Wewe yawezekana ni under 30. Dr. Slaa ni ndiyo kati ya wabunge wa kwanza kabisa CHADEMA na upinzani Dr.Slaa alikuwa mbunge mara ya kwanza 1995, na amekuwa mbunge kwa miaka 15 yaani vipindi 3. Ndiyo maana nasema wewe ni mfuasi wa Lowassa na wala CHADEMA hauijui na upinzani haujui munakurupuka tu muna post vitu vya ajabu - ajabu kwenye mitandao ya kijamii kama haujui CV ya dokta muuliza baba yako au ndugu zako wakubwa.
Dr.Slaa ndiyo mbunge wa kwanza kuwatuhumu na kuwaita vigogo wa serikali kuwa ni mafisadi akiwa mbungeni mwanzoni mwa miaka ya 2000. Dr.Slaa ndiyo mbunge wa kwanza kupinga posho na mishahara mikubwa ya wabunge na viongozi wa serikali mwanzoni mwa maika ya 2000. Ilikuwa kama 2002 ivi au 2003. Wewe vipi?.
Kama haumjui dokta bora ukae kimya unajidhalilisha na kujitafutia laana maana hiyo CHADEMA ndiyo yeye kaijenga mpaka amepata ulemavu wa mkono, wewe vipi? Umaarufu wa CHADEMA umeletwa na dokta. Kama ulishiriki kwenye harakati za CHADEMA kati ya 2007 na 2010 na ukashiriki kwenye uchaguzi wa 2010. Huwezi kulipinga hili. Mimi nimeshiriki uchaguzi wa 2005 wakati huo CHADEMA walimuweka Freeman Mbowe kuwa mgombea wao wa Urais akiwa na sera ya majimbo. Sina hakika kama Mbowe ali add mbunge yeyote mpya baada ya uchaguzi CHADEMA ilionekana kama ilivyo ACT- Wazalendo leo hii, wakiwa na mbunge mwenye mvuto mmoja tu ambaye ni Dr.Slaa. Kama hamuna vya ku-post acheni kujidhalilisha. Vijana acheni utoto wenu, munatuchefua........