Ni vigumu sana kukufahamisha wewe unayechukualia wingi wa maghorofa kuwa ndio maendeleo ya wananchi..Ama ukubwa wa koti ndio afya ya aliyelivaa, lakini nitajaribu kama sii wewe wenzako wataelimika.Hapo ndipo pazuri, nakuomba nioneshe haya kama uyasemayo yana ukweli:
1) Umeme: Nioneshe Kikwete kawekeza mpaka sasa MegaWatt ngapi kwenye umeme halafu nioneshe Rais yoyote wa kabla yake pamoja na mkoloni uzijumlishe halafu uniambie hapa Kikwete hajafanya. Nangoja.
2) Elimu, swali ni kama namba 1.
3) Maji safi: swali ni kama namba moja.
4) Na kadhalika: swali ni kama namba moja.
Na ukija na data za uhakika kuhusu maji, shule, umeme na kadhalika (yako), kuwa Kikwete katika kuwekeza kwenye hayo amepitwa na japo Uongozi wote uliomtangulia, leo hii ntaachana na CCM, Its an open challenge.
Ni vigumu sana kukufahamisha wewe unayechukualia wingi wa maghorofa kuwa ndio maendeleo ya wananchi..Ama ukubwa wa koti ndio afya ya aliyelivaa, lakini nitajaribu kama sii wewe wenzako wataelimika.
Kwanza kabisa kosa kubwa unalofanya ktk maelezo yako ni KUELEWA, Bi Faiza huelewi na hutaelewa isipokuwa kwa bakora. Wewe umesema umetuomba mimi na Mbunge wangu kukasome kitabu cha sijui Zungu gani na kuleta mifano kama:- "Kusemwa kwa kiongozi ni kwa maendeleo na si kwa kuwa hajafanya hiki au hajafanya kile. Kusemwa kwa kiongozi ni kuwa kafanya hiki hakikuwa sawa na sasa sisi tunafanya hiki,"
Tatizo lako kujaelewa ulichokisoma. Na itakuwa hakuna maana kwangu mimi na mbunge wangu kwenda kusoma kitabu wakati wewe mwenyewe kujalimika na ulichokisoma, kitakachofuata ni kubishana kama tunavyobishana hapa. Lakini nitakwambia tu kwamba maelezo yote ulozungumza hapo juu yanawahusu nyinyi wana CCM na MAPUNGUFU ya maendeleo, Ni nyie mnatakiwa kutazama chama na mafanikio/mapungufu yake kwa jicho hilo la kutazama urithi mloachiwa mtauendeleza vipi kwa sababu SERA mnazotumia ni zile zile zilizoachwa hivyo mnatakiwa kujenga strategies bora zaidi ili mpate kuendelea mbele zaidi.
Hivyo yote uloandika hapo juu ni sawa na kusema hivi:- Hakuna sababu ya wanaCCM kumlaumu uongozi wa JK, isiipokuwa ni kutazama kafanya hiki hakikuwa sawa (mapungufu) na sasa nyie mnafanya hiki. Na ndivyo imefanyika wakati wote toka Mwinyi, Mkapa na hadi JK wote hawa wamekuwa wakipongezana kwa kazi waloachiana na kisha kutafuta njia strategies bora zaidi ktk kile watatachokifanya.. Lakini alilaumiwa Nyerere kwa sababu ya MAKOSA ya kiitikadi na sera zake zilikuwa tofauti kabisa na Ubepari kupelkea kushindwa kuleta maendeleo yaliyokusudiwa - somo hili hali apply!
Hivyo basi, tofauti kabisa na mtu asiyekubaliana na Itikadi na SERA, mtu asiyekubaliana na fikra nzima ya makusudio yanayotakiwa kufanywa, mpinzani wa mfumo mzima japokuwa lengo ni kufikia maendeleo, anaweza kabisa kukosoa makosa ya kiuongozi, sera, na hata kifikra ya upande wa pili. Kwa mfano wewe Muislaam hukubaliani kabisa na mafundiusho ya Kikristu (makosa) hivyo swala la kutolaumu Uongozi halihusiani kabisa kwani maendeleo yanayodaiwa kuwepo huyaoni kama ni mapungufu isipokuwa ni makosa na wanazidi kupotea. Hivyo kwa kila ushauri wako utakuwa against mafundisho ya Kikristu na vitendo vya viongozi wao ni sehemu kubwa na mifano ya upotoshaji.
Ushauri wako hapo juu kuhusiana na Dale haumhusu Regia, yeye ni mpinzani kiitikadi na sera za CCM na anaoyaona makosa, hivyo Rostam ni mfano mzuri wa sera zisivyoweza kufanya kazi na ana kila haki ya kuwaonyesha wananchi jinsi chama na wawakilishi wake walivyoshindwa kupeleka maendeleo kwa wananchi..Na ndio maana huwezi wala mafundisho ya Dale yasingeweza kabisa kutumika ktk Uijamaa vs Ubepari!
Swala la Maendeleo, Unataka mimi nikuonyeshe ni MegaWatts ngapi kaziongeza JK..Hivi kweli hii akili? Wewe kuzungumzia swala la dharura, kutoa tender kwa mashirika ya nje kuja kimu tatizo la Umeme kwa gharama kubwa kuwa swala la kujisifia? Yani wewe huna gari, lakini kwa sababu ya matatizo ya Usafiri unapokodisha gari unaona ni sifa kubwa ya kuwa na usafiri wa kukodisha kuliko yule mwenye Bajaj yake?..Umepanga nyumba Upanga, wewe mbora kuliko mwenye ardhi na nyumba yake Kariakoo! -
Hvi Kikwete ameongeza Megawatts ngapi zinamilikiwa na Tanesco au shirika lolote la ndani? au kawezesha vyanzo vipi vipya? - HAKUNA! isipokuwa wewe unahesabu mchango wa dharura, hali mali sii yetu kesho tukiwaletea za kuleta wanatupeleka mahakamani na kulipa kama kina Dowans, hii wewe unaona sifa?. Hivi kweli mtu unaweza jivunia Taxi unazokodisha na kuhesabu taxi hizo ktk maendeleo yako ya usafiri! - Nimechoka!...
Hayo mengine, wala sina sababu ya kuendelea kubishana - ni Ujinga!
FaizaFoxy,
Wewe mgumu sana kuelewa na sikuwezi maana una midomo miwili sintaweza shindana nawe...
1. Unapofanya makosa hakuna sababu ya kuendeleza makosa..
2. Wazee wangu wamenisomesha hadi form IV sawa, lakini kwa sababu nilikuwa nafanya vizuri na nashinda mitihani lakini kama ningekuwa sishindi nisingepita hata darasa la nne. Na mara zote watanisaidia ktk mapungufu yangu lakini kama siwezi kuelimika na nashindwa mitihani hilo halina msaada wa wazazi.
Labda nikupe funzo ktk maji yako wee mwenyewe. Mkiristu akisema ni makosa kwa mwanamme kuwa na wake zaidi ya mmoja na akatoa mfano wa waislaam aliowaona! Ni muhimu wewe ufahamu kwanza katumia imani gani, Pili, toa majibu ambayo yeye atayaelewa kwa kuhalalisha kitendo hicho na sii kutukana na kuzugumzia mapungufu ya kibinadamu kama sababu ya kuhalalisha ndoa hizo. Hivyo, soma swali kabla hujatoa majibu unatia aibu..
Haya ya kusema yeye (Regia) kafanya nini unakwepa ukweli na kuanza kushambulia upande wa pili kwa kutazama maisha ya mtoa hoja badala ya imani iliyotangulia.
Hutanielewa kamwe!... Kuhusu dini, nimekueleza tu jinsi ya kukabiliana na hoja za watu sina maana nyingineyo.1) Nadhani hapo umekubali ile sentensi ya Regia kuwa ni kosa, au?
2) Ndio maana nikakuambia dhamira haitawasuta ukiwa wamejitahidi na wamefikia walipofikia wakashindwa. Dhamira humsuta mtu pale ambapo hajafanya kabisa.
3) Huko kwenye dini kwa hapa hunipeleki lakini kwa kukujibu, huo mfano dhaifu, kwani hakuna katika biblia (kitabu cha wakristo) paliposema oeni mmoja tu.
Naona maswali yangu umeamuwa kuyawacha kama yalivyo na umekosa majibu. Si kosa lako ni ukweli na ukweli mara nyingi inakuwa ni vigumu kuukana. Kama namba moja hapo juu umekubali kuwa Regia kafanya makosa kwa kauli za kibaguzi, basi aombe msamaha kwa mara nyingine, kwani kauli zake za kibaguzi hapo nyuma aliziombea msamaha, na kama wewe unashindwa kumshauri Regia kuwa hizo kauli ni za kibaguzi na wewe ntakuweka katika kundi hilo hilo, ambalo nna uhakika wewe ni muungwana na halikufai (kundi la ubaguzi). Leo hii hata liwe ni jambazi la wazi wazi huwezi ukalibaguwa, ujambazi ni ujambazi na ubaguzi ni ubaguzi huwezi kumbaguwa mtu kwa rangi yake au dini yake au cheo chake au umaskini wake au utajiri wake au kwa kutokutenda kwake au kwa kutenda kwake, ingekuwa tunabaguwana kama anavyotaka Regia, basi pasingebaki mtu hapa Tanzania. Ni wengi wenye kufanya madhambi lakini hatuwabagui na kuwaambia mkatafute raia ya ughaibuni. Jee, huko ughaibuni ndipo walipo waovu? Kama ni hivyo basi hata wale Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania ni waovu? siamni kuwa ni hivyo.
Mkandara nakuelewa sana humu JF, miaka mingi sana tumekuwa pamoja (bahati mbaya id yangu ya zamani ilikula ban ya maisha) humu JF na mitazamo yako naifahamu sana, Sijawahi kuona ukiutetea ubaguzi kama unavyoutetea katika nyuzi hii, mpaka nafikia kujiuliza, huyu kweli ni yule Mkandara wa siku zote? Ina fikia wakati mpaka huwa hatujui u dini gani kwani hauko biased kwenye mambo ya dini, nakuasa mambo ya siasa yasikufanye mpaka ukawa biased kiasi cha kuutetea ubaguzi.
Nijibu kutoka ndani ya moyo wako kuwa yale maneno ya Regia niliyokuwekea rangi nyekundu sio ya kibaguzi na kwako ni sawa kabisa.
Haaa! haaa! Faiza Foxy namjua sana yaani kupita maelezo isipokuwa yeye ndiye hanijui ila kwa kupitia JF...Hapa anae faidi hili jukwaa ni mimi tu. Faiza namjuwa na Mkandara namjuwa na wao wanajuana lakini hawajui kama wanajuana. Haya mitoto ya mujini leteni vitu.
Hutanielewa kamwe!...
Sikia, swala hapa sii Regia kasema nini na yeye nani bali tunatazama tuhuma zake zina ukweli gani? kama kuna uongo ndipo tunaweza kumshambulia katika uongo alosema na kutoa facts ni zipi. Na nadhani huko nyuma tumekubaliana kwamba hali ya Igunga ipo sehemu kubwa ya nchi hivyo sii swala la Rostam kafanya bali ndio hali ya uongozi nchini..Lakini kisiasa, Regia ni Chadema na kaandika aloandika kwa kutazama kuzingatia tofauti zake kisera na CCM na kuyaweka ktk matunda waliyovuna wana Igunga... Hii ndio siasa bibie! huko ndiko alikotokea na binafsi nimemwelewa ktk hilo..
Rostam ni FISADI tena sii mdogo na amechafua hadi jina la chama chenu. Yawezekana ni mmoja kati ya watu walotukimbiza sisi kutoka CCM hivyo mtu kama huyu mimi siwezi kumuunga mkono hata kama angekuwa mweusi au blue. Kwa umaskini wa nchi yetu Rostam ni sawa na kina Mubarak au washenzi wengine woote wa kisiasa ambao wanatumia mamlaka waliyopewa kujipatia Utajiri mkubwa hali wakiwadhalilisha wananchi - Haipendezi.
Hili neno Dubwana ni kiswahili safi ambacho unaweza kumuita mtu yeyote mwenye roho mbaya ilopita hata mfano hata akiwa mweusi, maana dubwana halina rangi isipokuwa matendo yake. Na hakika ukifika Igunga na ukaona hali ya wananchi wake kwa uchungu unaweza kumwita Dubwana na kuomba bora angejivua hata uraia - I wouldn't say that but will understand one who dare to say that!
Ni lugha ya kawaida kabisa kwa waswahili na sioni tatizo. Maajabu nayoyapata hapa ni kwamba nyie waswahili tena vijana wa mujini ndio mnashinwa na ghadhabu za ajabu ajabu ktk mijadala ambayo majibu yake rahisi kabisa kuyajibu tena kwa ustaarab na ukaeleweka.
Haaa! haaa! Faiza Foxy namjua sana yaani kupita maelezo isipokuwa yeye ndiye hanijui ila kwa kupitia JF...
Hivi unawafahamu Mzee Kenge na Mama BP weye ?...mjini (hususan Kariakoo) tumezowea na tumekulia na wenye asili za mataifa mbali hukuti tunabaguana zaidi ya kutaniana "wee mwarabu, wee mdosi, wee mdengereko, wee mkavirondo". Hatusemi wala hatumwambii mtu ni Dubwana, kama ni dubwana basi limeumbwa na Mungu na yeye au wewe unaejiona si dubwana pia umeumbwa na Mungu. Sasa Dubwana ni lipi? ni lile linalovaa hata nywele za maiti au lile linalobaki na maumbile yake aliyoumbwa nayo? acha hizo..
Hapa anae faidi hili jukwaa ni mimi tu. Faiza namjuwa na Mkandara namjuwa na wao wanajuana lakini hawajui kama wanajuana. Haya mitoto ya mujini leteni vitu.
Zombaa, toka umerudi hatujatafutana? ni pm unambie ndio nani, au nipigie.
Duh, wanitafuta hivyo! haya bismillah kuwe na kheri tu...Zombaa, toka umerudi hatujatafutana? ni pm unambie ndio nani, au nipigie.