Mwenyekiti Serikali ya Mtaa, Diwani, Mbunge na Rais wote CCM; vipi maendeleo mtaani kwako unayaona?

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Katika historia ya vyama vingi nchini, uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na uchauzi mkuu wa 2020 ulighubikwa na sintofahamu nyingi na kupelekea vyama vya upinzani kukosa uwakilishi wa kutosha ngazi ya Serikali za Mitaa na Bungeni.

Wote tulishuhudia wagombea wengi wa vyama pinzani wakienguliwa na mamlaka za usimamizi wa uchaguzi kwa sababu nyingi zisizokuwa za Kikatiba ambazo zingeweza kurekebishwa na kufanya uchaguzi kuwa wa ushindani. Uchaguzi ule wengi waliuchukulia kama uchafuzi tu.

Tukiacha na hilo,

Tulisikia kauli mbalimbali za viongozi wa CCM wakiwataka wananchi kuchagua wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka urais ili waweze kupata maendeleo ya haraka.

Kwa nyakati mbalimbali Hayati Magufuli alikuwa akisema kuwa hawezi kupeleka maendeleo yoyote maeneo ambayo wamechagua mpinzani, kwani ili sufuria liweze kukaa vizuri kwenye mafiga lazima yawe mawe matatu, ukiweka gunzi sufuria haliwezi kukaa.

Binafsi kata na jimbo nalotoka, baada ya uchaguzi wa 2020 hakuna maendeleo ya msingi yaliyofanyika. Zimejaa siasa za majitaka, viongozi wenyewe wanahujumiana. Mpaka mbunge wangu ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki alidai kuhujumiwa na wanaCCM ili kumgombanisha na wananchi. Kwa unafiki huu na migogoro hii, jimbo pamoja na kuwa na mafiga yote matatu ya mawe tumejikuta tukiendelea kubaki nyuma. Stendi yenyewe bado inasuasua.

Tukiwa tunaelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, unayaona vipi maendeleo eneo unaloishi?

Je, ni sahihi kuwa na viongozi wote wanaotoka chama kimoja?

Unashauri nini kuhusu chaguzi zijazo?
 
Mdee alifanya la maana sana kupinga udikteta wa Mbowe.

Mdee ni shujaaa, mwanamke wa shoka

Njaa ndiyo imemfanya mbowe kuanza kupokea ruzuku inayotokana na wabunge aliowaita haramu
 
Siasa za vile,na uchaguzi wa namna ile,haifai kabisa katika ulimwengu wa leo.Lazima watu wawe tayari kukubali mabadiliko kwa vitendo na bila hofu kabisa.
Uchaguzi wa kisiasa unatakiwa kuwa huru bila mizengwe yoyote,kwa sababu vyama vyote vipo kwa ajili ya ustawi wa watu.
 
Back
Top Bottom