BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 ambapo kwa mujibu wa Muongozo, Serikali za Mitaa zimeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 145 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.
Hivyo, pamoja na shughuli nyingine, Serikali za Mitaa zina wajibu wa kuimarisha demokrasia katika maeneo yao na kuitumia demokrasia hiyo kuharakisha maendeleo ya wananchi. Kwa mantiki hiyo, msingi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hufanyika kila baada ya miaka mitano kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288. Uchaguzi utakaofanyika mwaka 2019 utakuwa wa sita tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa nchini Tanzania mwaka 1992.
Katika Uchaguzi huo, wananchi watapata fursa ya kuchagua Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Wenyeviti wa Mtaa, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, na Wajumbe wa Kamati ya Mitaa. Hivyo, kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni utekelezaji wa dhana ya ugatuaji wa madaraka ambayo inasisitiza Serikali kupeleka madaraka ya kisiasa kwa wananchi ili waweze kuchagua viongozi watakaowawakilisha katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Sasa ukiangalia jinsi hali ilivyo hapo mtaani kwako? unaona Mwenyekiti wa Mtaa wako anastahili tena kurudi kwenye hiyo nafasi?