi ya mwisho uliposema....HAKIKA WEWE UNA LAANA.....
 
Asante kwa kuisasambua post yangu vilivyo sasa naomba uingie huku, ukachote yenye kuwiana na nilichoandika
Oath of fidelity
Oath of allegiance
Priest oath
Confirmation oath
Kiapo ni kiapo na hakuna kiapo kibaya kama cha hiari
Na hili la kusema kuwa Ulimwengu wa kiroho hauchangamani na kanuni za kidunia si kweli kabisa ingekuwa ni hivyo basi ingekuwa haina maana mwili uharibikao kuwa makazi ya kiroho
Kaka nitapitia pia huko tena ingawa nimeshapita pita sana kwingi. Nashukuru kwa ushauri. tupo kwa ajili ya kuelimishana kukosoana na kusameheana walau tufikie mahali pa kufurahia maisha yetu sote.
 
Asante kwa michango yako pia
 
Dr Slaa kaangukia kwa shetani na mtu mwenye mapepo ya kutisha Josephine. Mapepo yatamuua Slaa
 
Hapana hebu soma ile sentensi ya mwisho uliposema....HAKIKA WEWE UNA LAANA.....
Mshana ndicho ulichofanya kwa Slaa na mimi nimekupinga na ndio nikamwambia huyu ndugu afanye kinyume chake yaani yeye awe Slaa, mimi ndio nimwambie kwa uhakika kabisa kuwa ana LAANA KWA HAKIKA ...nawe pia post yako ililenga kutuaminisha hivyo..nemeipinga kama ulivyojaribu kunipinga mimi nilivyo fanya kwa huyu ndugu yetu.

Nashukuru nawe umeingia kwenye mtego huu.
 
Ni kwakuwa tumetawaliwa na utashi wa kibinadamu japo binafsi sijamhukumu moja kwa moja bali nimetoa mtazamo wangu kiroho ambao umelenga alipotoka Dr mafanikio na changamoto zake, alipo na aendako ni rahisi kugundua Hana makazi ya kudumu kila alikopita
 
Back
Top Bottom