Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Kwa hiyo ulitaka atangaze ahadi kisha asitekeleze? Bora kasema ukweli kuliko kudanganya.
 
Watanzania wavivu wankupenda dezo dezo kwa kila kitu mnatia aibu, mnalalamikaaa hata kuwasoma mnaboa bora mie naishia kwa kichwa cha majanga yenu.
 
Hivi alikuja kuwafariji ama?
Ambao walitoa ahadi ya kuchangia wasitoe kabisa!!Bora wawafikishie wahusika
 
Ninachompendea Rais wangu huyo Dr Magufuli ni kwamba anasema ukweli, iwe tamu ama chungu, yeye atasema tu kama ilivyo. Sasa watu wengine mnapenda mdanganywe, aje aseme tutawajengea nyumba, halafu mtakaaa weee kusubiri hizo nyumba wala hazitajengwa.. bola huyu anasema ukweli ili ujipange kabisa
" to speak is silver but to keep silence is gold" Pope John the second.
 
Mlishaambiwa lazima muishi kama mashetani, mkaanza kufurahia kwa nyimbo na mapambio. Mnapoishi kama mashetani, mnaanza kulia na kusaga meno. NA BADO, HIYO TRELA, MOVIE LITAENDELEA 2021. Mkifika 2025 mmenyooka Nchi nzima!!!!
Sisi sio watu wa mchezo mchezo! Tunafanya tunacho kitamka!
 
MH JPM amewambia watu ukweli, wewe ulitaka awadanganye? Hata km hukukichagua chama tawala lkn ndiyo kinachotawala na hadi unatawaliwa nacho.Kama unadhani wewe genius sana kuliko JPM,gombea 2020 uchukue nchi tukuone.
Tatizo hapa sio ukweli anaousema leo ila ni uongo alioutumia mwanzo wa kuomba misaada kwa ajili ya waathirika afu akaitumia kukarabati miundombinu ya serikali, afu ikumbukwe alitoa katazo la watu kuwasaidia wahanga direct ila misaada yote ipitie serikalini
 
Wewe ulitaka wahanga wa tetemeko la ardhi kagera wafanyiwe nini na Serikali? Wajengewe nyumba, kununuliwa samani za ndani, vyombo vya kupikia, kupewa pesa ya kujikimu na kupewa chakula kila siku? hebu tunaomba maoni yako mkuu
Wala usipate shida, tafuta hata online kazi ya mfuko wa maafa ulio chini ya ofisi ya waziri mkuu afu utupe mrejesho
 
Maandalizi sikulala usiku kucha nikiandas hotuba hii kwa wa miezi takribani mitano ninawaza nimeairisha kwena Zambia na nchi nyingine ili niandae hotuba hii ya leo.
Hivi Rais hana washauri au ni nani anaye muandikia hotuba....yaani Rais akisimama huwa ninafumba macho na masikio maana lazima atachafua khali hewa tu kwa kauli zake.
 
Ni bora kuwa muwazi kuliko kutoa ahadi hewa! Ingekua yule wa upande wa pili ndiye mwenye mamlaka ingawa alikwenda na kutia aibu vile vile kwa zile hulka zake za mvua za mabomu, ungesikia akisema mambo ambayo utekelezaji wake usingefanyika mpaka anazeeka!
 
Hivi kwnn mnapoadress mnasingizia wasaidizi wa raisi kama yy alikuwa mjumbe wa kamati ya usalama kagera sasa wasaidizi wake wamemdanganya vipi

Anyywayy raisi weru hakosei kabisa na yy ni mkweli daima poleni wanakagera
 
Tatizo hapa sio ukweli anaousema leo ila ni uongo alioutumia mwanzo wa kuomba misaada kwa ajili ya waathirika afu akaitumia kukarabati miundombinu ya serikali, afu ikumbukwe alitoa katazo la watu kuwasaidia wahanga direct ila misaada yote ipitie serikalini
Watu hawamuogopi mungu siku izi, dah!
 
Lakin mi bora anaekwambia ukweli sasa, ili ujue unajipanga VP, kuliko yule anaekufariji na kukuahidi halaf asitimuze hyo ahadi
 
Ukitaka kuwa na afya ya roho na mwili ifundishe akili yako kuona ya kwamba ni wewe mwenyewe ndio unapaswa kujitegemea na kujisaidia na si mtu mwingine.

Kweli kuna wakati tunahitaji kupata msaada kwa wengine lakini wakati huo huo wa kusubiri msaada tafuta njia mbadala we mwenyewe uone unatoka vipi kwenye shimo uliopo. Pia jiwekee akilini mwako kwamba msaada sio lazima upate inategemea na huruma ya mtoaji huo msaada.

Haya mambo ya kutegemea sijui serikali sijui wahisani ndo maana hatuendelei sio mwananchi mmoja mmoja wala taifa.

Misaada inakuja na longo longo kibaooo mara nitakujengea hospital msosi utajijua mwenyewe. Sasa hapo faida ya kusubiri msaada iko wapi? Msaada unaweka kama akiba ukija unabeba unaendelea na mishe zako.

Tupambane tu ndugu zangu wenyewe serikali haina mpango wa kututoa wala nini. We fanya hustle zako mwenyewe, omba Mungu kama una amini. Hiyo ndio option tuliobakiwa nayo.

NB: SIUNGI MKONO DHULUMA
 
.
Mimi siyashangai maneno haya. Mara zote ninapokuwa nasimamia dissertations za wanafunzi wangu, sura ya tatu (methodology) hutugombanisha. Huwa namwuliza kila mwanafunzi: What is your research philosophy? Wengi wanakuwa hawajui. Inabidi kuwaongoza taratibu.

Kimsingi kuna research philosophies mbili: Realism / Postitivism Vs Phenomenology / Constructionism. Hao wa kwanza wanasema koleo ni koleo, sio kijiko. Yaani, ukweli unagunduliwa, hauchongwi na msemaji. Hawa wa pili wanasema koleo inaweza kuitwa kijiko bila tatizo kubwa. Yaani, ukweli unaweza kuchongwa, 2+2 ikawa tano, kwa sababu kura zilizopigwa zinasema hivyo!

Ni maoni yangu kwamba, viongozi wa dini ni phenomenologists. Hivyo, unaweza kuelewa kwa nini, wametofautiana na JPM juzi kuhusu suala la UKUTA wa Chadema. Kuna mifano mingine mingi ya aina hiyo.

Kwa ujumla, tangu tupate uhuru tulikuwa na marais wanafenomena. Sasa kwa mara ya kwanza tunaye rais mwanasayansi. Tuukubali ukweli huo. He is a positivist, fulstop. Hivyo, tunapojadili kauli zake tuzijadili tukiwa tumevaa miwani ya positivism. Tutamwelewa, hata kama hatukubaliani naye.
Hivi kumbe wewe ni mhadhiri!!! Haya subiria uteuzi naona hicho ndo unatafuta
 
(i) "Waambie hao wanasiasa wawajengee hizo nyumba zenu wenyewe.. "

(ii) "kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe..,"

(iii) "jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya serikali, siyo kujenga nyumba za wananchi"

(iv) "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani"

(v) "sasa mkuu wa wilaya nataka nikueleze hapa.., sitaleta chakula hapa, hakuna chakula cha serikali, serikali haina shamba "

(vi) " nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie"

>>>> Hayo ni ya maneno ya 'FARAJA' kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli akiwa Kagera leo.., una maoni yapi katika kauli hizo za Rais wa watanzania wakiwepo wale wahanga qa tetemeko kule Kagera!!?

Binafsi; sina deni hata chembe.., hii dhambi haiwezi kunitafuna (ya kuichagua CCM).., siyo mmoja kati ya wale ambao walichagua CCM.., siyo mmoja wapo kabisa!
Sasa mkuu unajifanya bingwa wa kunukuu kauli za rais kutaka kutuaminisha alichoongea ni uongo?, je, kuambiwa kila mmoja abebe msalaba wake mwenyewe ni tusi?, wanasiasa wanaowahadaa wananchi kuwa ni jukumu la serikali kujenga nyumba zilizobomoka huku wakitumia shida ya tetemeka kujiongezea umaarufu sasa wakiiambiwa wawajengee wananchi hizo nyumba ni tusi?, rais kawaeleza ukwel ambao serikali yake itatekeleza ikiwemo ukarabati/ ujenz wa miundo mbinu iliyoharibika. Miundo mbinu hiyo kumbuka inatumiwa na wanakagera hao hao.pia suala la njaa halihusian na tetemeka hivyo wananchi wote wanapaswa kafanya kazi kwa bidii ikiwemo kulima na wajiwekee akiba za chakula, sasa serikali huwa inalima wapi hadi ianze kugawa chakula kila sehemu?, hatukatai utaoji wa misaada ya chakula kwa mazing mf yametokea mafuriko na chakula kimeharibiwa maji hapo hakuna namna lazima serikali isaidie.
 
Back
Top Bottom