Dr. Slaa ni mwanasiasa ambaye wale wapinzani halisi wataendelea kuthamini kila alichokifanya akiongozwa na uzalendo. Alikuwa tayari kuumizwa na kukutana na majanga ya kila aina kwa ajili ya CHADEMA, alikuwa na malengo ya kutengeneza succession plan ya uongozi. Leo hii hawa UKAWA walioshindwa kupambana na nguvu ya fedha, wanamkejeli kama vile hakuna cha maana alichokifanya. Lakini bahati nzuri ni kwamba Mungu husikiliza maombi ya waja wake, hatimaye ile mitandao ya rais wa awamu ya nne na yule mzee wa monduli, imepotezwa kisiasa.
Sasa tumerudi kwenye siasa za ukweli, zisizoongozwa na wanamtandao, marafiki wawili yaani mkwere na mmeru walikuwa wanataka kulivunjavunja Taifa ambalo wazalendo aina ya Dr. Slaa walitumia kila aina ya hekima ili liweze kufika pazuri. Mungu ametuepisha majanga makubwa, kwani mtandao unaomuingiza mtu madarakani, ni lazima utumikiwe, madhara ya mitandao ni ubaguzi ndani ya jamii, watu kutazamana kikabila na kikanda. Yule asiyekuwa wa upande wa mitandao inabidi awanyenyekee wanamtandao ili aweze kupata maisha mazuri.
Kwangu mimi Dr. Slaa alisaidia sana katika kuwakumbusha watanzania kwamba anayefaa ni muadilifu mwenye hulka ya unyenyekevu kwa umma na sio mwanasiasa aliyetumia nguvu nyingi katika kujijengea ngome ya kumpeleka Ikulu.