.
Mimi siyashangai maneno haya. Mara zote ninapokuwa nasimamia dissertations za wanafunzi wangu, sura ya tatu (methodology) hutugombanisha. Huwa namwuliza kila mwanafunzi: What is your research philosophy? Wengi wanakuwa hawajui. Inabidi kuwaongoza taratibu.
Kimsingi kuna research philosophies mbili: Realism / Postitivism Vs Phenomenology / Constructionism. Hao wa kwanza wanasema koleo ni koleo, sio kijiko. Yaani, ukweli unagunduliwa, hauchongwi na msemaji. Hawa wa pili wanasema koleo inaweza kuitwa kijiko bila tatizo kubwa. Yaani, ukweli unaweza kuchongwa, 2+2 ikawa tano, kwa sababu kura zilizopigwa zinasema hivyo!
Tangu tupate uhuru tulikuwa na marais wanafenomena. Sasa kwa mara ya kwanza tunaye rais mwanasayansi. Tuukubali ukweli huo. He is a positivist, fulstop. Hivyo, tunapojadili kauli zake tuzijadili tukiwa tumevaa miwani ya positivism. Tutamwelewa, hata kama hatukubaliani naye.
Mkuu;
Huwa sipendi kupinga na haswa kilichoandikwa na msomi. Ila, naomba kwa unyenyekevu nkuulize; Umeandikani?? Tuseme, umekubali kuwa nafuu angejikalia darisalama akala mabaki ya New year, au alichohubiri ndio sahihi??
Nilivyo msikia nkajiuliza:
Kwanza kumbe ndo maana hakutaka kwenda kule japo alivunja safari kwa ajili ya tetemeko hilo? Mahela yale yote yalokusanywa kuwasaidia wenzetu, hayakuwa tena rambirambi bali uwezo wa kujenga miundo mbinu??
Jamani, tuache, Tz kuonesha dalili za kuipinga ccm ni majanga matupu. Waweza tolewa ngozi, kisu ndo kikashtakiwa. Kweli, ile sauti yake si ya baba mwenye nyumba.
Angewaacha hivyo hivyo waugumie maumivu yako, huenda wakasahau mapema. Naona amewafanyia ka mama aliyefanyiwa upasuaji halafu mtoto akafa. Maumivu ni mazito zaidi.
Ati; Hao wana siasa wawajengee, wajua; huenda kuna aliyekupigia kura miongoni mwa waliokataliwa msaada. Je, atakuonaje?? Uzuri wa Mtz anasahau kabla ya jioni kufika