Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,704
2,000
(i) "Waambie hao wanasiasa wawajengee hizo nyumba zenu wenyewe.. "

(ii) "kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe..,"

(iii) "jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya serikali, siyo kujenga nyumba za wananchi"

(iv) "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani"

(v) "sasa mkuu wa wilaya nataka nikueleze hapa.., sitaleta chakula hapa, hakuna chakula cha serikali, serikali haina shamba "

(vi) " nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie"

Hayo ni ya maneno ya 'FARAJA' kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli akiwa Kagera leo.., una maoni yapi katika kauli hizo za Rais wa watanzania wakiwepo wale wahanga qa tetemeko kule Kagera!!?

Binafsi;
Sina deni hata chembe.., hii dhambi haiwezi kunitafuna (ya kuichagua CCM).., siyo mmoja kati ya wale ambao walichagua CCM.., siyo mmoja wapo kabisa!
 

erique

JF-Expert Member
Apr 23, 2010
552
1,000
Ninachompendea Rais wangu huyo Dr Magufuli ni kwamba anasema ukweli, iwe tamu ama chungu, yeye atasema tu kama ilivyo. Sasa watu wengine mnapenda mdanganywe, aje aseme tutawajengea nyumba, halafu mtakaaa weee kusubiri hizo nyumba wala hazitajengwa.. bola huyu anasema ukweli ili ujipange kabisa
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,964
2,000
Sidhani kama atatokea mwenye KIBURI kama FARAO.

Sidhani kama atatokea DICTATOR kama Adolf Hitler

Sidhani kama atatokea mwenye DHARAU kama Idd Amini

Lakini kwa maajabu ya Mungu yanayoshangaza..
Leo hii wote hao ni MAVUMBI.

Huyu ni Muigizaji walishapita wale Origional.

God's time will tell.
 

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
405
1,000
Ninachompendea Rais wangu huyo Dr Magufuli ni kwamba anasema ukweli, iwe tamu ama chungu, yeye atasema tu kama ilivyo. Sasa watu wengine mnapenda mdanganywe, aje aseme tutawajengea nyumba, halafu mtakaaa weee kusubiri hizo nyumba wala hazitajengwa.. bola huyu anasema ukweli ili ujipange kabisa
Eah bora
 

nivoj.sued

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
220
250
"Waambie hao wanasiasa wawajengee hizo nyumba zenu wenyewe," "kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe," "jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya serikali, siyo kujenga nyumba za wananchi," "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani," "sasa mkuu wa wilaya nataka nikueleze hapa.., sitaleta chakula hapa, hakuna chakula cha serikali, serikali haina shamba," na " nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie."
.
Mimi siyashangai maneno haya. Mara zote ninapokuwa nasimamia dissertations za wanafunzi wangu, sura ya tatu (methodology) hutugombanisha. Huwa namwuliza kila mwanafunzi: What is your research philosophy? Wengi wanakuwa hawajui. Inabidi kuwaongoza taratibu.

Kimsingi kuna research philosophies mbili: Realism / Postitivism Vs Phenomenology / Constructionism. Hao wa kwanza wanasema koleo ni koleo, sio kijiko. Yaani, ukweli unagunduliwa, hauchongwi na msemaji. Hawa wa pili wanasema koleo inaweza kuitwa kijiko bila tatizo kubwa. Yaani, ukweli unaweza kuchongwa, 2+2 ikawa tano, kwa sababu kura zilizopigwa zinasema hivyo!

Ni maoni yangu kwamba, viongozi wa dini ni phenomenologists. Hivyo, unaweza kuelewa kwa nini, wametofautiana na JPM juzi kuhusu suala la UKUTA wa Chadema. Kuna mifano mingine mingi ya aina hiyo.

Kwa ujumla, tangu tupate uhuru tulikuwa na marais wanafenomena. Sasa kwa mara ya kwanza tunaye rais mwanasayansi. Tuukubali ukweli huo. He is a positivist, fulstop. Hivyo, tunapojadili kauli zake tuzijadili tukiwa tumevaa miwani ya positivism. Tutamwelewa, hata kama hatukubaliani naye.
 

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,704
2,000
Mheshimiwa Rais kweli anafuatilia habari za ulimwengu huu!? .., anasema nini!? Kwamba hajawahi kuona serikali ikiwajengea wananchi wake makazi kisa tetemeko.., OMG..., anatazama habari za kimataifa kweli..,!?

.., amesahau mafuriko ya juzi huko Indonesia..,!? Serikali ya Indonesia ilitoa ahafi ya kuwajengea watu (waathitirika) makazi yao yote bila kubagua!

Wakati sisi tunatafuna rambi rambi za wahanga wa tetemeko kule KGR zilitolewa na wananchi wa kawaida, wadau na wahisani.., wananchi hadi sasa wanalala na kushinda nje.., (tunajenga majengo ya serikali na miundombinu yake) na viongozi wetu wanapiga nyundo za utosi kwenye vidonda vyetu..,

.., nchi ya INDONESIA ilisema wazi, inakwenda kuwajengea makazi ya kuishi wananchi wake wote waliokumbwa na mafuriko ya novemba mwaka huu, yalisemwa na Indonesia's disaster-management agency (BNPD), vijiji 12 katika wilaya 5 vyenye wakazi 60,000 vimeathirika.

Leo kule KGR, (02-01-2017) mheshimiwa Rais anasema hajawahi kuona serikali yoyote ikiwajengea majumba waathitirika wake kutokana na tetemeko (janga la asili).., aisee., nimesikitika sana., najiuliza, mheshimiwa kweli anafuatilia habari za kimataifa!!?

Sasa tujibu maswali yetu.., zile pesa za michango kutoka kwa wahisani, mashirika, taasisi, watanzania kwenda kwenye mfuko wa maafa zilikuwa na lengo la kujenga miundombinu ya serikali tu.., bila kuwasaidia wahanga katika kusimama upya!!?

Tujifunze mazuri kutoka kwa wenzetu hawa.., watu kwanza.., majengo na vitu baadae.., kipaumbele ni watu (kwao) siyo vitu (kwetu)...
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,635
2,000
(iv) "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani"
hivi mtu anayetoa au kutetea kauli kama hii anahitaji maombi-hivi kweli ni nani asiyejua majanga kama tetemeko la ardhi yakitokea hutokea kila mahala mpaka mashambani ambapo watu wamelima mazao,watu ambao wamekumbwa na hilo janga nidhahiri katika sehemu zao mpaka mazao yatakuwa yameathrika.,sasa kwa hili hiyo ni nini jukumu la serikali kama si kuwasaidia watu chakula?????? naomba mnipe majibu nyie mnao tetea kauli ya JPM na kama mazao hayakuharibika watu mbalimbali waliokuwa wanatoa michango yao ikiwemo vyakula kusaidia waathirika walitoa michango ambayo haitakiwi au ???
tafadhali watetea kauli ya JPM naombeni majibu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom