Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Kwa Hotuba ya Kagera, ni bora angekaa kimya

Ningekuwa mm kule bukoba wala nisingekubali matusi km hayo yaani ardhi kuwa ya kijani mana yake majani yamestawi na nyie ndo ng'ombe mule majani serikali haina shamba la chakula
 
nakumbuka kikwete alisema
"naondoka mimi, tuna leta CHUMA hiki. pale nilipo shindwa mim yeye atafanya kwa kasi zaidi. na mlisema mi mpole mpole sasa mabadiliko ya kulemta mkali, na ameanza kutema che cheeeee"
mheshimiwa chapa punda mzigo ufike 2020 maana hamna namna.
 
(i) "Waambie hao wanasiasa wawajengee hizo nyumba zenu wenyewe.. "

(ii) "kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe..,"

(iii) "jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya serikali, siyo kujenga nyumba za wananchi"

(iv) "asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula., hauwezi kugawa chakula ardhi ni ya kijani"

(v) "sasa mkuu wa wilaya nataka nikueleze hapa.., sitaleta chakula hapa, hakuna chakula cha serikali, serikali haina shamba "

(vi) " nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie"

>>>> Hayo ni ya maneno ya 'FARAJA' kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli akiwa Kagera leo.., una maoni yapi katika kauli hizo za Rais wa watanzania wakiwepo wale wahanga qa tetemeko kule Kagera!!?

Binafsi; sina deni hata chembe.., hii dhambi haiwezi kunitafuna (ya kuichagua CCM).., siyo mmoja kati ya wale ambao walichagua CCM.., siyo mmoja wapo kabisa!
Kauli hizi zingetoka kabla ya kuhamasisha uchangiaji sijui kama kungekuwa na mwitikio kama ulioonekana
 
Hapa mtoto ni kuzalia nje tu apate uraia mwingine. Kwa design hii kazi ipo, na watu wanashangilia. Hehehe! Bongo ina vituko
 
"Serikali inatoa mahitaji muhimu tu kama reli, barabara, madawa, shule na kununua ndege... "
 
Huo ukijani Missenyi umeanza 1 Jan 2017? Kulikuwa kukame just a few weeks ago hata ng'ombe walikuwa wanajifia hovyo kwa kukosa majani.

Nimewaona wale akina mama wametoa macho kwa mshangao na taharuki wakati mtukufu Rais akiwapa "vidonge vyao" na kuwakumbusha once again kwamba serikali haina shamba. Sasa wakafanye kazi na tukutane 2020 kupokea elfu 2, chumvi, Tshirt, shanga na khanga.
 
Ninachompendea Rais wangu huyo Dr Magufuli ni kwamba anasema ukweli, iwe tamu ama chungu, yeye atasema tu kama ilivyo. Sasa watu wengine mnapenda mdanganywe, aje aseme tutawajengea nyumba, halafu mtakaaa weee kusubiri hizo nyumba wala hazitajengwa.. bola huyu anasema ukweli ili ujipange kabisa
Hivi kwanini huwa tunatoa rambirambi kwenye misiba!
kuna jinsi yeyote rambirambi inaweza kumrejesha aliyekufa?
je, inafaida gani kwa mfiwa hata akiwa tajiri, fukara huwa tunachanga tu! au ni kujipendekeza?

Anza kujiuliza maswali ya msingi kabla hujaandika!
Hakuna ukweli wowote ktk hili!
endapo serikali ilipokutwa na maafa imeomba misaada kwa watu binafsi na taasisi, iweje leo iwakataze watu wasiombe misaada!
ofisi ya waziri mkuu ilikataza watu wasichangie kwa account yeyote Zaidi ya namba zitakazotolewa na ofisi yake, kwanini basi wasingeruhusu wananchi wajitengezee wenyewe account zao za maafa labda wangeweza kuhamasisha misaada ya kuwatosha!
initially ilikuwa kama jukumu lote lipo kwa serikali, lkn kumbe wao walikuwa wanakusanya zao tu, Mungu aepushe mbali, lkn maafa mengine kama yatatokea inaweza kuwafanya wananchi wakatengeneza accounts zao za misaada!
 
NA WALE WALIOAHIDI MICHANGO WALETE MICHANGO YAO....hahhaha....ni amri sio ombi....
Hivi nisipopeleka nitafungwa..[emoji23][emoji23][emoji23]
Nimecheka sana aisee
 
Sidhani kama atatokea mwenye KIBURI kama FARAO.

Sidhani kama atatokea DICTATOR kama Adolf Hitler

Sidhani kama atatokea mwenye DHARAU kama Idd Amini

Lakini kwa maajabu ya Mungu yanayoshangaza..
Leo hii wote hao ni MAVUMBI.

Huyu ni Muigizaji walishapita wale Origional.

God's time will tell.
Sawaa..!
 
Back
Top Bottom