Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Huyo Lisu unayemsifia amejaa hasira, jazba na majigambo mwanasheria msomi hana lolote
Yote hayo atatakiwa kujieleza kwenye kampeni ndugu.

Usilazimike wewe kuwalisha watu maneno kwamba kuna vingi vimefanywa.

Ndo mana nikasisitiza, endapo akipambana na mtu mwenye uwezo wa kujenga na kuvunja hoja kama Tundu Lissu, atakuwa na wakati mgumu sana kwenye kampeni.
msi
 
Hakuna tume huru hivyo atapita
Pammoja na kutowepo tume huru,Magufuli atashinda kwa jinsi alivyojitwisha miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa.
Mtu wa kuhakikisha inakamilika kwa wakati ni yeye tu.
Hakuna jinsi hasa hii miaka 5 ijayo.
 
Kwa hiyo anakamilisha kwa pesa yake?
 
Atakuja kijijini kwetu atuambie amejenga flyover daslam? Au amenunua ndege? Au amejenga SGR? Wakati huo huo ajira hakuna, ongezeko la mishahara hakuna, maisha yamezidi kuwa magumu. Unadhani tutamuelewa? Kama alikuja kipindi cha kampeni akatuahidi milioni 50 kila kijiji na akatuahidi kutujengea soko na miaka mitano ishapita hakuna kitu, unadhani atakuja kutueleza nini tumuelewe?
Atasema alinunua wabunge wa upinzani akawaingiza sisiemu
 
Naomba uwaze kama mtu mwenye akili timamu.Usijichetua ubongo kama CCM
Mtu mjinga mjinga utamshauri nini mpaka akuelewe?Nitatumia njia gani kuwashauri hao mamilioni ya watu?Kwa platform gani na nitatoa wapi resources?Na watanisikiliza kwa vile nina mamlaka gani??
Anamaanisha kuwashauri vyama vya upinzani, siyo mamilioni ya watu
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
Hatuna shida na porojo sie tunataka actions; sasa bank yenu tayari ina i-rank Tanzania kuwa ya uchumi wa kati.
 
This is bullshit thread
 
Hoja yangu imejikita kwenye ufundi wa kufanya kampeni. Na ukumbuke kampeni ndo mchezo wenyewe wa siasa.

Wewe unadhani Magufuli amefanya mengi kwa mtizamo wako, ila hayo unayoyaona ni mengi kwenye ulingo wa kampeni, story itakuwa tofauti sana.

Magufuli anatakiwa kuwa imara wa hoja kwenye kampeni, kampeni ni vita vya hoja.

Na ujuzi wa wapinzani kwenye kampeni unaweza kukufanya ukajuta hata kwanini ukiongozwa na Magufuli.

Ufundi wa kampeni
Umeibua swala muhimu sana kwenye kampeni, na ukweli una kawaida ya ubishi wa kufichika. Lakini hii point yako imekuwa ngumu sana kuwaingia Watanzania. Kote hata jana nilipita Uswaa/ Machame nikienda Upareni na swali hili lili ibuka , lakini watu wote wanakwambia waongeaji wazuri hawawataki kwao ni wanini ? wao wanataka matokeo. Na ambayo Magufulu anawapa.
 
Yaah kabisa ingepaswa mdahalo kufanyika 2015.

Nna imani kabisa midahalo ni njia nzuri sana ya kumsoma kiongozi, sijui kwanini Tanzania huwa haifanyiki hii kitu
Mwaka 1995 mgombea wa CCM, Mkapa alikuwa hoi dhidi ya Mrema lakini elimu yake na uwezo wake wa kujenga hoja ulimsaidia kushinda uchaguzi ule. Mkapa hakuwa anajulikana sana na wananchi kwasababu alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje lakini mpinzani wake aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu kwa hiyo alijulikana na kupendwa sana hasa na vijana lakini alishindwa uchaguzi. Nyota ya Mkapa iliyomsaidia kushinda ilijitokeza kwenye MIDAHALO ya wazi na wapinzani wake ambayo ikampaisha mpaka ushindi kwa sababu aliwafunika wote na kuinuka kidedea. Bahati mbaya sana pamoja na ushindi huo, CCM kikaogopa kabisa MIDAHALO kwenye kampeini za uchaguzi. Mkapa alikuwa wa kwanza na wa mwisho kushiriki! Kikwete pamoja na umahili wake wa lughà hakushiriki kwa sababu Chama chake hakikuafiki ingawa wapinzani wachache walishiriki. Magufuli pia hakushiriki kwa sababu hizohizo lakini yeye aliishia kufanya push-up jukwaani na kushinda so kwa kishindo.
 
Umeibua swala muhimu sana kwenye kampeni, na ukweli una kawaida ya ubishi wa kufichika. Lakini hii point yako imekuwa ngumu sana kuwaingia Watanzania. Kote hata jana nilipita Uswaa/ Machame nikienda Upareni na swali hili lili ibuka , lakini watu wote wanakwambia waongeaji wazuri hawawataki kwao ni wanini ? wao wanataka matokeo. Na ambayo Magufulu anawapa.
Suala la Magufuli kuleta matokeo bado ni subjective sana. Huwez kuwaaminisha watu wa huko vijijini kwamba Magufuli anapiga kazi kwa kununua ndege ambazo wengine wataishi watakufa hawatazipanda.
 
Kuna ukweli ambao tutaupinga kwa sababu siasa inatuamrisha tufanye hivyo, upinzani unataka uzungumze yale ambayo hayajafanywa.

Lakini hakuna sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania ambayo haijaona mkono wa Magufuli kwa hiki ama kile na maeneo mengi yameona karibu vitu vyote kwa pamoja.

Kila binadamu anafikiri kivyake na ana haki ya kusema kile ambacho anafikiri ni muhimu kuliko vingine. Ila kwa maendeleo ya pamoja yanayo wagusa wengi na kwa muda mfupi kwa Mkoa wa Kilimanjaro ni hii mara ya kwanza.

Siwezi kusemea mchango wa Rais Magufuli mikoa mikoa mingine ambayo sikupa bahati kuitembelea kwa hii miaka mitano.
 
Back
Top Bottom