Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Sidhani kama atatokea mwenye KIBURI kama FARAO.

Sidhani kama atatokea DICTATOR kama Adolf Hitler

Sidhani kama atatokea mwenye DHARAU kama Idd Amini

Lakini kwa maajabu ya Mungu yanayoshangaza..
Leo hii wote hao ni MAVUMBI.

Huyu ni Muigizaji walishapita wale Origional.

God's time will tell.
There you talking mtu mzima
 
Ni bora kuwa muwazi kuliko kutoa ahadi hewa! Ingekua yule wa upande wa pili ndiye mwenye mamlaka ingawa alikwenda na kutia aibu vile vile kwa zile hulka zake za mvua za mabomu, ungesikia akisema mambo ambayo utekelezaji wake usingefanyika mpaka anazeeka!
Angekuwa muwazi tangu siku janga limetokea ili kila mtu ajue anajibeba vipi na kipindi anaomba misaada angesema ni kwa ajili ya taasisi za serikali
 
Samahani kutumia maneno haya ....lakini tunakoenda hata Ras akijamba Chadema watatoa tamko kajamba vibaya ....hatari sana..... kukosoa sawa ...ila inapitiliza ....
Lupyee una matatizo makubwa wewe!!!.... Unataka kusema kuwa kama raisi akinanihino.... kwa kuwa tu ni raisi tuseme kuwa kananihino... lakini hii inanukia vizuri sana hivyo tusishike pua!???
 
Wala usipate shida, tafuta hata online kazi ya mfuko wa maafa ulio chini ya ofisi ya waziri mkuu afu utupe mrejesho
mfuko wa maafa una fedha kiasi gani?? na unashugulikia maafa ya aina gani Tanzania nzima?????
 
Mkuu mm cjawahi kulipwa wala kunufaika na lolote kutoka ccm ila penye ukweli ni lazima tuseme ukweli,HV mkuu inamaana swala la kubinafsisha shule kwako kutoka ccm na kuipeleka serikalin kwako unaona ni swala dogo??? HV unajua ni walimu wangapi watapata ajira za kudumu kutoka serikalini?? HV unajua ni wanafunzi wangapi watanufaika na elimu ya bure baada ya kuingizwa ktk mfumo wa serikali??hv unajua kwa kauli ile magufuli ameokoa shilingi ngapi za ada zilizokuwa zinatakiwa kulipwa na wazaz ambao ni watanzania wanyonge wakazi wa bukoba??hebu acheni unyumbu nyie watu hlf siyo lazima ukiwa mpinzani basi ni lazima upinge kila kitu.
Kwani unadhani hiyo ilikuwa bado shule au shule jina.
Wazazi walishindwa kabisa kuiendesha,hapa ni kwamba amekiondolea chama aibu na fedheha.
Ebu jaribu kugoogle matokeo yao ya mwaka jana uone walikuwepo wanafunzi wahitimu wanagapi na matokeo yao yalikuwaje.
 
Hivi wale Wa Magomeni Quarters ilikuwaje? Si Nyumba zinajengwa na watakaa Bureta?
 
Bora kuwa na kiongozi mkweli km magufuli kulikoni wanafki.
Ukweli upi wa kuwasakizia waadhilika wa tetemeko la ardhi kuwa wamebomoa nyumba zao makusudi ili serikali iwajengee mpya.
Kama ni mkweli angeeleza fedha za kitengo cha maafa zilitumika lini kwenye janga hili au kwa nini hazikutumika kukarabati miundombinu,na rambirambi zikawaendea walengwa.
 
Wewe ulitaka wahanga wa tetemeko la ardhi kagera wafanyiwe nini na Serikali? Wajengewe nyumba, kununuliwa samani za ndani, vyombo vya kupikia, kupewa pesa ya kujikimu na kupewa chakula kila siku? hebu tunaomba maoni yako mkuu
Hata kauli ya kiungwana ingewafariji wana Kagera lakini sio kejeri na masimango,hiyo nikuongeza chumvi kwenye kidonda.
 
Sasa nyie mnajipa tabu bure kwani ni mara yake ya kwanza kutoa kauli za kusikitisha ?

Huyu mimi nimemuachia Mungu akakutane naye na ninamuombea sana asije akakutana na ghazabu ya Mungu ,narudia naomuombea sana asije akakutana na ghazabu ya Mungu ...itamla vizazi na vizazi vyake

Bora ghazabu zetu waswahili anaweza akaona ni kelele tu na hakuna wa kumfanya kitu kwa sababu mamlaka ya kutawala dunia hii na vyote vilivyomo kapewa yeye

Kwa hiyo Mtukufu sana unataka kutuambia leo hii ukifa tusihangaike na rambirambi kwa sababu kifo hatujaleta sisi wananchi ? Leo hii tukiugua tusifarijiane kwa sababu magonjwa hajaleta mwananchi ,halafu kwa kauli hizi unakaa kusema uombewe ?
Hayo maombi afanye nani ? Uombewe kwa kipi kwani ulilazimishwa ukae kwenye nafasi hiyo ? Wakuombee waliokuweka kwenye nafasi hiyo pale Chamwino Dodoma ,pamoja na kina Lubuva
Mungu kaseme na huyu kiumbe wako ila nakuomba usiseme naye kwa ghazabu


Poleni wana wa Kagera ,vita ninyi ,tetemeko ninyi,ukimwi ninyi dah ngoja niishie hapa nisije nikalia mbele ya mwanangu
 
Bukoba chakula chao ni ndizi kwa hiyo wanataka serikali iwapelekee ndizi na wana mashamba mahekta ya migomba mi nimekaa bukoba sehem moja inaitwa kiziba kwa wazba na buyango nimekaaa sasa wanataka chakula cha serikali kwani hata ndizi zimekaushwa na tetemeko !!

Huo ni uhuni ni kisingizio tu kwamba hawana chakula ila wanatala kupiga mzigo bora kawambia ukweli
Ina maana chakula kikichokuwa kinatolewa na wasamaria wema kwa wahadhilika wa tetemeko kilikuwa ni kwa ajili ya nini mkuu.
Kukaa kote Bukoba we uliona chakula chao ni ndizi tu kama uliwahi walau kuingia Bukoba sokoni,idadi ya magunia ya mchele yaliyosheheni pale hiyo mikungu ya ndizi hauoni ndani.
 
Zile billion 3-5 zilizokusanywa; kwahiyo tuliikusanyia serikali masaada na si wananchi,
Kufa kufaana.
Kuhusu chakula nadhani hajakosea,kama ardhi ina rutuba
watu walime,ila alitakiwa kuahidi chakula cha muda huu,kuzingatia majani yanaota
mara moja mvua inaponyesha lakini mahindi/mihogo
ili uvune si chini ya miezi mitatu,labda kama majana nayo yanaliwa.

Kuhusu janga la tetemeko,serikali ilitakiwa kutumia michango
ya wahisani na wananchi kutoa walau vifaa kidogo vya ujenzi
afu fedha za serikali(mfuko wa maafa) zijenge miundo mbinu
ya serikali.Sasa mshangao unatushika pale tulipochanga
kusaidia watu walioonyeshwa kwenye TV wakiwa na hali mbaya
leo hii wanaambiwa wasitegemee chochote,hii ni mbaya.

Kilichonifurahisha ni kuwa wanasayansi hawawezi siasa,
wanapiga kama vile wako maabara,maabara kama unapima
damu yenye ukimwi ,vyombo vinakupa majibu yenye ukimwi
kama damu ni salama majibu yanakuwa salama.
 
Vision kama za hitler, ila hitler alikuwa anaona kuwa anachokifanya ni very perfect!!!
Jaman no one who is perfect! Japo pia hao wahanga walishaambiwa "watu wasifikiri hayo matetemeko yaliletwa na serikali"; but tutafika2
Samahani kutumia maneno haya ....lakini tunakoenda hata Ras akijamba Chadema watatoa tamko kajamba vibaya ....hatari sana..... kukosoa sawa ...ila inapitiliza ....
 
Tatizo humu kuna makundi mawili, wanaomkubali na wanaompinga. Kwa hyo lolote atakalofanya mnatafuta namna ya kujustify au kupinga.
Angalia tukio na uchambue, shida unaanza kuangalia uko upande gani halaf ndo unachambua. Yapo mazuri aliyofanya lakini na mabaya pia yapo.
Hayo sio maneno ya kuwaambia wahanga.
 
NA WALE WALIOAHIDI MICHANGO WALETE MICHANGO YAO....hahhaha....ni amri sio ombi....
Hivi nisipopeleka nitafungwa..[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa yanayoendelea akitokea mtu akapeleka mchango mpya au alio ahidi kutoa kusaidia wahanga wa tetemeko kagera...BASI UPIMAJI WA MAGONJWA YA AKILI HAUNA BUDI KUFANYIKA KUUSOMA UBONGO WA MTU HUYO.
 
Tatizo humu kuna makundi mawili, wanaomkubali na wanaompinga. Kwa hyo lolote atakalofanya mnatafuta namna ya kujustify au kupinga.
Angalia tukio na uchambue, shida unaanza kuangalia uko upande gani halaf ndo unachambua. Yapo mazuri aliyofanya lakini na mabaya pia yapo.
Hayo sio maneno ya kuwaambia wahanga.
.
Umeanza gwaride kwa mguu wa kulia! Hakuna kambi mbili--wanaompinga na wasiompinga. Tuongelee wanaopinga hoja x ya mtu y na wanaoikubali hoja x ya mtu y basi. That way, JF will be a home of Great thinkers!
 
Back
Top Bottom