Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa

Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa

Kama yeye anajua ni ukweli na anaanda press conference ya mamilioni kuusema ukweli, si angeenda tu mahakamani akafungue kesi?
Yakusemwa mdomoni tumeshayasikia mengi hatutaki porojo tena ,mwenye ushahidi akafungue kesi mahakamani FULLSTOP

Mwanasiasa gani ulishamwona akikimbilia mahakamani? Miaka yote CHADEMA wamekuwa wakizunguka na ushahidi wa kashifa mbalimbali, mbona hawaendi mahakamani? Jifunze kazi ya kila Kada.
 
Ni kwakuwa ile roho ya kiapo chake bado iko live kabisa na alitamka bila kutegemea...kwa nje kajichanganya na dunia nje ya kiapo chake lakini wito aliouwekea nadhiri bado uko moyoni na hili ndio tatizo

Aisee ukweli mtupu .
 
It is very sad for what you have written. It seems you have no knowledge of philosophy nor theology let alone the Code of Canon Law of the Catholic Church.In Brief, an ordained catholic priest, in a grave matter can ask voluntarily to be removed of the priestly obligation. The Vatican issues a laicization i.e to reduce an ordained minister(Deacon, Priest, Bishop) to the state of the laity(laici), a normal faithful. An ordained priest receiving this permission can decide to validly marry in the catholic church.God does NOT curse people. To be a priest is NOT a certificate to go to heaven or a sign of sainthood.  Cardinal Rugambwa, the first black African Cardinal and Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere both died.  It is Mwalimu Nyerere who is now venerated by the whole universal catholic church and NOT the Cardinal though Rugambwa was the prince of the Church.Metaphysically, the soul is not confined into the body nor does the soul suffer for the soul is spiritual and thus eternal just as God himself is eternal. It is a fallacy of post hoc ergo propter hoc to think that because someone has renounced priesthood therefore the bad omen will befall his future, could be a mere coincidence. Jesus said don't think that those Jews which the siloam tower had fallen on them are the most sinful people of all the people in Israel.
 
Itakua alimaanisha Mathayo 5 : 33 - 37

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.


Mkuu hebu angalia vzr hii 3:33haipo
 
Hakuna kitu kibaya kama kukariri usichoweza kukisimamia wala kukielezea

Hilo jicho lako la rohoni ni ukengeufu unaotokana na kutaka kutumia Neno la Mungu kuhalalisha matamanio yako. Kumtangazia laana Dr Slaa nikujitakia laana wewe mwenyewe. Sisi tunaoona kwa macho ya nyama hatuwezi kamwe kujikweza mpaka kiti cha hukumu cha Mungu.

Hebu chambua contents zake ukioanisha na hiyo laana inayomsumbua. Anzia pale alipojiunga na siasa mpaka kuijenga CHADEMA, mpaka hotuba yake ya kujitoa CHADEMA. Yapi katika aliyoyaamini yanaashiria amelaaniwa? Naomba ufanye hivyo ili tuone hujakariri. Oanisha contents na biblical curse
 
Ni sahihi kabisa lakini ningependa tujikite kwenye hoja za kiroho zaidi kuliko kisiasa

Kwani hii laana ya kiroho imekuwa triggered na nini? Tofauti yake na CHADEMA au nini? Alipokuwa nasi alikuwa mbarikiwa, alipoturudi alikuwa mlaaniwa! Mwacheni Mungu awe mkweli na wanadamu wote waongo.
 
Mshana Jr

Hongera, ulichosema ni kwa sababu uko upande Fulani kwa hiyo kila utachosema kitaelemea huko. Bahati mbaya nchi yetu haina Wachambuzi Huru wote wameelemea upande fulani.

Dr Slaa analaumiwa kwa kinachotokea Sasa ktk Siasa za Tz, kwa nini kwa sababu kaamua kusema ukweli ambao Mh Mbowe hakuusema, alitudanganya kwamba wamekubaliana na Dr Slaa apumzike atajiunga nao mbele ya safari!

Kwako MshanaJr, wewe ulikua wapi kusema haya uliyoyasema sasa mpaka baada ya Dr Slaa kuamua kufunguka.

Hoja ya CDM ilikua UFISADI ndicho Dr alichosema Je? ktk Kampeni zenu hilo lipo kama halipo kwa nini?

Ilikua bora kumpotezea Dr, kwa jinsi alivyofunguka kuliko kupambana naye tena kwa kumtusi elewa kwamba unatoa nafasi nyingine ya Dr kurudi Hewani jambo ambalo litakua Bomu la kuimaliza CDM

Lowasa ni Mgombea dhaifu kuwahi kutokea ktk CDM hawezi kujitetea kwa kombora lolote litakalo rushwa kwake ana sifa ya kupata Pesa toka kwa marafiki zake kama alivyosema mwenyewe, hawezi na hana maneno ya kuzidi dk 10. Jana Sumbawanga kaongea dk 5 leo Namanyere kaongea dk 5 hii inatosha kumfanya aende lkulu? Kumbuka watu wanakwenda ktk viwanja vya Kampeni kumsikiliza Mgombea, mpiga Kura amekaa uwanjani zaidi ya saa 3 Lowasa anaongea dk 5 hii ni sawa?

Usimtafute mchawi kosa ni lenu wenyewe mmewapa CCM ujasiri ambao hawakua nao kabla poleni kwa sababu kazi iliyokua ifanywe nao mnaifanya nyinyi kujibu Makombora.

Kama Uchaguzi Serikali za mitaa uliibeba CDM kwa Ajenda ya Escrow account basi Uchaguzi huu CCM itabebwa na Ajenda ya Lowasa
 
Sheria za Kanisa lao zimebariki uamuzi wake wa kujitoa, chakuwashiani? Kwa hiyo mapadri wote waliteswa na viapo? Karugendo je, Nkwera ambaye alienda kuanzisha kanisa lake?

Hii sio hoja!
 
Alimuasi Mungu na kutupa mbali upadri, je atasita kuasi UKAWA? atasita kuasi CDM?
 
Mshana Jr

Hongera, ulichosema ni kwa sababu uko upande Fulani kwa hiyo kila utachosema kitaelemea huko. Bahati mbaya nchi yetu haina Wachambuzi Huru wote wameelemea upande fulani.

Dr Slaa analaumiwa kwa kinachotokea Sasa ktk Siasa za Tz, kwa nini kwa sababu kaamua kusema ukweli ambao Mh Mbowe hakuusema, alitudanganya kwamba wamekubaliana na Dr Slaa apumzike atajiunga nao mbele ya safari!

Kwako MshanaJr, wewe ulikua wapi kusema haya uliyoyasema sasa mpaka baada ya Dr Slaa kuamua kufunguka.

Hoja ya CDM ilikua UFISADI ndicho Dr alichosema Je? ktk Kampeni zenu hilo lipo kama halipo kwa nini?

Ilikua bora kumpotezea Dr, kwa jinsi alivyofunguka kuliko kupambana naye tena kwa kumtusi elewa kwamba unatoa nafasi nyingine ya Dr kurudi Hewani jambo ambalo litakua Bomu la kuimaliza CDM

Lowasa ni Mgombea dhaifu kuwahi kutokea ktk CDM hawezi kujitetea kwa kombora lolote litakalo rushwa kwake ana sifa ya kupata Pesa toka kwa marafiki zake kama alivyosema mwenyewe, hawezi na hana maneno ya kuzidi dk 10. Jana Sumbawanga kaongea dk 5 leo Namanyere kaongea dk 5 hii inatosha kumfanya aende lkulu? Kumbuka watu wanakwenda ktk viwanja vya Kampeni kumsikiliza Mgombea, mpiga Kura amekaa uwanjani zaidi ya saa 3 Lowasa anaongea dk 5 hii ni sawa?

Usimtafute mchawi kosa ni lenu wenyewe mmewapa CCM ujasiri ambao hawakua nao kabla poleni kwa sababu kazi iliyokua ifanywe nao mnaifanya nyinyi kujibu Makombora.

Kama Uchaguzi Serikali za mitaa uliibeba CDM kwa Ajenda ya Escrow account basi Uchaguzi huu CCM itabebwa na Ajenda ya Lowasa


Mkuu pokea like yangu;

Kunawatu wamejitoa ufaham mpaka unawaonea huruma,
Kunamtu hum jf akiwahi kuleta uzi kuwa wtz wana iQ ndogo wakati huo sikumweelewa ila sasa namuelewa vzr,

Hao jamaa wanahitaji kupimwa akili, et rais anahutubia dk 5, 7, 6. Halafu yy ndiye mgen rasimi...
 
Hicho ndicho mama yangu alikisema jana,akatoa mifano ya mapadre wengine walioasi kiapo na jinsi walivyoishia. Mimi namhurumia kuangukia ktk mikono ya yule mama, usiku nimeota kwamba she is an agent of the devil. Mama aliudhika sana kitendo cha Slaa kuwapakazia maaskofu.

Miung ikulaani wewe, ilaani na simulizi za UWONGO za mama yako! Mabaya kuweza kumtokea mtu bila kuwa na kisa chochote, kwa hiyo unataka kusema Waafrika wote wa Kongo wanaoteseka wana laana?

Mapadri wengi ni mabasha (nimeota), hicho ni kigezo pekee cha kukufanya uwe na laana. Kuhusu ushetani nadhani hakuna shaka kuwa ni kanisa gani liko karibu na shetani kuliko yote...
 
Ni kweli kabisa ukiamua kumtumikia Mungu usiache
hivi kumtumikia Mungu nilazima uwe padri, mtume, nabii, shemasi, papa, Askofu, Ustaadh, Shekh nk.

Mi siamini hivyo labda mshana jr utusaidie ili dhamira yako ya bandiko la kisiasa mchanganyiko na kidini lieleweke. Kwa sababu umejaribu kutumia dini kwa maana ya nguvu ya kiapo kumsigina Dr. Slaa kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Hayo ya kiroho ni ya kweli kabisa na yanawatesa watu wengi sana. Soi mapadri tu hata wana ndoa ambao waliapa mbele za Mungu kuwa watakuwa pamoja hadi kifo lakini wengine wanaamua kuchepuka na matokeo yake madhara yanakuwa mengi sana ktk familia. Tunapaswa kumheshimu Mungu.
 
Usilete uchawi kwenye Biblia tafadhali. Neno la Mungu lisitumike kuhalalisha tamaa za kidunia. Laana ya kiapo cha upadre inatoka wapi kwenye Biblia? Kwamba Slaa anasumbuliwa na laana ni maneno ya watu wanajaribu kuukwepa ukweli. Kristo alifanyika laana ili awakomboe walio chini ya laana. Slaa si wa kwanza kuacha wito wa upadre. Kinachofanywa ni kupata kibali cha Kutoka lakini daraja la upadre halifutiki. Hivyo title itaendelea milele kwa mujibu wa kanisa katoliki. Muhimu watu wenye busara watajadili hoja alizotoa Dr Slaa kuliko kujikita kwenye teolojia ambayo haina mahusiano na siasa. Laana ionekane leo baada ya kuwaumbua akina mshana, ila kabla ya hapo alikuwa rais wa moyoni mwa watanzania? Acheni ajenda za kipuuzi, jadilini maudhui ya hotuba ya Dr Slaa. Vinginevyo tusihamishe mada tukaleta ubishi wa kiteolojia, taifa ni la imani zote. Mungu akusamehe.

Mleta hoja hajadili ya jana mrudie tena umsome
 
Kwanza tufahamu kuwa yaliyotokea na yanayotokea hayana budi kutokea na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Pili yote anayoyafanya Kwasasa Slaa hana hiari nayo si kwa maana ya ccm au wale wanaomfadhili kwa sasa bali ni laana ya kiapo na nadhiri zake...hawa wanaomfadhili ni kiambishi tu cha nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu .

Slaa anateswa na haiba na kiapo, nadhiri na ahadi ya kutumikia kiapo.. Nimekutana na viapo Nimeishi maisha ya viapo lakini SIKUAPA. viapo ni vibaya na viapo havifi na kuviuwa kunahitaji mlolongo mrefu na wenye mambo mengi.

Slaa Aliitwa kwa wito kuonyesha na kutumia vipawa vyake kwa njia ya upadri akakubali na kupokea mpaka daraja la upadirisho mbele ya mimbari takatifu...aliingia mkataba na Mungu na kukamilisha wito.

Bahati mbaya sana akakengeuka nakuanguka moja kwa moja na tangu hapo viapo nadhiri na laana vikaanza kumuandama.

Siasa sio dini siasa ni propaganda siasa ni unafiki siasa haina kweli na Siasa haiongozwi na roho mtakatifu.

Kwa laana ile ya kiapo na nadhiri akajikuta anaangukia kwenye Ulimwengu wa mapepo na roho za kutangatanga.. Na tangu hapo ameendelea kutangatanga kuanzia kwenye mahusiano mpaka kwenye maisha.

Hakuna ambacho ameweza kufanya kikakamilika, amekosa ndoa takatifu amekosa maisha ya kudumu Kwenye siasa amekosa Kuacha Heshima na historia ya kutukuka kwenye lolote alilolifanya.

Kila alipoanza alianza vizuri kwa mafanikio na kupendwa sana lakini mwishoni kila kitu kikaenda kombo na kugeuka ubatili.... Kiapo kinamtesa.. Na haya ndio atakuwa maisha yake mpaka kaburini .

Viapo ni vibaya hakikisha unatengua kama hutaki kuendelea nacho viapo vina roho na roho haifi, mengi mabaya yatamtokea Dr na hii ni kanuni ya kidunia katika Ulimwengu wa roho.


KATIKA KANISA KATORIKI,,KUNA VYEO AMBAVYO NI PAROKO, MSINYORI, ASKOFU, KADINARI & PAPA AMBAVYO MUHUSIKA ANARUHUSIWA KUSTAFU. LAKINI UPADRI SIYO CHEO BALI NI NADHIRI YA MAISHA NA KUBWA KULIKO NADHIRI ZOTE KWA MWANAUME ALIYEAMUA KUWA PADRI NA HUWEZI KUSITAFUU UPADRI KABISA ILA KUFUKUZWA INAPOBIDI KANISA KUFANYA HIVYO. nilipitia hotuba ya slaa kunasehemu imeandikwa kuwa yeye ni padri mstaafu... sikweli hakuna padri mstaafu.......
 
Cjui ni nn mnashindwa kuelewa, mshana... Amejikita ki Roho

Anae taka kujikita kwa alichokiongea anzisha uzi.

Pili sheria za kanisa sio sheria za Mungu..
Mkuu nadhani tupo tumemwelewa na hata michango au hoja tulizo ziibua zinafanana na bandiko lake, ametamani sana tuungane nae kutumia hoja za kidini kumsigina Dr. Slaa kisiasa. Kwa kisingizio cha ukiingia kwenye utume wa kiroho basi hutakiwi kutoka.

Inawezekana ni kweli au sio kweli sasa wewe njoo na hoja za kweli Dr. ana Laana na ushaidi wako (maana umemuelewa vizuri mshana) na kisha utuonyeshe hiyo laana ni ipi. Kisha njoo na tafisri ya Kiapo, Agano, Nadhiri, Upadri, Siasa, Laana, Hatia nk. Tumia nukuu zozote unazozifahamu au mafundisho yoyote yale... Lakini vyote uvielekeze kwenye kuonyesha alicho fanya Dr. ni batili!

hii itatusaidi labda sisi ambao bado hatujawaelewa ninyi kwa kosa la Dr. kumwelezea EL alivyo.
 
Ni kitu cha ajabu sana binadamu tena Mkristo kutamka hadharani kwamba yeye ni kipimo cha uadilifu katika jamii yake. Ndio maana hata Sumaye alimshangaa Kinana kuwa kama kweli anaweza kuongelea uadilifu basi yeye (Fredrick) ni Malaika!
Hebu jiulize hata Yesu mwenyewe aliyekuwa na kiwango cha juu kabisa alivyoongelea uadilifu aliikana hiyo stage na kusema aliye mkamilifu ni Mungu pekee aliye juu!!
Na kwa kukumbushana tu jamani kuna baadhi ya Maandiko Matakatifu yanayotukumbusha kuwa tusihukumu kabla ya kuhukumiwa na tuishi katika sala kwa kigezo kwamba kuna watu wameishi katika maisha ya kitakatifu lakini muda kidogo kabla ya kumalizia maisha yao wakamkana Mungu na hivyo kulaaniwa. Hivyo hivyo kuna watu wameishi katika dhambi maisha yao yote na karibia na mwisho wakatubu na kumrudia Muumba wao na wakasemehewa!

Maelezo marefu lakini yanaipanua hii picha ya Dr. Slaa kukutana na Dr. Mwakyembe na kisha kumuomba asaidie kuueleza ubaya wa Lowassa kana kwamba EL ni mtu asiyestahili kusamehewa hata pale atakapotubu dhambi zake! EL keshasema kuwa RICHMOND alielekezwa na wakubwa wake basi naye Dr. Slaa atueleze ni kwa nini anaitesa familia yake kwa mihogo na maharage huku akikodisha ukumbi kwa 80m kutushawishi tuichague ccm!
 
Back
Top Bottom