Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,600
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia watu. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia watu ambayo ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi kuwa wa kipekee sana.

Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
 
Tulisumbuka kumjua Magufuli 2015, lakini leo hii tunajua tutapata nini kama akichaguliwa. Watanzania wanataka matokeo na sio maneno au ulevi. Muda wa kumtafakari umepita.
Hoja yangu imejikita kwenye ufundi wa kufanya kampeni. Na ukumbuke kampeni ndo mchezo wenyewe wa siasa.

Wewe unadhani Magufuli amefanya mengi kwa mtizamo wako, ila hayo unayoyaona ni mengi kwenye ulingo wa kampeni, story itakuwa tofauti sana.

Magufuli anatakiwa kuwa imara wa hoja kwenye kampeni, kampeni ni vita vya hoja.

Na ujuzi wa wapinzani kwenye kampeni unaweza kukufanya ukajuta hata kwanini ukiongozwa na Magufuli.

Ufundi wa kampeni
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!

Yote hayo atatakiwa kujieleza kwenye kampeni ndugu.

Usilazimike wewe kuwalisha watu maneno kwamba kuna vingi vimefanywa.

Ndo mana nikasisitiza, endapo akipambana na mtu mwenye uwezo wa kujenga na kuvunja hoja kama Tundu Lissu, atakuwa na wakati mgumu sana kwenye kampeni.
 
Hatutaki sijui Hoja sijui Usahihi wa kutamka Maeneo Mara Precision, Sisi tunataka kazi ipigwe Basi mtu akisema nataka Tujenge MELI mpya Ziwa Victoria inajengwa hatutaki Porojo na Usahihi wa kutamka maneno mtu wewe kazi kuahidi tu hakuna unachofanya!!!

Magufuli atashinda mapema Sana mkuu!!
 
Tulisumbuka kumjua Magufuli 2015, lakini leo hii tunajua tutapata nini kama akichaguliwa. Watanzania wanataka matokeo na sio maneno au ulevi. Muda wa kumtafakari umepita.
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
Hatutaki sijui Hoja sijui Usahihi wa kutamka Maeneo Mara Precision, Sisi tunataka kazi ipigwe Basi mtu akisema nataka Tujenge MELI mpya Ziwa Victoria inajengwa hatutaki Porojo na Usahihi wa kutamka maneno mtu wewe kazi kuahidi tu hakuna unachofanya!!!

Magufuli atashinda mapema Sana mkuu!!
Asante Naantombe Mushi, hawa wengine nilioorodhesha hoja zao hapa ni wajinga wa magu na ndio watanzania wengi walivyo, WAJINGA na ndio maana watampigia makofi dikteta na mkabila huyu bila kujua au kujali chochote. Ujinga ni kitu hatari sana!
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia watu. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia watu ambayo ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuhamisha upepo na hisia kwa wananchi kuelekea upande wa upinzani, kitu ambacho kitawapa wakati mgumu hata hiyo dola yenyewe ambayo italazimika kukilinda chama tawala kilichoshindwa kwenye kampeni.

Itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshundwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda.

Enzi za porojo na mapambio kwenye majukwa ya kampeni zimeshapita. Watu watakupima kwa matendo yako ya nyuma na unayokusudia kuyafanya.

Kwa bahati nzuri Matendo ya kimaendeleo ya Rais Magufuli yamedhihirika kwa kila mwananchi mwenye macho ...Matendo yake ni tiketi ya moja kwa moja ya kuingia kwa kishindo katika awamu ya pili
 
Hapa CCM wangeomba mjadala wa wagombea wengine yaani Membe,Lisu na Magufuli..hapa ndy patamu!mjadala uwe live kama Marekani !!
Hili ni moja linaloua upinzani.

Hawana taratibu za kitaasisi...wanaendeshwa na matukio.

Wangelikubali 2015 leo hii ingeonekana ni utaratibu na pasipo shaka mjadala ungekuwepo.

Ila hadhira yetu haihitaji mijadala....hatujafikia maendeleo ya chaguzi zetu kuamuliwa na mijadala na hoja.
 
Hili ni moja linaloua upinzani.

Hawana taratibu za kitaasisi...wanaendeshwa na matukio.

Wangelikubali 2015 leo hii ingronekana ni utaratibu na pasipo shaka mjadala ungekuwepo.

Ila hadhira haihitaji mijadala....hatufikia maendeleo ya chaguzi zetu kuamuliwa na mijadala na hoja.
Yaah kabisa ingepaswa mdahalo kufanyika 2015.

Nna imani kabisa midahalo ni njia nzuri sana ya kumsoma kiongozi, sijui kwanini Tanzania huwa haifanyiki hii kitu
 
Asante Naantombe Mushi, hawa wengine nilioorodhesha hoja zao hapa ni wajinga wa magu na ndio watanzania wengi walivyo, WAJINGA na ndio maana watampigia makofi dikteta na mkabila huyu bila kujua au kujali chochote. Ujinga ni kitu hatari sana!
Kampeni zikianza CCM wataumbuka sana. Ubaya hauna wema, uongo wao utadhihirika kwenye hoja.

Na wananchi sio wajinga kihivo.
 
Kama kuna mengi yamefanywa ya kipekee basi amani hivyo, na yule anaeona yaliyofanywa ni ya kawaida sana endelee kuona hivyo. lakini katika suala la uongozi kila kiongozi hufanya kwa nafasi yake, hata watangulizi pia walifanya kwa nafasi yao kutokana na hilo ndiyo hata yeye ameweza kufanya kwa nafasi yake maana waliotangulia walitengeneza njia ndo maana hata yeye ameweza kufanya aliyofanya.
kuelekea october, hofu yangu ni KIZAZI CHA SHULE ZA KATA kina hasira ipi huko mitaani kama kitakuwa na voting ID, na kwa kufuatilia comments zao kwenye social media. Toka 2010-2020 kizazi hicho ni kingi sana.
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
Atakuja kijijini kwetu atuambie amejenga flyover daslam? Au amenunua ndege? Au amejenga SGR? Wakati huo huo ajira hakuna, ongezeko la mishahara hakuna, maisha yamezidi kuwa magumu. Unadhani tutamuelewa? Kama alikuja kipindi cha kampeni akatuahidi milioni 50 kila kijiji na akatuahidi kutujengea soko na miaka mitano ishapita hakuna kitu, unadhani atakuja kutueleza nini tumuelewe?
 
Asante Naantombe Mushi, hawa wengine nilioorodhesha hoja zao hapa ni wajinga wa magu na ndio watanzania wengi walivyo, WAJINGA na ndio maana watampigia makofi dikteta na mkabila huyu bila kujua au kujali chochote. Ujinga ni kitu hatari sana!
Wewe nae ni CERTIFIED POYOYO haswah, sikia hatutaki harakati zisizo na kichwa Wala miguu n porojo za bei rahisi, tunataka UTEKELEZAJI, kumbuka huu ni Uchaguzi wa pili wa JPM na sio ndio anaanza pengine hata hoja yenu ingekuwa na mashiko lakini kwakuwa wote tumeshuhudia alichofanya Sasa unataka awe Fundi wa kuzungumza ili iweje mkuu!!!

Tatizo unajifanya unajua wakati kumbe unajua kabisa HUJUI!!!
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
Hakuna tume huru hivyo atapita
 
CCM utaratibu wao unajulikana. Campaign speech inapangwa let say kwa masaa matatu. Zinapigwa nyimbo za Marehemu Komba non stop na show kadhaa kutoka kwa wasanii kwa masaa mawili na nusu. Magufuli anapanda jukwaani kwa nusu saa tu. Mwisho wa mkutano.

Siku ya uchaguzi, Tume inafanya yake. Msijidanganye na the so called “ujengaji hoja jukwaani”. Hizo hoja zilipaswa kujengwa kabla ili tupate Tume iliyo huru kabisa. Kwa sasa hakuna namna wanayoweza kumtangaza mwingine zaidi ya Magufuli. The earlier you get used to this, the better for you
 
Wewe nae ni CERTIFIED POYOYO haswah, sikia hatutaki harakati zisizo na kichwa Wala miguu n porojo za bei rahisi, tunataka UTEKELEZAJI, kumbuka huu ni Uchaguzi wa pili wa JPM na sio ndio anaanza pengine hata hoja yenu ingekuwa na mashiko lakini kwakuwa wote tumeshuhudia alichofanya Sasa unataka awe Fundi wa kuzungumza ili iweje mkuu!!!

Tatizo unajifanya unajua wakati kumbe unajua kabisa HUJUI!!!
Aache ukabila, udini, ubabe, udikteta, ubaguzi na mambo ya kienyeji.
 
Back
Top Bottom